DEREVA DALADALA AFUMANIWA NA BINTI YAKE

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Issa Mnally na Richard Bukos

AMA kweli za mwizi arobaini! Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Temba, mkazi wa Kimara-Rombo, Dar ambaye ni dereva wa daladala amefumaniwa laivu na mkewe akiwa gesti na binti yao wanayemlea.

NI MTEGO
Tukio hilo la aina yake lilijiri wiki iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo maeneo hayohayo ya Kimara-Rombo, majira ya saa 10:00 jioni ambapo Temba ambaye ni dereva wa daladala inayofanya safari kati ya Kimara na Kariakoo alinaswa kiulaini baada ya kuwekewa mtego.

OFM YATAARIFIWA
Baada ya mke wa Temba kuweka mambo vizuri aliitaarifu Oparesheni Fichua Maovu ya Global Publishers ambapo alihojiwa maswali muhimu kisha kutakiwa kuwajulisha polisi ili kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.

MWANZO WA YOTE HADI FUMANIZI
Kwa mujibu wa mke wa Temba, siku kadhaa nyuma aligundua kuwepo kwa mawasiliano ya kimapenzi kati ya mumewe na binti yao hivyo akalazimika kufanya uchunguzi wa kina.

CHANZO SMS 
Mama Temba alisema kuwa katika harakati zake, siku ya tukio alifuma ujumbe wa simu ‘SMS’ kwenye simu ya binti huyo, aliposoma alishtuka kuona ujumbe wa kimapenzi kutoka kwa mumewe.
Kwa kuwa hakuamini alichokisoma, mama Temba ilibidi amwite binti yake ili amweleze vizuri juu ya ujumbe huo.
Alisema kuwa binti huyo (jina linahifadhiwa) mwenye umri chini ya miaka 18, hakuwa na hiyana alimweleza ukweli juu ya tabia ya baba yake huyo kumtaka kimapenzi.
Aliendelea kusema kuwa alipombana kujua kama ‘walishaduu’, binti huyo alidai kuwa amekuwa akimtolea nje.

KAZI YA KUMNASA
Mama huyo alisema kuwa hakuwa na papara mara baada ya kuambiwa taarifa hizo, alichokifanya alimtaka binti yake huyo amkubalie na  amwambie baba yake huyo wapange wakutane wapi.
Mama huyo alijifanya binti yake na kuanza kuchati na mumewe masuala ya mapenzi bila kufahamu kuwa anachati na mkewe.
Katika kuchati, Temba alituma SMS: “Tulia natafuta mtu wa kumwachia gari (daladala) halafu nitakutumia SMS kukuambia tukutane wapi, leo nataka nifungue ukurasa wa mapenzi na wewe, mwanangu nakuhakikishia utakuwa na maisha mazuri sana.”
Baada ya kukubaliana kukutana gesti hiyo, mama huyo alikwenda kutoa taarifa katika kituo kidogo cha polisi kilichopo maeneo hayo ya Kimara-Rombo na kupanga jinsi ya kumnasa.

FUMANIZ KABAAANG!
Majira ya saa 10: 00 jioni, Temba alipata mtu wa kumwachia daladala na kutinga katika gesti hiyo kisha kumtumia SMS binti huyo akimtaarifu ameshafika.
Tofauti na alivyotarajia, ujumbe huo ulitua kwa mkewe ambaye alimwambia binti huyo amfuate mara moja lakini ahakikishe ‘tunda’ halitafunwi.
Ilidaiwa kuwa binti alipofika chumbani alimkuta mtu mzima akiwa amevaa taulo tayari kwa kuvunja amri ya sita na binti yake huyo bila kujua kuwa nje ya nyumba hiyo ya wageni kulikuwa na mkewe na polisi.
Ilisemekana waliachiwa kama dakika kumi na tano ndipo timu nzima ya polisi wakiongozwa na mkewe wakaingia ndani kwani hawakufunga mlango na ‘shughuli’ ilikuwa bado haijaanza.
Habari zilisema kuwa mwanaume alipomuona mkewe anaingia chumbani akiwa ameongozana na polisi nusura apasuke kwa mshtuko kwani alishindwa kuyaamini macho yake.
Ilielezwa kuwa mume alijaribu kutumia kila aina ya lugha kumuomba msamaha mkewe lakini mke aliamuru askari kumtaiti kwa kumpiga pingu na safari ya kwenda kituoni ikaanza.

