DR.SLAA AMKOSOA RAIS KIKWETE KUHUSU RWANDA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo kwa vile wanatambulika kama wauaji.

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza Watutsi.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, amempandisha cheo,” alisema.

Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi.

Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


CHANZO: NIPASHE
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. We slaa una wazimu ni sawa maji kuita water

    ReplyDelete
  2. HUO NDIO UKWELI RAYISI KAGAME ANAHAKI KUPINGA USHAURI HUO,HAO MNAWO SEMA KWAMBA KAGAME AFANYE NAO MAZUNGUMZO,NIWALE MWAKA 1994 WALI CHINJA WANYARWANDA LAKIMOJA ELFU,IWE JE LEO KIKWETE ASEME KAGAME AFANYE NAO MAZUNGUMZO. DR SLAA ANALIJUWA HILO NDIO MAANA KASEMA HIVYO MIMI NAMUUNGA MKONO KWAKWELI. WATU WENGI HAWAJUWI FDLR NIWATU GANI?SIO KAMA WAASI WAYU GANDA AWO WAASI TUNAWO WAZOWEA LAHASHA, HAO NI NTERAHAMWE WALIOCHINJA WATOTO WAMAMA NA WAZEE.KAGAME YEYE ANASEMA ATAKAE JISALIMISHA ATAPUNGUZIWA ADHABU.

    ReplyDelete
  3. WALA MSIMLAUMU DR. SLAA KWA KUMKOSOA KIKWETE; KAMA MNAJUA WAZI MAMBO MANGAPI YANATOKEA TANZANIA NA HAKUNA AMBAYE ANAONGEA CHOCHOTE? KIKWETE AANZE KUTATUA MATATIZO YA NCHI YALE KWANZA NDIO AINGILIE MAMBO YA NCHI ZA NJE. BY THE WAY KIKWETE NI NANI HASA MPAKA AMWAMBIE KAGAME USHAURI WAKE? MTU YOYOTE AMBAYE ANAMPINGA DR. SLAA HAELEWI UKWELI WA MAMBO. JE MMEONA NCHI YEYOTE AU RAISI WA NCHI NYINGINE YEYOTE KUMSHAURI KAGAME? AU KIKWETE KUTAKA KUJIONYESHA TU KUWA ANAFANYA KITU CHA MAANA KWA WATANZANIA. KIKWETE AANZE KUONYESHA UTAWALA WAKE KWA WATANZANIA KWANZA; MAISHA NI MAGUMU MNO ATATUE MATATIZO YA NCHI YAKE NDO AANZE KUONGEA EXTERNAL AFFAIRS. NYIE MNAOTUKANA NA KUKEKELI DR. SLAA HAMUELEWEI NA NI BVEBDERA FATA UPEPO.

    ReplyDelete
  4. kweli rais kikwete amesema vizuri?ukijuwa wa nyarwanda wa tutsi,niwabaya sana wanajifanya wana kuja na ngombe zao kila inchi kuomba na fasi ya kulisha majani,ukiwapa nahapo njo wataishi pia wa tajifunza rugha yako kesho wana kunyanganya inchi yako.wana mpango wakamate inchi kama izi hapa,Rwanda,burundi,uganda,congo DRC,Tanzania,congo brazza ville,kenya,centre africa.wana taka wafanye umoja wa wa tutsi,na mwenye anatia izo juudhi ni kagame,na yoweri museven.

    ReplyDelete

Top Post Ad