CESC FABREGAS APEWA RUKSA KWENDA TEAM YOYOTE...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kocha mpya wa klabu ya Barcelona Gerardo Tata Martino ametoa tamko juu ya mustakabali wa kiungo wa klabu hiyo Cesc Fabregas kwa kusema kwamba uamuzi wa kubaki ama kuihama klabu ya Barcelona upo mikononi mwa mchezaji mwenyewe na hawezi kumuingilia katika uamuzi wowote. Anakwambia anaamini kuwa Cesc anaipenda Barca na hataondoka kwenye klabu hiyo baada ya kuwepo kwa ofa za kumsajili toka klabu ya Manchester United.
Cesc alikuwa uwanjani jana wakati Barca ilipocheza na Santos katika mchezo wa kirafiki ambapo mabingwa hao wa zamani wa ulaya walishinda kwa nane bila huku Cesc akifunga mawili. Manchester United walipeleka ofa mbili kwa ajili ya kiungo huyu ambapo ya kwanza ilikuwa paundi milioni 26 kabla ya kuja na ya pili ambayo iliongezeka na kufikia paundi milioni 31. United huenda wakarudi na ofa ya tatu ambayo itakuwa ya mwisho ambayo inaaminika kuwa itafikia paundi milioni 41.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad