PICHA ZA MTANZANIA ANAYE TEMBEA KWA MGUU KUTOKA MBEYA MPAKA DAR

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Anakwambia safari yake ya kutembea kwa mguu kutoka 87.8 Mbeya mpaka Dar es salaam anaiita Uzalendo Tour kuisupport Taifa Stars na anategemea baada ya kuimaliza, watu wengi wataiunga mkono timu ya taifa Taifa Stars.
Anavyotembea kwa sasa anakutana na watu wengi sana na watu wengi wamekua wakimpigia simu baada ya namba yake kutajwa hewani Clouds FM, wengine amekutana nao njiani na wamekua wakimpa vitu mbalimbali vikiwemo viatu na nguo mpya.
Katoka Mbeya saa kumi alfajiri akafika Makambako saa moja na dakika 19 akiwa tayari katembea kilometa 186, akachukua gari mpaka 92.9 Iringa mjini kwa sababu ilikua imeshakua usiku tayari… akachukuliwa na gari la Wambura mdau wa Power Breakfast ya Clouds FM na kumuacha Iringa mjini alikolala mpaka asubuhi na kuianza safari tena.
Anakwambia saa nane kamili alikua anauanza mlima Kitonga na akaumaliza kwenye saa tisa na dakika kadhaa, baada ya hapo alitembea mpaka kitongoji cha mwisho kabla ya kuianza Ruaha kisha akachukua gari mpaka Morogoro mjini kwa sababu ilikua usiku tayari,  ameamkia 88.5 Morogoro mjini na sasa anakuja 88.5 Dar es salaam.

Anasema hii ni idea aliyokua nayo kwa muda mrefu sana lakini akashindwa kuifanya kutokana na kukosa mda ila anamshukuru sana Gerald Hando wa Power Breakfast @Cloudsfm ambae amemsaidia sana kufanikisha hii safari.
Sio sehemu zote anatembea kwa mguu, usiku ukiingia inamlazimu apande gari.

Source:Millard Ayo
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Innocent safari13 July 2013 at 07:35

    Safi sana!!! Vijana kama hawa wanahitaji kusapotiwa.anastahili kupewa tuzo nakuwekwa ktk record za mashujaa

    ReplyDelete
  2. wewe jembee!!

    ReplyDelete
  3. Mbona sielewi,kama kaamua kutembea kwa nini apande gari?

    ReplyDelete
  4. Alitakiwa atembee kwa mguu kweli na asipande gari hapo danganya toto

    ReplyDelete

Top Post Ad