MASOGANGE BALAA JIPYA,MAHAKAMA YAMFUTIA DHAMANA ARUDISHWA LUPANGO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

HUKU  akiwa hajui nini hatima ya kesi inayomkabili ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini, Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ amepata balaa jipya,GUMZO LA JIJI lina taarifa kamili... 
   

 

                          Dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo nchini humo, Masogange na mwenzake aliyekamatwa naye, Melisa Edward wamefutiwa dhamana hivyo wamerudi tena rumande.
Agnes Gerald ‘Masogange’.
KWA NINI DHAMANA IFUTWE?
Habari zinadai kuwa, dhamana za wawili hao zimefutwa kufuatia kuhisiwa kwamba wana mpango wa kuondoka nchini huko kinyemela na kurejea Tanzania, jambo ambalo limetafsiriwa kama jaribio la kuikimbia kesi hiyo.
“Unajua huku Sauzi si kila mtu anawaonea huruma Masogange na Melisa kwa tatizo lililowapata, sasa utakuta maskani mtu anaropoka vitu vya ajabu pengine vya uongo bila kujua kuwa si kila mtu anayesikiliza atayaachia hapohapo, wengine ni ‘mainfoma’ wanayafikisha mbele.

“Hicho ndicho kilichomtokea Masogange, wakati baadhi ya watu wakiwa kwenye mchakato wa kumsaidia ili kujua jinsi gani kesi yake itakwenda haraka, wengine wanakwenda kuongea mambo ya ajabu kwa watu wao wanaowatuma kuwapelekea taarifa, eti kuna watu wanajipanga kuwatorosha, si sheria ikafuata mkondo wake.
“Hii inatupa wakati mgumu sisi tuliokuwa tumsaidie, mara kwa mara tunaitwa na kuhojiwa na jeshi la polisi. Ndiyo maana dhamana yao imefungwa, ukiangalia nini kilichosababisha ni maneno ya uongo yanayotokea maskani,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake.

MASOGANGE AKAUKA MITANDAONI
Licha ya kukumbana na kesi ya madawa ya kulevya, Masogange aliendelea kutumbukiza picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kuzielezea, lakini baada ya kufutiwa dhamana amekauka mitandaoni kwa picha za karibuni.
“Nyiye si mnaona, siku hizi haposti tena picha zake mpya kama palepale katikati baada ya kukamatwa. Siku zile alikuwa nje kwa dhamana, sasa yupo rumande hawawezi kumwachia akacheza na simu,” kilisema chanzo.

WABONGO WALIOJITOLEA FEDHA KUMWOKOA WASIKITIKA
Baada ya staa huyo kutiwa nguvuni Julai 5, mwaka huu, baadhi ya Watanzania waishio Bongo na kule Afrika Kusini walidaiwa kuchanga fedha kwa lengo la kumsaidia mrembo huyo lakini kufuatia kuvuja kwa taarifa za kufungwa kwa dhamana yake, wamekosa nguvu na kusikitikia kitendo hicho.
Kamanda Nzowa.
SHERIA ZA AFRIKA KUSINI NA TANZANIA KUHUSU ‘UNGA’ SI SAWA?
Inadaiwa kuwa, nchini Afrika Kusini mtu akikamatwa na ‘unga’ anaweza kuwa nje kwa dhamana wakati kesi yake ikiendelea kusikilizwa mahakamani, Tanzania mtu akinaswa na unga kesi inasikilizwa akiwa rumande.

