TANZANIA TURUDISHE MAJESHI YETU NYUMBANI-TUNATUMIKA KAMA CHAMBO KWA VITA ZISIZO TUHUSU

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nikiwa kama mtanzania mpenda Haki na Amani ninahuzunishwa sana na taarifa za kukamatwa, kutekwa, kujeruhiwa na kuuwawa kwa askari wetu wa JWTZ waliopo sehemu mbalimbali duniani wakipigana vita visivyotuhusu sisi watanzania moja kwa moja.
Ni huzuni kubwa sana kuona vijana wetu wa kitanzania waliopo jeshini kutumika kama chambo vitani katika nchi nyingine. Tanzania tusijifanye ni wazalendo wa nchi zingine wakati wenye nchi zao wenyewe hawazijali. Zipo namna nyingi bora zaidi za kuleta amani duniani kuliko kupeleka majeshi ya kupigana vita.

Mpaka sasa bado sijaona faida ya moja kwa moja kwa nchi yangu katika vita hivyo.
Tanzania kwa sasa imepeleka vikosi vyake katika nchi za DRC, Sudan nk.

Ninatoa ombi kwa serikali ya Tanzania kuwarudisha haraka askari wetu nyumbani waje kulinda mipaka yetu, misitu yetu, Tembo wetu, Makazi yetu, Mali zetu na maisha ya watanzania. Popote pale mtanzania mpenda Haki na Amani tuungane katika hili katika kupiga kelele na kushinikiza.


Source:Jamii Forums
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuna mambo namaamuz yanayofanywa naviongoz wetu YANAUMIZA sn!!! Cjui wanatuchukuliaje?!?! R.I.P Mwalim Nyerere. 4me tutaheshmiana next uchaguz.. yanini kulazimisha kulalia godoro lenyrkunguni na jamvi lipo?!?.....dawa yenu tunayo.....

    ReplyDelete
  2. Samahani mtoa mada ila nadhani kwa hilo unalosema ni sawa na kujitoa ndani ya umoja wa mataifa je ikitokea mapigano tanzania ina maana misaada isije usiongee kwa kufata hisia zako kifo ni sehemu ya maisha na serikali ya tanzania haijipeleki yenyewe bali inaambiwa na umoja wa mataifa msilete siasa jamani kwa kila jambo nchi ngapi zinatoa majeshi yao kusaidia wengine wacha siasa za vibarazani ndugu yangu

    ReplyDelete
  3. Ningependelea serekali ikapeleka wanjeshi zaidi .kwani hiyo ndiyo kazi waliyo ajiriwa

    ReplyDelete
  4. Hawana cha kufanya mitaani zaidi ya kunyanyasa raia, waache wakafanye kazi yao si kulipwa bure na kupiga raia ovyo.

    ReplyDelete
  5. Usichokijua sawa na usiku wa giza uliza ni kwanini mpango huo upo duniani sio Tanzania tu..TUMEPOTEZA NDUGU ZETU WAKIWA WANATEKELEZA MAJUKUMU YAO...Africa inatakiwa tuache kujitenga na kujiiona sisi au wale ni bora zaidi au wale waathirka wa kivita ni wajinga... wangekufa wazungu kule mngesema wamefuata nini wachonganishi n.k. Africa itakombolewa na mwafrika tu...

    ReplyDelete

Top Post Ad