NATUMIA UANAMKE WANGU KUFANIKISHA MAMBO YANGU KAZINI- JE NIKOSA?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nakubali im guilty as charged pia kwenye hii shutuma!!!!!!! Ila nimekuwa najiuliza ni Zambi au sio zambi? Ni sahihi au sio sahihi?
Kuna hii tabia ya mdada au mmama unatumia uanamke (feminine ways) wako kujifanikishia mambo yako kazini. Sasa kwenye ushindani unatumia uanamke wako kuchakachua outcome ili ikufeve wewe.


Mfano sisi watu wa sales n marketting kila mtu anakuwa na portifolio ya clients wake anaowahudumia na team yake. Afu ushindani individual, na as a team ni mkubwa sanaaa! Bonus, commissions, na incentives zinahusika sanaaa kwa mshindi. Sasa basi full kutoana roho!

Hapo ndo feminine ways zinapogeuka silaha kuu kwa clients huko! Watu wanajitoa mhanga tu! Chezea bonus na promotion weyeeee! Huku kwetu hata uwe na masters 100, kama huperform wonders promotion utaisikia hewani tu! Uje na diploma uje na masters mfumo ni pyramid lazima uanzie from roots. Bosi wako kuwa Diploma wewe masters 2 sio jambo la kustua. Sasa basi mpaka tunalogana ili kuperfom na kupata nyota! If you want a promotion show u deserve it!

Katika mazingira hayo nikakutana na client mmoja hivi, tena Mchagga mwenzangu, na kijana mwenzangu tu! Anasimamia biashara za Dingi yake, ila shule kidogo alikimbia umande! Sema si unajua tena kama kampuni ya Dingi yako unakuwa bosi tu automatically n u can make major decisions kwa maslahi yako! Dady will forgive you! Nili itrojuziwa na Zombi langu flani hivi. Tena Zombi likamwambia huyu dada bwana mpe ile contract, ni shemeji yako. Akakubali.

Kwenda, fogo akanishobokea, wakati anajua mshkaji wake ni Zombi langu, i really acted professionally mwanzoni, nikamkataa, na kumwambia taratibu za kazi zinanibana (Afu nilikuwa simzimii wala nini pia ) He isnt a guy that takes No easily! Akanifanyia UMAFIA na kutaka kuninyima contract na kuwapa competitors wetu! Chupi ilinibanaje!

Ikabidi nitumie Backup plan ya kuwa sweet n charming kwake. Napendezajee kila nikienda pale, na trip za kwenda kumlamba miguu zikaongezeka (Kazi zingine za kitumwa sanaa) It worked! Akanipa contract. (It seems he had longterm plans na mimi, za kuwin my heart genuinelly sio kwa kutumia contract kama silaha) We became friends! Akaniunganisha na watu wengine wakubwa zaidi yao, na wana madeal manono manono. (U sichezee power of networking kabisaa) Hadi kuna watu walinishinda kabisaa, akanipatia hizo contract.

I must say soon baada ya kukutana na huyu kaka my career life imebadilika sana. I was nobody nimegeuka tishio. Nimeshinda in a row miezi kibao tena kwa gap la hatari. (Kwangu its a big deal coz hii kazi sijasomea, nimejilobby lobby tu! Sina cheti hataa! So ningevurunda wangenipeleka kwenye profession yangu!) Saivi sina mpinzani! Na pia nimekuwa na amani moyoni.

Hakuna cha buree. Tatizo kwenye portifolio yangu 70% ya major clients kanitafutia huyo kaka. Sasa siku hizi ANANIKERAAAA! Akipiga simu ananiita laazizi, sweety, mambo gani sasa hayo? A nanitokea live live na kunikosesha raha! Nabakia kumkwepa tuu. Na yeye gaidi, nimeumwa dada mwengine ndo anawaservice amedown size volume, hadi nirudi. Nyama kweliiii!!!!!!! Nikifikiria kumtosa, hadhi yangu itashukaje sasa! Narudi kuwa NO BODY!!!!!!! Napambana nae hivi hivi. Ila mwisho wake sio mzuri. Najuuuta kumfahamu!

Afu watu wamegundua natumia uanamke wangu na usista duu kuclose deals ndo maana nashinda! They even assume the worst about me hasa wanaume niliowashinda. (Majungu ya ofisini si mchezo) Ila mbona nina clients wamama tu! Perharps my selling skills are extra odinary! Au nina nyotaaa! Hihihihiiiiiiiiiiii!

Eti jamani wana jamvi, mtu afanyaje, usipotumia feminine skills, utashangaa mwezi unaisha hujaclose hata dili moja!!! Your career life will be in smokes! Afterall Client mwenyewe kajiingiza kingi, kuassume kuwa if he gives you the deal there might be something more. Akija kujua hakuna lolote its too late!

Ila tatizo dunia ndogo hii! Watu wanajungua mimi nawapuuzia, siku unaolewa wanamwambia mumeo huyu dada tulifanya nae alimaliza wateja wote! Hatari! Mumeo akifatilia kweli walikuwa wateja wako wazuri! SI UTRATRA HUO!!!!! Ataamini lipi? Na kweli wengine wanpeleka mambo next stage willingly ili tu kuwachuna clients coz wakogi loaded with cash. Lakini si unajua tena Akioza mmoja mnaonekana wote baaaaaass! Kazi hii unakuwa huaminiki kama bar maid au secretary.


Source:Jamii Forums
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole ccta ndo maisha uliyoyachagua ili umake life na utaki kushushwa au kujishusha kuwa mpole endelea kutumia uanamke wako

    ReplyDelete
  2. innocent safari21 July 2013 at 21:11

    Mbio za sakafuni huishia ukingoni.ni bora ungechagua kuishi maisha ya kawaida

    ReplyDelete
  3. Hakuna jipya chini ya jua... yote yapo na yanafanyika duniani kote.. ndipo ilipo kuja semo ile ya maisha ni mapambano...

    ReplyDelete
  4. basi sema najiuza!!acha kuzunguka!!ila biashara yako ni kama ile barter trade system

    ReplyDelete

Top Post Ad