WATHUMIWA WALIOKAMTWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA NA HONG KONG WAFUNGUKA NA KUANZA KUWATAJA WAKUBWA WAO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge Wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania kutoka jimbo la Kinondoni, inasemekana ametajwa na wafungwa wa kitanzania waliofungwa jela huko nchini Hong Kong kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.

Taarifa hiyo iliyomhusisha Mbunge huyo na mtandao huo mkubwa wa biashara hiyo ya madawa ya kulevya nchini Tanzania, ilitolewa katika barua maalum iliyoandikwa na mmoja wa Wafungwa katika magereza ya nchini Hong Kong ambapo inasemekana kuna wafungwa wa kitanzania wanaofikia 200.

Kati ya hao wafungwa 200 waliopo magerezani na vizuizini, 130 tayari wameshahukumiwa na 70 bado wanasubiri kesi zao kutajwa. Kuanzia Mwezi wa Tano mpaka wa Sita mwaka huu wa 2013, tayari Watanzania wapatao 50 wameshakamatwa na madawa ya kulevya wakati wakijaribu kuingia katika viwanja vya ndege vya nchi za China na Hong Kong.

Mbali na Hong Kong, pia kumekuwepo na taarifa mbalimbali za raia wa Tanzania ambao wamekatwa na madawa ya kulevya nchini Afrika ya Kusini na kwingineko duniani. Mmoja kati ya waliokamatwa na madawa hayo ni mwanadada mahiri wa Kitanzania ambaye alikuwa mrembo katika video mbalimbali za Bongo Flava anayeitwa Agnes Gerald au kama anavyojulikana na wengi kwa jina la Masogange.

Waraka huo wa mfungwa huyo wa Kitanzania pia umeorodhesha idadi kubwa ya wafanyabiashara wengine nchini Tanzania ambao ni wahusika wakubwa katika biashara hii haramu ya madawa ya kulevya.

Madawa hayo ya kulevya yanasemekana yanaingizwa nchini Tanzania kwa wingi kwa njia ya meli na boti mbalimbali yakitokea katika nchi za Pakistan, Afghanistan na nchi nyingine za Mashariki ya mbali.

Ni muhimu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha kampeni kubwa ya kuwakamata wahusika wote katika biashara hii na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, athari za madawa hayo zimezidi kuonekana sehemu mbalimbali nchini Tanzania na dunia nzima.

Soma barua iliyowataja wafanyabiasha hao wakubwa wa madawa ya kulevya nchini Tanzania hapo chini.




Kama ni kweli haya sasa ni majangazzzzzzzzzzzzz haswa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Balaa kubwa...mbona majanga?

    ReplyDelete
  2. Hii biashara ni hatari sana na tena ukwa mshabiki wa kufatilia ni kina nani wanahusika walahi utauliwa kabla ya siku si zako. mm namfahamu dada mmoja mumewe alikuwa ni punda. basi kila siku safari za uingereza na australia. basi mwanaume alikuwa ana hela huyo acha. nikimuuliza dada yangu shemeji anafanya biashara gani dada yangu ananijibu anauza batiki a mashati ya vitenge ulaya. mm nasema moyoni moyoni mmh haiwezekan. kwan hata mwaka ulipita siku akasafiri kwenye biashara yake ya mashati ya vitenge na batiki. wenzake wasipige simu australia. wakakamatwa na wako nadi hadi leo hiyo ilikuwa 2010 mwanzoni. basi huku kwa dada yangu acha aanze kutapatapa. kila siku nyumbani kwake wanaenda mapolisi. wengine si mapolisi wengine ni wezi. siku moja nakwambia akapigiwa simu na mtu asiye mjua. akamuuliza una shida gani? basi dada yangu akasema shida yake. yule jamaa asiyejulikana akamwambia dada yangu ammpe account number yake akienda bank atakuta hela na hizo hela akishazipata asimtafute tena na wala asiwe na wasiwasi mumewe atatoka tu na akaambiwa ile simu card aidestroy. basi dada yangu akafata maelekezo kesho yake kweli kwenda bank akakutana na kitita chake. kwa hiyo ndugu zangu hii nchi ishaliwa. tunaongozwa na mafisadi na wauza madawa ya kulevya. ww unafikiri Lowassa anapata wapi hela za kutoa misaada kila leo? mm ndiyo maana huwa najisemeaga watanzania waliobahatika kuwa nje ya nchi wakawa na maisha yao wakakae hukohuko hata kama unachamba vibibi au unabeba box mara mia kuliko kuja nchi watu wanajidai ooh mali asili nying wakati wanafahidi wachache wenye roho za tamaa ambao hawaridhiki. basi ibene aau fanyeni hayo mauza mauza tengenezeni barabara, rekebisheni miundo mbinu ya maji hata umeme. tumieni hizo hela haramu na za wivu kufungua biashara na muajiri vijana wanaotangatanga mitaani. basi mnajikusanyia hela kwa uchoyo na ubinafsi uliopitiliza. utafikiri hamna watoto. ILA ALL IN ALL KARMA IS BITCH. Kama haitakukumba ww jua kwa njia moja ua nyingine kizazi kitalipa tu. VIONGOZI MBULULAS WA TANZANIA. very stupid utafikiri wakienda ulaya na amerika sijui hawaoni hayo maendeleo ya wenzetu mm nachukia sana.

    ReplyDelete
  3. Ndo maana hata wale kinadada wawili waliokamatwa Africa kusini walipita na mzigo airport Dar bila kukaguliwa,na pamoja na aibu yote hiyo hakuna kiongozi wa serikali aliyechukua hatua dhidi ya wahusika.Sijui kama nchi hii viongozi wapo,wamelala au sijui ni vipi..

    ReplyDelete

Top Post Ad