ATEMBEZWA NA TAULO MTAANI
Kabla ya kupelekwa kituoni jamaa huyo aliibua timbwili zito na kusababisha watu kukusanyika na kuongoza msafara kuelekea polisi huku akitembezwa na taulo mtaani huku mkewe akimbebea nguo nyingine ikiwemo ‘boksa’.
“Yaani hata siamini, mume wangu nilimuamini sana kumbe ananizunguka,” alisema mke wa Temba kwa huzuni.
Alipofika kituoni, Temba aliandikisha maelezo ambapo hadi mashushushu wetu wanaondoka eneo hilo, kulikuwa na watu kibao waliokuwa wakipiga kelele ‘weweee...’.

Source:GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mi sielewi baada ya kumfanyia hivyo mumeo wa ndoa napengine mmeshazaa mnaachana au... sawa kakosa but kuna namna takumaliza kec zakifamilia like that unaweza fikiria umemdhalilisha at da same time umejidhalilisha?! Thanx God hawajado... Ita watu mkae chini km vp nenda polis lakini sio kumjazia watu?!! Aibu ya mumeo ni yako?!! Ss hao ulowaita wamekusaidia nn!? Km si kuwafaidisha kwa habari? Wenzio wamepata story umebajki na aibu yako.....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani mdau kama ulikuwa akilini mwangu ! shule muhimu haki ya nani, sasa wanahari wanakulipa ukisha jidhalilisha au? Ivi watu tunaakili gani jamani! Badala ya kuwaita wazazi kimya kumya washuhudie uchafu wa mumeo then kama ni uwamuzi wachukuliwe,wewe unawaita waandishi wahabari! Ili iweje? Kwanza wanaume hawana haya..apo umejidhalilisha wewe mwanamke na huyo binti yako..huyo binti atakuwa hana raha mitaani na hata shulekwa aibu ulio mpa mwanao! Embu badilikeni basi khaa


      Hala huyo mumeo anamatatizo kichwani,kweli umtake mwanao kimapenzi ? So nasty! Jela nimuhimu kwa huyo mumeo hafai kuwa mitaani.

      Delete
    2. Ni kweli Anonyz hapo juu AKILI NI MALI wanawake tubadilike,hahahaaaa sipati picha ww mwanamke mumeo unamtembeza na taulo la guest!! Ww umembebea nguo??? Umumjazia watu??? Unajiona Jasiriiiii!!!!! SHAME ON U!!! Hujafundwa namna yakutatua kesi zafamilia?? BUUUUUU.... mwanamke huna haya?? Kwa akili yako yeye na ww nani kaaibika?

      Delete
  2. Hope anonymous mliocoment hapo juu ni wanawake,sorry mmeolewa? Mnabusara ktk maamuzi yenu.kama bado plz naomba mawasiliano i nee a wife like nyie plz plz plz!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante mdau. sijuwi wenzangu ila mimi nimeolewa tayari:) sijuwi wenzangu.. good luck

      Delete
  3. Ngoja niulize... hivi angekuwa mwanamke kafumamiwa si angepigwa talaka. Safi sana mwanamke wanaume wanaonea sana, kupenda ngono tu. Tena ungemtembeza na boksa..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hayo ni maoni yako mwanaume ni mwanaume tu,jilinganishe nae afu uone. Akienda gest naww nenda akimtongoza mwanao naww mtongoze rafiki yake mwisho wa cku utajua km mnalingana.

      Delete
  4. Aibu kubwa sana kwa baba mzazi hata aibu haoni wanawake tele wamejazana unachukua bintiyako heeee....nampa hongera sana hiyo mke wa temba na bintiye aliye mwaminifu kwa mamake.

    ReplyDelete
  5. Ww mama huoni kama na ww umejidhalilisha?ucngefanya hvyo hyo mumeo aibu yake ndio yako mngeyamaliza chumbani kama angerudia mngeshirikisha wazazi jamani wanaume wenzangu tukitaka kuoa tutafute wanawake wenye busara pia shule pke yake haitoshi utakuta huyu mwanamke ni msomi lakini busara hana!

    ReplyDelete
  6. kwa wajihi wa huyo ndugu, hawezi kuwa na mtoto aliyepevuka..ndo maana habari sio kamilifu (mtoto wanayemlea)!! hapo hamna kesi coz tendo halikufanyika!! huyo mwanamke atakuwa sio mtanzania, watanzania tuna utu na kuthamini heshima zetu....

    ReplyDelete
  7. Busara ilitakiwa kama alifanikisha kumtega wangeenda yamaliza hukohuko gest kumjazia watu na kumtembeza na taulo barabarani wakati hata haja mdi binti ni udhalilishaji, hajafundishwa huyo mama, inawezekana mhusika alijiokotea mtaani akaweka ndani hayo ndio matakeo take.

    ReplyDelete

Top Post Ad