HIVI UMALAYA NI TABIA AMA KUTORIDHIKA NA MPENZI MMOJA?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Habari wana jamvi, ni matumaini yangu hatujambo sote. Jamani me nina tatizo moja naomba mchango wenu. Niliolewa na mume wangu halali kabisa wa ndoa. Mwanzoni tulipendana sana, lakn gafla mwenzangu akachange akawa mkali kwangu bila sababu, anachelewa kurudi cku nyngne harud kabisa. Sikuwah kumfokea wala kumuulza ulikuwa wapi, nilimpokea tena kwa mahaba yote niliyofundshwa na bibi yangu, nampa chakula anakataa, nampeleka bafuni namuogesha na ninagundua kabisa mume wangu ametoka kwa mwanamke mwingne, lakin nampa haki zake zote za msing.
Ilifkia kpnd natukanwa na wanawake zake kny cm, lakn yeye haoneshi hata kushtuka. Cjawah kumshatki hata kwa mshenga, nilikuwa namvumilia najua ndo mume nimepewa na mungu. Kilichokuja kutokea ni kwamba alihama nyumbani akaniacha na wanangu wadogo ni mapacha wenye umri wa mwaka1, nimewalea mwenyewe kwa shida hvyo hvyo na vibiashara vyangu mpaka leo, ikafikia cku wakaja ndugu zake kunifukuza kwenye nyumba ile nikarud kwetu na wanangu. Huko nikaona nimfuate mshenga nimweleze, mshenga akamuita, alipomuita alikuja na ndug zake hao wenye maneno yani washari balaa, basi ktk kuongea ikanekana wanandugu walipanga tangu huko kwao kwamb waje kuivunja ndoa yangu, mume wangu bila ya huruma akanipa talaka mbele ya ndug zake na wanangu wakilia kwa uchungu kama walijua kilichokuwa kinaendelea.
Nikaanza maisha ya upweke na wanangu. Cha ajabu baba yao huwa anakuja analia eti nimsamehe tulee watoto we2. Anasema et yey hapendi kuwa malaya ila inatokea tu . Nisaidien wajameni, me cmpendi hata kidogo yan amenitoka kabisa kwa jnc alivyonitenda na hawa malaika.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Achana nae yudaa uyoo!

    ReplyDelete
  2. achana nae sio ridhiki yako hiyo.

    ReplyDelete
  3. Si vyema kurudiana na mtu wa namna hiyo ni hatari kwa maisha yanayoendelea.

    ReplyDelete
  4. msamehe mlee watoto wenu.

    ReplyDelete
  5. Kama unataka kurudiana nae bora mkapime HIV

    ReplyDelete
  6. Sex addiction ni ugonjwa

    ReplyDelete
  7. hata ukimsamehe atarudia tu kikubwa maombi MUNGU atakupa jibu hilo limekuwa tatizo kwenye ndoa nyingi sasa

    ReplyDelete
  8. huyo mpotezee kabisa mwambie akaendelee huko alikoona pamaana

    ReplyDelete
  9. Yaani usithubutu tabia haina dawa. Atakuja kukuua kwa ukimwi wanao wateseke bure. Tulia mwanamke mwenzangu Muumba atakupa mwingine mwema. Acha aende zake mpumbavu huyo. Sie wakristo twafundishwa usimtende vibaya mke wa ujana wako nae kakutenda. Usikubali hata atakuona unamuhitaji saaana ndo atakutesa zaidi. Pole mpenz

    ReplyDelete
  10. pretend kama wanavyokuambia upate ukimwi

    ReplyDelete
  11. ..........YOTE NI SAWA,WACHANGIAJI WAMEHUKUMU VZR,,LAKINI UJUE KUNA HUKUMU KUKATIWA RUFAA MAANA MAHAKAMA YA WANAJAMII WAMESIKILIZA MAELEZO UPANDE MMOJA,,,INAWEZEKANA HUYO JAMAA AKIPEWA NAFASI YA KUJIELEZA KUMBE WEWE NDO MWENYE MAKOSA SANA,,HIVYO IULIZE NAFSI YAKO KAMA KWELI ULIYOSEMA NI KWELI AMA UMEWAHI KITUONI KUSHITAKI ILI MWENZIO AKAMATWE..WEWE NDO UNAUJUA UKWELI NA MAAMUZI,,CHUKUA YA WANAJAMII CHANGANYA NA AKILI YAKO UTAPATA JIBU,,,MAANA UKWELI UNAO WEWE.

    ReplyDelete
  12. Mi ninamashaka na jambo 1,kwann hata ndugu wanakukatili??

    ReplyDelete

Top Post Ad