MASKINI:PAPII KOCHA ATUMA TENA UJUMBE MZITO KWA RAIS KIKWETE YA KUOMBA KUACHIWA-JE RAIS ANAZISOMA KWELI AMA?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MF/NA: 836'04 Johnson Nguza
(Papii Kocha) Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam
Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania

YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga. Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya kiMUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais....Nakuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais, kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu. Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo, na ukweli kutoka moyoni sikufanya kosa hilo.

Si mimi, baba yangu Nguza wala ndugu yangu yeyote aliyefanya kitendo kile. Lakini wenye mamlaka wakatuona tuna hatia na kuamua kuteketeza kizazi chetu gerezani.

Natamani kiama ifike ili mwenyezi Mungu aweke wazi ukweli wote uliojificha nyuma ya pazia. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi. Lakini pia sisi ni binadamu wenye nafsi na miili kama wengine. Waliotumia mamlaka yao kutuweka gerezani nao ni binadamu pia, wenye miili na nafsi.

Ipo siku nafsi zetu zitapaswa kutoa hesabu ya tuliyoyafanya hapa duniani. wakati huo miili yetu tunayoitumia kunyanyasa wanyonge itakuwa imeoza mavumbini.

Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu. Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu. Mungu akubariki. Wako mtiifu

Mfungwa NO:836'04 JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

24 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. imenifanya nikalia. Its hurt soo Much

    ReplyDelete
  2. dah it hurts much when punishd 4 wat u didn't do

    ReplyDelete
  3. dah it hurts much when punishd 4 wat u didn't do

    ReplyDelete
  4. Mungu atawasaidia tu ndugu zangu tumuombe mungu CHADEMA ichukue nchi mwaka2015 mtatoka tu, watu wengi wanajua kabisa kua mmefungwa bila hatia kwa kesi ya kusingiziwa. Kikwete hawezi kuwasamehe ata umlambe miguu

    ReplyDelete
  5. Kijana Mungu anakuona, kama kweli hujafanya hilo kosa basi nina imani mheshimiwa raisi atafuatilia suala lako na kukuondoa hapo gerezani...Lakini endelea kumuomba Mungu na ujumbe zambi zako...nina imani utakuwa huru kabisa!

    ReplyDelete
  6. Mh.jk amesikiliza kilio chenu! Mtkuwa huru punde tu!

    ReplyDelete
  7. kama kweli hamkufanya ni unyama sana kufungwa maisha gerezani!bt MUNGU mkubwa anajua yote ataamua kwa haki!Poleni sana.

    ReplyDelete
  8. Maisha ya dunia si kitu laiti ungejua uendapo ungependa kumsaidia kila mwenye shida sehemu inaweza kukufanya hujisahau Upo duniani kwa kazi gani na kwa mda gani Fanya ulichotumwa kwanza ili upate nafasi ya kufanya chako baadae . Mungu atawasaidi amen.


    ReplyDelete
  9. Machozi yamenitoka huzuni imenijaa usoni natamani kusaidia ila sijuwi pakuanzia! Kweli unaiteketeza familia ya mtu kwa vile umeamua tu!!?? Binadam tunajisahau sana, Mungu baba sikia vilio vya wanao Yarabii.

    Papy please kaka yangu tumia muda huo wewe na familia yako kumlilia Mungu trust me huwa hamtupi mjaa wake...mitikhani mnayo pata na familia yako ni migumu lkn Mola hawezi kutupa mitikhani ambayo hatutoiweza !

    I pray for y'all inshaallah kheri.


    Onyinye.

    ReplyDelete
  10. So sad...4sure huwa nikiusikia ule wimbo wa Seya wa mivalo nimzuri but huwa naumia zaidi..! INSHA'ALLAH ZIDI KUMUOMBA MOLA NACC BINAADAM WENZIO TUNAKUOMBEA SN! M'MUNGU ATUTIA WEPEC.... Cna uwezo zaidi ya dua mm ni Mtu wa kawaida tu...pole PAPY WE ALWAYZ LOVE U.

    ReplyDelete
  11. innocent safari22 July 2013 at 09:02

    Kwa mungu yote yanawezekana muomben mungu sana atawaweka huru
    Kama alivyowaweka paulo na sila huru.polen sana wanadamu

    ReplyDelete
  12. very Sad, Wallah. Mr. President hana budi kuwafikiria kina Nguza katika hili.

    ReplyDelete
  13. HILI JAMBO LINA SIRI NZITO SANA NDANI YAKE. YANASEMWA MENGI ILA WAJUAO UKWELI NI WAKINA NGUZA, NA MPANGAJI NJAMA ZA KUWAANGAMIZA JELA KAMA KWELI HAWAKUTENDA KOSA. AIDHA MUNGU NDO ANAJUA ZAIDI NA AMESHAANDAA HUKUMU KWA WAHUSIKA.

    PAPII AFANYE NINI?
    KWA VILE ANAJUA UKWELI ULIVYO AWE MUWAZI KWA WATANZANIA, ASEME KISA NA UKWELI HUSIKA. KAMA KUUMIA AMESHAUMIA SANA KWAYO ASIFICHE SIRI HII, HEBU AMFICHUE MBAYA HUYO ILI WATANZANIA WAMJUE NA BILA SHAKA WATACHUKUA HATUA ZOZOTE.

    ReplyDelete
  14. wengi walotoa maoni ni wanaume kwa sababu hajui uchungu wa uzazi

    ReplyDelete
  15. papi mkhaswaaaaa ukweli na uwazi ndio unao takiwa.cha msingi toeni ukweli woote wa tukio sisi wananchi na watu wahaki za binadamu tutafatilia kwa kina.kama hukumu ishapita.ila muamuzi wa kweli na haki ni mungu

    ReplyDelete
  16. mungu amesikia kilio chenu na hakika atafanya njia..

    ReplyDelete
  17. Chadema ntawapa kura yangu nikiamini mtawasaidia hawa ndugu zangu,la cvyo ntatenda kitendo walichocngiziwa wametenda.

    ReplyDelete
  18. yani kama hawa jamaa hawakufanya vile kwakweli MUNGU atawalipia, dunia sio nyumbani kwetu tunapita tu

    ReplyDelete
  19. hata kama sio yeye nina uhakika p utatoka tu !!mungu akulinde

    ReplyDelete
  20. nafikiri siku wakiachiwa wapenda haki wengi watafurahi sana pia jambo hili linatakiwa lifanyike mapema kwani uhai wa siku hizi ni wamagumashi tunaweza kuja sikia hapo tena duniani huku tunaimba atolewe atolewe kila siku kila mtanzania ananung'unika kivyake mh.jk wahurumie nakuona ni mtu mwenye huruma na ni mtu wa watu tusisubiri mpaka wafie gerezani then ndio tunashtuka watanzania inawauma lakini siku wanafia gerezani itawauma zaidi na waliofanya hivyo malipo tyao yako hapahapa

    ReplyDelete
  21. INNA LILAH WA INNA ILLAH RAJIUN

    ReplyDelete
  22. Mh.muonee huruma kwani nae ni binadam kama wewe

    ReplyDelete

Top Post Ad