WEMA SEPETU JELA INAMUITA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KUNA kila dalili kwamba mrembo anayetamba kwenye filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au Madam jela inamwita na anatakiwa kufanya maombi ili kukwepa kifungo maishani mwake.
Hali hiyo inafuatia staa huyo kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena Jumatano iliyopita, pale alipopanda katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe jijini Dar kwa kosa la kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni meneja wa hoteli moja iliyopo Kawe Beach jijini Dar, Godluck Kayumbu.
Kabla ya  kupandishwa  kwa ‘pilato’,  staa huyo anayemiliki Kampuni ya Endless Fame alikuwa akisakwa na askari kwa siku kadhaa na kufanikiwa kuwapiga chenga za hapa na pale.

ANASWA AKIFUTURU
Hata hivyo, mbio zake ziliishia ukingoni Julai 16, mwaka huu, alipokamatwa saa mbili usiku akiwa anafuturu na wageni wake nyumbani kwake, Kijitonyama Dar.

MTITI KIDOGO
Askari saba walifika nyumbani kwake wakiwa ndani ya Land Rover ‘difenda’ kwa ajili ya kumkamata, hata hivyo walipata upinzani kidogo kutoka kwa mlinzi wa staa huyo ambaye alikuwa akizuia bosi wake asikamatwe ambapo ilibidi askari hao wakaze msuli na kutuliza mtiti uliokuwa ukitaka kutokea.

WEMA AGEUKA MBOGO, ALALA SELO
Baada askari kumfikia staa huyo, walimtaka kwenda naye kituo cha polisi kwa kutumia difenda walilofika nalo ambapo Wema alipinga na kugeuka mbogo kwa kudai kwamba hawezi kupanda difenda kutokana na hadhi yake.

Pamoja na askari kutaka kumpandisha kwa nguvu, staa huyo alipinga na ikakubaliwa apande gari lake aina ya Audi Q7 huku akiwa chini ya ulinzi wa askari.
Safari ikaishia Kituo cha Polisi cha Kawe ambako staa huyo aliandikisha maelezo na baada ya zoezi hilo akatupwa selo.

WEMA HAUOZI
Kama lilivyo jina lake, wema hauozi, staa huyo alipata dhamana saa 5 za usiku baada ya kudhaminiwa na msanii  mwenzake wa filamu, Kajala Masanja.
Kajala aliwahi kutolewa katika mdomo wa jela na Wema siku za nyuma baada ya kukutwa na hatia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar alipotakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 13 au kwenda jela, Wema alimlipia kiasi hicho cha fedha.
WAPAMBE FULL SHANGWE
Wapambe wa Wema waliokuwa wamejazana nje ya kituo hicho cha polisi, walilipuka kwa shangwe baada ya bosi wao kuchomolewa kutoka selo. Staa huyo aliondoka na gari lake lililokuwa likiendeshwa na meneja wa kampuni yake aitwaye Petit Man.

ATEMBEZWA KWA MIGUU
Julai 17, asubuhi Wema alirudi kituoni hapo na kuwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kupelekwa mahakamani kusomewa mashitaka yake.
Katika hatua ya kushangaza, staa huyo alitembezwa kwa miguu umbali wa mita 200 kutoka kituo cha polisi hadi Mahakama ya Mwanzo ya Kawe.
APANDISHWA KIZIMBANI
Wema alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake na Mh. Hakimu, Bernice Ikanda na kudaiwa kufanya vurugu, kushambulia kwa kumpiga makofi na kumtukana Kayumbu.
Mbele ya hakimu, Wema alikana mashitaka na hakimu aliiahirisha kesi hiyo mpaka Julai 31, mwaka huu.

IKO SIKU WEMA ATAFUNGWA GEREZANI
Kumbukumbu kutoka kwenye makabrasha yetu zinaonesha kuwa, mrembo huyo ni mtu wa majanga, mara kwa mara amekuwa akifikishwa polisi na mahakamani kutokana na ugomvi.

ALIVUNJA KIOO CHA GARI LA KANUMBA
Mwaka 2009, Wema alidakwa na Polisi Kituo cha Magomeni na baadaye kupandishwa katika Mahakama ya Kinondoni, Dar kwa Hakimu Emilius Mchalu kwa kosa la kuvunja kioo cha gari la aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, Marehemu Steven Kanumba chenye thamani ya shilingi milioni moja. Hata hivyo, Kanumba aliifuta kesi hiyo.

ALIMTISHIA MAISHA BOB JUNIOR
Kama vile haitoshi, mwaka 2011, Wema huyohuyo alikamatwa na Polisi wa Oysterbay jijini Dar na kufikishwa Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la kumtusi na kumtishia maisha mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rahem Nanji ‘Bob Junior’.
Katika kesi hiyo, Hakimu Mariam Masamalo alimtia hatiani Wema kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya shilingi 40,000 ambapo alilipa fedha hizo.
ALIMTUSI REHEMA FABIAN
Aidha, mara baada ya Wema kuachiwa huru mahakamani hapo alikamatwa tena na polisi kwa kile kilichodaiwa kumtusi Miss Kiswahili 2008, Rehema Fabian. Wema alipelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar kwa maelezo zaidi.

ALIMTUKANA MSANII
Aidha, Wema amewahi kulala kituo cha Polisi Oysterbay, Dar akiwa na mashoga zake, Kajala na Dida kwa madai ya kumshambulia mwigizaji mmoja wa Bongo, kwenye pati iliyofanyika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar. Kesi hiyo iliisha kwa mazungumzo nje ya polisi.
Imeandikwa na Musa Mateja, Mwaija Salum, Makongoro Oging’ na Shakoor Jongo.


Source:GLP


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu Wema toka afungue hiyo Endles fame cjackia katoa movie yoyote!! Zaidi ya skendo! Sielewi... Wapambe namashogazake ni wafanyakaz wake! Huyo meneja wake ss... Cjui Kadinda nikm bodgad wake... SERIOUS is that ofic or KIJIWE??? coz hatuckii kazi?!?!?

    ReplyDelete
  2. wema wamuweke ndani bila dhamana maana asikii sana ,Malaya yeye,ugomvi yeye,matusi yeye kujifanya anazo sana yeye sasa mtu gani huyo hatulii kila kona kaandikwa yeye ndo maana kawa jamvi la eageni kila anayemuitaji hujiendea kwa dau la umalaya si auze tu huko ohio ilielewekekuliko kuuzia nyumbani

    ReplyDelete
  3. naanza kukuchukia kwa maswala madogo sana the bs lady y lakini ebu epuka ugomvi wa uswazi kama wewe unajijua una hazi

    ReplyDelete
  4. KUMBUKENI BINADAMU HATUKO SAWA
    NDO UNAKUTA MLEVI KUPINDUKI
    MALAYA ASO HADITHIKA
    MAMA ANADANGURO NA ANA KAA NA WATOTO
    MWINGINE ANATUMIA MADAWA YA KULEVYA
    MWINGINE ANAWAVUTISHA WANAE
    MWINGINE ANATUKANA MBELE YA WTT
    BASI HII NI HALI YAVIUMBE KAMA WAKUTULIA KUNA SIKU ATATULIA KAMA NO NDO MAJAALIWA YAKE TENA
    KUNA WALOUMBWA NA HAYA NA WASO NA HAYA
    KIBAYA WEMA KAJULIKANA DUNIA NZIMA INAMAANA HIYO NDO TABIA YAKE ALOKUA NAYO KWENYE DAMU

    ReplyDelete
  5. Mkiangalia story na matukio ya Wema inamaana ndo atakuwa hivyo hivyo alikvyo
    BINADAMU WAMEUMWA KIAJABU NI KAMA VIDOLE HAVIFANANA,
    SOMA HIYO HABARI WAMEMBAKA MTOTO WA MIAKA 9 WAKAMCHOMEKA MIWA SASA HAO UTAWAITA NI KINA NANI ?
    KUNA ANAYEAMKA ANATAFUTA NANI AGOMBANE NAE ,KUNAANAYE AMKA HANA KULA ANAWAZA WAPI APATE YA POMBE , KIKUBWA MOLA AMJAALIE MEMA NA AMPE FAHAMU
    MIE SITHUBUTU KUTUKANA MTOTO WA MTU AU KUSEMA VIBAYA KUHUSU WEMA NAAMINI NA UZAZI AU NAWATOTO WA NDUGU .MUNGU AMPE FAHAMU TU
    MAMA YAKE ANAUMIA SANA

    ReplyDelete
  6. Exactly hapa ndo utaona kuwa POLISI wa kibongo awana kazi muhimu ya kufanya,Polisi sita na defender wanakwenda kwaajiri ya wema kwa jesi ya kumtukana mtu..NOSENSE BONGO POLISI..Kwanini kati yao sita wanne wasiende kushughulika na kutafuta Majambazi wanaoua watu na kupora kila siku au wauza madawa ya kulevya na Mafisadi walaji rushwa;Nadhani ingekuwa swala la muhimu kabisa...Inawezekana vipi Hawa Majambazi awakamatwi na wanaendelea kufanya matukio makubwa ya ya kinyama lakini hakuna taarifa yoyote kuhusu hawa majambazi na ukisikia wamekamatwa basi ni wananchi wenyewe ndo wameshughulika,Sasa kuna umuhimu gani kuwa na jeshi la polisi..Sometime start to think nyinyi POLISI NDIO MAJAMBAZI WENYEWE..Watoto wa wakubwa wanafanya mangapi mabaya na hata wengine ndo wanauza madawa ya kulevya na hakuna reaction yoyote kutoka kwenu Instead of follow wema sababu ya kumtukana mtu plssssss...STUPID POLISI..Acheni ubinafsi,ujangili na muwe FAIR kwa wanachi wote cause iyo ndo kazi yenu...INFACT katika watu SIWAPENDI POLISI your the FIRST ONE na VMAFISADI WENU.PUMBAVUUUUUUUUU...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na wewe Wema RESPECT YOURSELF..kuna watu wanapesa na wazuri zaidi ya wewe na awa behave like you,Who think your..For your own good just JIREKEBISHE cause hawa polisi wanakutafuta uingie kwenye kumi na nane zao na utakwenda kunyea debe kweli..BOMBOKLAT FOOLISHNES.

      Delete
  7. who the f*ck iz wema sepetu?sasa wakina oprah winfrey,beyonce,mary j blige wasemeje?

    ReplyDelete
  8. Huyo kuma wamuweke tu ndn atajirekebisha

    ReplyDelete

Top Post Ad