WAZAZI WAUA MTOTO WAKIGOMBANIA CD YA MSANII "DIAMOND"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Vilio  na  simanzi  vilitanda Jumatano iliyopita Mwananyamala Kisiwani, jijini Dar kufuatia mtoto wa mwaka mmoja, Rahim Rajab kufariki dunia kwa kuangukiwa na watu watatu, akiwemo baba yake mzazi, Rajab Said..



Tukio la watu hao kumwangukia mtoto huyo lilitokea Jumatatu iliyopita na lilisababishwa na ugomvi mkubwa wa CD yenye nyimbo za mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ulioibuka ndani ya chumba cha kulala kati ya mama wa marehemu na mpangaji mwenzake aitwaye Aisha.


Akizungumza kwa machungu kuelezea tukio hilo, mama mzazi wa marehemu Rahim, Habiba Ally alikiri kuwa kisa cha kifo cha mwanaye ni CD tu.Akasema: 

" Kwa kweli hakuna kingine zaidi ya CD, naamini hivyo kwa kuwa mimi sikuwa na ugomvi wowote na Aisha. Tulikuwa tunaishi kawaida tu ukiacha mikwaruzo ya hapa na pale.” 

Akaongeza: Jumamosi iliyopita, Aisha alikuja ndani kwangu na CD zake tatu, ya Diamond, Kingwendu na ya Coast Modern Taarab. Alipomaliza kuangalia aliziacha, akaondoka zake.

“Jumapili mimi nikaenda nazo kwa mama zote tatu kwa ajili ya kuziangalia, tulipomaliza na mimi niliziacha huko. 

“Jumatatu usiku Aisha akaja kunidai, nikamwambia zipo kwa mama. Kwa kuwa anapajua anapoishi mama, si mbali akaenda kuzichukua zote tatu. 


Ajabu aliporudi tu, akaja tena kwangu na kusema hajapewa CD ya Diamond kitu ambacho si kweli na ndipo ulipozuka ugomvi wote huo hadi kusababisha kifo cha mwanangu.”

Akizungumza msibani juzi, bibi wa marehemu, Jamima Hassan alisema siku ya tukio alipigiwa simu na mkwe wake (baba wa marehemu) akamwambia kuna ugomvi nyumbani kwake unaohusu CD kati ya mkewe na mpangaji mwenzake ambapo bibi huyo aliamua kwenda kutatua ugomvi huo.

“Niliondoka muda huohuo kwani huyo Aisha alitoka kwangu kuchukua CD zake muda mfupi tu, sasa nilijiuliza ni CD gani wanazogombania?


“Nilipofika nilikuta ugomvi umepamba moto, baba wa mtoto na mume wa Aisha aitwaye Shaban Sangali walikuwa wameungana kumtoa nje ya chumba Aisha bila mafanikio. 

“Wakati naingia, Aisha alikuwa akitukana matusi mazito na tulipojitahidi kumtoa nje alitusukuma kwa nguvu. Ndipo yeye, mume wake na baba wa mtoto waliwaangukia watoto waliokuwa wamelala kitandani,” alisema bibi huyo.


Akaendelea: Tulipowaangalia watoto ambao ni mapacha, hali zao zilikuwa mbaya, tukaamua kwenda kwa mjumbe wa mtaa kuripoti, akatupa barua, tukaenda Kituo cha Polisi Mwinyijuma, pale wakatupa PF3 ya kuwapeleka Hospitali ya Mwananyamala ambako walilazwa kwa matibabu.


Bibi huyo alisema siku iliyofuata, Rahim alifariki dunia, ikabidi waende Polisi Oysterbay ambapo walifungua shitaka lenye faili kwa kumbukumbu No. OB/RB/1150/2013 MAUAJI.

Watuhumiwa katika RB hiyo ni Aisha na mumewe, Sangali ambao walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.


Majirani waliozungumza na mwandishi wetu  walisema wakati ugomvi kati ya Aisha na Habiba unatookea, mume wa Habiba alikuwa anarudi kutoka kazini, akakutana na kimbembe hicho.

Walisema aliingilia kati kuamua bila mafanikio. Wakati huo mume wa Aisha alikuwa chumbani kwake na amefungulia muziki wa redio kwa sauti ya juu hivyo hakujua nini kinaendelea kwenye chumba cha mpangaji mwenzake.


Ikaelezwa kuwa, kuna watu walikwenda kumgongea na kumwambia mkewe anapigwa na mume wa Habiba kwa kushirikiana na mkewe.


Ilibidi mwanaume huyo atoke mbio hadi chumbani kwenye ugomvi ambako alikuta baba wa marehemu akijitahidi kuwaamulia wawili hao bila mafanikio.

Habari zinasema mwanaume huyo aliingilia kati kuongeza nguvu lakini katika hali ya kuwalemea, Aisha aliwasukuma wote na kisha wao kuwaangukia watoto hao mapacha waliokuwa wamelala kwenye kitanda kimoja.


Katika hali ya kusikitisha, marehemu amemuacha pacha mwenzake aitwaye Rahima Rajab ambaye ni kulwa.


Wengi wanaamini kuwa maisha ya Rahima yangekuwa ya furaha zaidi kama Rahimu angekuwepo na kwamba itamsononesha sana akikua na kusikia mwenzake alifariki dunia kwa ugomvi wa mama yake na mpangaji mwenzao kisa ni CD ya nyimbo za mwanamuziki.
GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndo tatizo la uswhilin m2 auwez ukagomban kisa cd huy alikuwa na yake ila ameuwa bila kukusudia

    ReplyDelete
  2. Njama za ufreemason hizo,lazima kafara ili nyota ya platinum izidi kungara ng'aring'ari.

    ReplyDelete

Top Post Ad