POLISI HAWAKAUKI NYUMBANI KWAKE
Habari kutoka vyanzo vya hapa Bongo zinadai kuwa, askari polisi (kituo cha kazi hakijajulikana) wamekuwa wakifika nyumbani kwa msanii huyo, Kijitonyama, Dar na kuwauliza mambo kadhaa majirani.
“Jamani ishu ya Masogange vipi? Maana hapa mtaani kuna polisi wamekuwa wakija mara kwa mara na kumuulizia kama yupo. Wao hawajitambulishi kama askari lakini watatu kati yao wamebainika ni polisi,” kilisema chanzo hicho.
Kiliendelea kudai kuwa, Julai 20, mwaka huu alifika askari mmoja na kuuliza majirani kama wamewahi kumwona mwanaume mrefu, mweupe akiingia kwenye nyumba ya Masogange.
“Julai 20 alikuja afande mmoja, akawauliza majirani kama kuna siku yoyote ambayo mwanaume mrefu, mweupe aliingia kwa Masogange, akajibiwa hajawahi kufika mtu wa aina hiyo.
“Ndiyo maana nikauliza kesi yake vipi kule Bondeni (Afrika Kusini)? Ila kuna kitu nilikisikia kwa baadhi ya watu kwamba kuna ndugu yake atakuja kuhamisha vyombo vyake kwa sababu wanajua kesi itachukua muda mrefu,” kilisema chanzo.
Masogange.
KUMBUKUMBU
Julai 5, mwaka huu, Masogange na Melisa walinaswa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo mjini Kempton Park, Afrika Kusini.
Ilidaiwa kuwa thamani ya mzigo huo wenye kilo mia moja na hamsini ni shilingi bilioni moja na laki sita...

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii biashara ni hatari sana na tena ukwa mshabiki wa kufatilia ni kina nani wanahusika walahi utauliwa kabla ya siku si zako. mm namfahamu dada mmoja mumewe alikuwa ni punda. basi kila siku safari za uingereza na australia. basi mwanaume alikuwa ana hela huyo acha. nikimuuliza dada yangu shemeji anafanya biashara gani dada yangu ananijibu anauza batiki a mashati ya vitenge ulaya. mm nasema moyoni moyoni mmh haiwezekan. kwan hata mwaka ulipita siku akasafiri kwenye biashara yake ya mashati ya vitenge na batiki. wenzake wasipige simu australia. wakakamatwa na wako nadi hadi leo hiyo ilikuwa 2010 mwanzoni. basi huku kwa dada yangu acha aanze kutapatapa. kila siku nyumbani kwake wanaenda mapolisi. wengine si mapolisi wengine ni wezi. siku moja nakwambia akapigiwa simu na mtu asiye mjua. akamuuliza una shida gani? basi dada yangu akasema shida yake. yule jamaa asiyejulikana akamwambia dada yangu ammpe account number yake akienda bank atakuta hela na hizo hela akishazipata asimtafute tena na wala asiwe na wasiwasi mumewe atatoka tu na akaambiwa ile simu card aidestroy. basi dada yangu akafata maelekezo kesho yake kweli kwenda bank akakutana na kitita chake. kwa hiyo ndugu zangu hii nchi ishaliwa. tunaongozwa na mafisadi na wauza madawa ya kulevya. ww unafikiri Lowassa anapata wapi hela za kutoa misaada kila leo? mm ndiyo maana huwa najisemeaga watanzania waliobahatika kuwa nje ya nchi wakawa na maisha yao wakakae hukohuko hata kama unachamba vibibi au unabeba box mara mia kuliko kuja nchi watu wanajidai ooh mali asili nying wakati wanafahidi wachache wenye roho za tamaa ambao hawaridhiki. basi ibene aau fanyeni hayo mauza mauza tengenezeni barabara, rekebisheni miundo mbinu ya maji hata umeme. tumieni hizo hela haramu na za wivu kufungua biashara na muajiri vijana wanaotangatanga mitaani. basi mnajikusanyia hela kwa uchoyo na ubinafsi uliopitiliza. utafikiri hamna watoto. ILA ALL IN ALL KARMA IS BITCH. Kama haitakukumba ww jua kwa njia moja ua nyingine kizazi kitalipa tu. VIONGOZI MBULULAS WA TANZANIA. very stupid utafikiri wakienda ulaya na amerika sijui hawaoni hayo maendeleo ya wenzetu mm nachukia sana.

    ReplyDelete

Top Post Ad