MSHINDI WA NYUMBA KUTOKA SHINDANO LA AIRTEL YATOSHA HUYU HAPA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam, Tanzania. Airtel Tanzania leo imetangaza mshindi wa kwanza wa nyumba kupitia promosheni ya Airtel yatosha Shinda nyumba inayoendelea na kuwazawadia wateja wake kila siku.

Bwana Silvanus Juma mkazi wa Iringa mwenye umri wa miaka 33 ambaye ni mhasibu katika shirila la Tanzania Rural women and children development foundation - TARWOC ameibuka mshindi na kuzawadiwa nyumba kisasa iliyojengwa na shirika na nyumba la taifa NHC iliyopo kigamboni jijini Dar es saalam. 


Akiongea wakati wa kuchezesha droo hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel bwana Jackson Mmbando alisema” kama tulivyowangazia awali leo ndio ile siku muhimu na maalumu ya kumpata mshindi wetu wa kwanza wa nyumba na tumeshuhudia bwana Silvanus Juma akiibuka mshindi kupitia droo ya kwanza tuliyoichezesha hapa.

Sambaba na hilo leo tunao washindi 7 wa wiki kutoka katika mikoa mbalimbali ambao hawa wataondoka na pesa taslimu shilingi milioni moja kila moja, washindi hawa ni pamoja na Peter Ignasho kutoka Muheza Tanga, Edita Rweyabura kutoka Bukoba, Steven Maguro , Rakesh Ali Mauji, Mwajuma Hassani kutoka Dar es Saalam, Siasa Yahaya Songo kutoka Manyoni Singida and Vero Mispela Kiwango kutoka Bihalamulo.

Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kuendelea kutumia huduma ya Airtel yatosha na kujiunga na vifurushi mbalimbali na kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali , kujiunga nirahisi piga *149*99# kisha nunua kifurushi chacko cha siku, wiki au mwezi na kisha kuingizwa moja kwamoja kweny droo ya kuweza kushinda milioni moja kila siku au zawadi kubwa ya Nyumba. 

Akiongea mara baada ya kutangazwa mshindi Bwan Silvanus Juma alisema”Ninayofuraha sana kupata zawadi hii kubwa kutoka Airtel napenda kutoa wito kwa watanzania na wateja wa Airtel waendelee kutumia huduma ya Airtel yatosha na waamini kuwa hakuna upendeleo. Binafsi sijawahi kushinda Bahati nasibu yoyote na nilikuwa siamini kama hakuna ubaguzi kwenye kushinda, lakini leo nashuhudia kwamba ushindi ni wa uhakika usio na upendeleo wala ubaguzi hivyo wajaribu nao wanaweza kuwa washindi.

Kwa upande wake moja ya wafanyakazi wenzake Bwana Beatus Magoti ambaye ni Mshauri wa fedha na utawala TARWOC alisema” tumefurahi sana kuona kijana mgodo mwenzetu ambaye ni mchapa kazi ameweza kushinda nyumba kupitia promosheni ya Airtel yatosha. Hii imetupa hamasa na sisi kushiriki na kueneza habari kwa wengine kushiriki na kushinda kama laivyoshinda Silvano.

Airtel inaendelea na promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba tatu ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake na kutoa huduma bora zenye gharama nafuu kupitia huduma ya Airtel yatosha. Sambamba na hilo Airtel pia imewawezesha wateja wake nchi nzima kutuma na kutoa pesa bure bila makato yoyote.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad