ATHARI ZA PICHA ZA NUSU UCHI NA TATTOO ZINAZO ZAGAA MITANDAONI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwezi wa kujistiri kwa wale wenzangu na mie ndiyo huo umeondoka, hapana shaka kuna wengine wanasoma hapa, huku wakiwa ndani ya yale mambo yetu. Siyo ishu, kila mtu ana uhuru wa kufanya kile akipendacho. Nchi yetu inaruhusu kuvaa chochote, ilimradi tu usiende utupu.

Nakumbuka miaka kama mitatu nyuma iliwahi kutokea hoja kuhusu mavazi, wengi walisema Serikali ilikuwa na mpango wa kupiga marufuku vimini na nguo za kubana.

Basi bwana siye tunaopenda mambo hayo roho zilikuwa juu, huku wengine tukitishia hata kuhama nchi ikiwa tutafikia huko kwa kukatazana mavazi.

Lakini kwa bahati nzuri rais wetu, Jakaya Kikwete alilitolea tamko suala hilo  na kusema kuwa kila mtu ana uhuru wa kuvaa kile anachojisikia, ili mradi tu asiende utupu. Hapo alimaliza kila kitu.

Tuachane na mambo ya mavazi, suala la msingi leo ni ‘mapicha’ na tattoo tunazochora mwilini na kuzitupia mtandaoni kila kukicha. Turudi kulekule kwenye uhuru wa kufanya kile unachojisikia, lakini usiku ukienda kulala jiulize mwisho wake nini?

Mimi na wewe hatujui kesho tutakuwa kina nani katika dunia hii, labda uniambie wewe huna ndoto za kufanya jambo litakalokufanya ukumbukwe, hata ukitoweka kwenye uso wa dunia.

Kila mtu, hasa wasichana waona fahari kuweka picha za nusu uchi  katika mitandao ya facebook, twitter na sasa instagram . Ujana, maji ya moto, kwa sasa hizo ‘likes’ na ‘comment’ unazopata zinakuvimbisha kichwa, lakini naamini baadhi yetu, miaka kumi ijayo tutatamani kurudi nyuma ili tuondoe historia mbaya tulioiweka mtandaoni.

Picha hizi zitatumika kukugandamiza kwa chochote unachokusudia kukufanya wakati huo. Ni nani atamchagua kiongozi mwenye picha kama zako unazotupia sasa.Kampuni gani yenye heshima itakayomwajiri mtu mwenye sifa mbaya kwa jamii.

Watu wengi wana uwezo kuona kinachoendelea kwenye mtandao, kumbuka miaka sita au saba kutoka leo siyo mbali, watu watakumbuka, wengine watakuwa na picha zako. Wasiokupenda watazitumia kama silaha ya kukuangamiza.

Kitu kingine ambacho unaweza kuja kukijutia ni hizo tattoo unazochora hivi sasa. Wapo watu hivi sasa wanalazimika kuvaa mashati yenye mikono mirefu, suruali au nguo zenye kuficha maeneo fulani ili waifiche michoro hiyo.

Itafika wakati unashindwa hata namna ya kuwaeleza watoto wako kwa kuwa wengi wanachora kwa kufuata mkumbo au kwa kuona Rihanna, Chris Brown kachora.  
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ana body nzuri kupiga picha hizo haki yake.

    ReplyDelete
  2. Mfano upo muheshimiwa temba wa tmk alifukuzwa jeshi na kukosa ajira kwasababu ana tatoo ,wizara za serikalini hupat kaz kama una tatoo,,pia ukienda wizara yoyote ukiwa umevaa kihuni hawakupokei tena unatimuliwa,,,,ni ulimbukeni ,vipo vya kuiga sio hivyo vya tatoo

    ReplyDelete
  3. Hizi pics ni nzuri tunazipenda sana waendelee kuzipiga

    ReplyDelete
  4. Yap ni kweli kabisa unapotaka kufanya jambo unatakiwa ufilirie na baadae kwa kuwa matendo mengine huleta majuto ya maisha.
    kukaa uchi sio sifa bali ni kujishushia heshima ya milele.

    ReplyDelete

Top Post Ad