LIYUMBA AKWAA BALAA JIPYA,YEYE NA MKEWE HAPATOSHI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MNAMKUMBUKA aliyekuwa kigogo wa Benki Kuu ya Tanzania aliyefungwa jela miaka miwili kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na ufujaji wa mali za umma, Amatus Joackim Liyumba? Basi amekwaa balaa jipya, Uwazi linajua kila kitu
Liyumba na mwanamke aliyedai ni mke wake, Aurelia Paulo Ngowi wamefikishana Mahakama ya Kinondoni, Dar kisa kikidaiwa ni mzee huyo kumtaka mwanamke huyo kuondoka haraka kwenye nyumba anayoishi na watoto wao wawili.
Nyumba hiyo ipo Mbezi ya Afrikana, jijini Dar. Mbali na kuwa makazi, lakini sehemu ya mbele ya nyumba hiyo ni Hoteli Amjen yenye kupata wateja kila siku.
Jina la Amjen linadaiwa ni muuganiko wa majina ya Amatus na Jennifer ambaye ni mtoto mmoja kati ya hao wawili wa mzee huyo. 
Aurelia ndiye aliyekimbilia mahakamani kuomba msaada ambapo shauri lake lilifunguliwa kwa namba 59, 2013 mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Rugemalira.
Baada ya ombi hilo, mahakama ilimwamuru Liyumba kumwacha mkewe na watoto hao waendelee kuishi kwenye nyumba hiyo mpaka shauri hilo litakapotatuliwa kisheria.
Haikujulikana mara moja kama Liyumba anataka mkewe na watoto waondoke kwenye nyumba hiyo na yeye kwa sasa anaishi wapi. 
Jitihada za kumtafuta zilifanyika, simu yake ya mkononi haikuwa hewani huku ikidaiwa kwamba namba husika haitumii tena.
Baadhi ya watu wake wa karibu waliliambia Uwazi kwamba, kwa sasa Liyumba anaishi Kinondoni, Dar es Salaam lakini kupatikana kwenye simu ni ishu nyingine.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mke wa liumba alikufa miaka mingi iliyopita alikuwa chotara wa kiarabu huyo atakuwa hawara tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwa kweli mdau! mi mwenyewe ndo naijua hiyo familia miaka mingi! huyo mama alizaaga nae tu! mchaga hana aibu looh! eti mke wake! wakati liyumba mke wake ameshatangulia mbele za haki na alikuwa mix ya kijelumani huyo mama.

      Delete
  2. Amatus,jina linamfaa baba Ana matusi balaa

    ReplyDelete
  3. janani watu wamezidi kumsinguZia huyu mzee wa watu! huyo mama alizaa nae miaka 30 iliyopita. na huyu baba alizaa na wanawake kama watano tifauti lakini hakuwahi kumuoa! Liyumba alioa mwanamke mmoja tu ambaye ni chotara wa kijerumani na ameshafariki!

    ReplyDelete
  4. Huyo binti ni muongo alikua akiishi pale na bwana wake kwenye chumba cha hio hoteli hamna cha familia wala nini katimuliwa na bwanake watoke ndio anatapatapa kutaka kumkomoa na kumdhalilisha baba wa watu.... Mitoto mingine bwana hovyoooo.....

    ReplyDelete

Top Post Ad