WAZIRI SITTA "KUNA WABUNGE MIZIGO CCM"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema baadhi ya wabunge wa CCM ni mizigo kwani hata wakienda bungeni, hawachangii na wanabebwa na chama.
Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa, alisema hayo juzi jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Nyamikoma, Kata ya Busega Mkoa wa Simiyu ikiwa ni sehemu ya kampeni za kuimarisha uhai wa chama.
“Ukweli ni kwamba, baadhi ya wabunge wa jinsi hii hawatufai. Wanakwenda bungeni hawachangii, wanakwenda bungeni hawana hata hoja za kuchachafya upinzani, hawachangii, hawa ni mzigo,” alisema Sitta.
Sitta alisema licha ya aina hiyo ya wabunge, pia wapo wale ambao hawafiki majimboni kwao kukagua shughuli za maendeleo.
“Wapo baadhi ya wabunge, hawajawahi hata siku moja kwenda kwenye majimbo yao kuwatembelea wananchi waliowachagua... inawezekana hata wapiga kura wakawa wamewasahau. Hawa hawafai hata kuchaguliwa wakiomba tena kura,” alisema na kuongeza:
“Haiwezekani mbunge akakaa mjini na kushindwa kwenda kuwatembelea watu wake jimboni. Mbunge anakwenda jimboni kwa kuchungulia halafu wananchi wanamshabikia na kumpa kura?
“Rais Jakaya Kikwete amejitahidi sana kuleta mabadiliko, ameleta mafanikio ya uchumi na mambo mengi. Inatakiwa wabunge waende wakawaeleze wananchi maendeleo haya, inawezekana hawayajui lakini watu hawaendi majimboni, wananchi watayafahamu vipi haya maendeleo?”
Akizungumzia mchakato wa Katiba Mpya, Sitta alisema: “Kwanza kuna viashiria vya baadhi ya watu kuanza kuipinga Katiba mahakamani. Watu hao wasiungwe mkono kwani ndio wanaoanza chokochoko.
“Katiba tunayoitaka ni kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania na Watanzania na si ya wengine. Hivyo hatuna budi kila mmoja kutumia nafasi hiyo kuwasilisha mchango wake wa kuboresha kwenye Mabaraza ya Katiba.”
Aliwataka wajumbe wa Mabaraza ya Katiba watumie nafasi kuwasilisha hoja zinazojenga na wasiwe mamluki wa kuharibu mchakato mzima.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa kauli kama hii:

    “Rais Jakaya Kikwete amejitahidi sana kuleta mabadiliko, ameleta mafanikio ya uchumi na mambo mengi. Inatakiwa wabunge waende wakawaeleze wananchi maendeleo haya, inawezekana hawayajui lakini watu hawaendi majimboni, wananchi watayafahamu vipi haya maendeleo?”

    Mzee Sitta, wacha kuwafanya watu mafara. Iwapo kungekuwa na maendeleo, wananchi wangefahamu tu, si mpala wabunge wakawaeleze huko majimboni. Toa hija nyingine, mzee. Maendeleo ya kuambiwa si maendeleo siku hizi. Hizi ni zama mpya, babu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeona, wananchi wa jimbo.la busega kawafanya wajinga kuwadanganya hadharani. Maendeleo huonekana kwa macho ya watu sio propaganda. Pia asidanganye watu kuwa uchumi umepanda, kwenye makaratasi sawa ila sio kwenye maisha ambayo wananchi wa chini tunayaishi. Kabali yenu 2015 tu.

      Delete

Top Post Ad