WAPENZI WANASWA AIRPORT DAR KWA DAWA ZA KULEVYA-MSICHANA NI MFANYAKAZI WA NDEGE

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la Polisi Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, linawashikiliwa watu wawili, wanaodaiwa kuwa ni mtu na mpenzi wake kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin kilo mbili  zinazokadiriwa kuwa  na thamani  ya  zaidi Sh90 milioni...Msichana inasemekana ni mfanyakazi wa shirika moja kubwa la ndege hapa Tanzania..
Mkuu wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa aliliambia gazeti hili jana kuwa watuhumiwa hao ambao mmoja ni mwanamke walikamatwa  juzi  saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Alisema watuhumiwa walikuwa wakisafiri kwenda Mji wa Bangkok Thailand kupitia Addis Ababa, Ethiopia ambapo walikata tiketi ya ndege la shirika hilo.
“Walipoanza kufanya ukaguzi watuhumiwa hawa walijichomeka katikati ya wenzao ndipo tulipowanasa na dawa hizo ambazo walizificha kwenye mabegi yao katikati ya nguo,” alisema Nzowa.
 Alisema  kuwa watuhumiwa hao waligawana dawa hizo kwani walipofanyiwa upekuzi na polisi walikutwa  kila mtu akiwa na  kilo moja.

Source:Mwananchi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad