MUME WA PILI WA WASTARA AIBUKA ADAI WASTARA NI MKE WAKE

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Na Issa Mnally
MIEZI nane baada ya kufariki dunia mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’, hatimaye mume wa pili wa staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Ahmed Kushi ameibuka na kudai kwamba anatambua kwamba staa huyo bado ni mkewe na anataka ampatie mwanaye aliyezaa naye.
Kwa muda mrefu kulikuwa na taarifa kuwa Wastara aliachana na mwanaume huyo kwa talaka kabla ya kuolewa na Sajuki lakini kuibuka kwake na madai kuwa bado mwanadada huyo ni mkewe kumezua mshangao mkubwa.



MADAI YA KUSHI
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Kushi alifunguka kwa mara ya kwanza kuwa yeye na Wastara walifunga ndoa ya Kiislamu mwaka 2000 na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Fares.
Alisema: “Kisheria bado ni mke wangu kwa kuwa nilikuwa nimempa talaka moja tu wala hazikufika tatu,” alisema Kushi na kudai kwamba ndoa yake na staa huyo ilidumu kwa mwaka mmoja na nusu na kuvunjika kutokana na kutawaliwa na migororo.
Jamaa huyo alidai kuwa zaidi ya mara tatu amekuwa akimtaka Wastara ampatie mwanaye huyo ambaye kwa sasa ametimiza miaka minane bila ya mafanikio.

KWA NINI WAKATI HUU?
Gazeti hili liliamua kumbana kwa kumuuliza kwa nini ameibuka wakati huu baada ya Sajuki kufa na mbona hakujitokeza kwa zaidi ya kipindi cha miaka kumi iliyopita? Pia akaulizwa kwa nini ameamua kutafuta umaarufu kwa kumdhalilisha? Akaishia kukaa kimya.

WASTARA AFUNGUKA
Baada ya Kushi kuibuka na ishu hiyo yenye utata, gazeti hili lilizungumza na Wastara ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kuhusu mtoto, kama kweli alikuwa na lengo la kumchukua mwanaye na ananijua, basi atakuwa anawajua wazazi wangu hivyo angefuata utaratibu.
“Hakuna utaratibu kama huo kama kweli anamhitaji mwanaye angeenda kwa wazazi wangu, huko ni kunidhalilisha kwa kuwa ananiona mnyonge baada ya kufiwa na mume wangu Sajuki.
“Kama siyo kunidhalilisha ni nini? Naomba asitumie jina langu kutafuta umaarufu kwa kunichafua. Naomba aache kwa sababu ananiongezea maumivu juu ya maumivu.”
Kuhusu madai kwamba bado ni mkewe, Wastara alilia: “Hivi huyo mtu alikuwa wapi muda wote nikiwa na Sajuki? Mbona hakuibuka wakati mume wangu akiwa hai? Najua anatumia kigezo cha kuondoka Sajuki kunionea lakini Mungu anajua.”

NI KWELI ALIFUNGA  NDOA NA KUSHI?
Pamoja na kumbembeleza aeleze kama kweli aliwahi kufunga ndoa na Kushi, Wastara alisema: “Sitaki kumzungumzia mtu, naomba watu wawe na huruma kwangu, wasitumie kigezo cha kumpoteza Sajuki kunidhalilisha.”

SHEHE AMPINGA KUSHI
Gazeti hili halikuishia hapo, lilimtafuta shehe wa Msikiti wa Nuur wa Magomeni-Mapipa jijini Dar, Juma  Simba ili kupata ufafanuzi juu ya talaka moja ambapo alimpinga Kushi kwa kusema kuwa kisheria Wastara si mkewe tena.
“Kumpa talaka moja si sababu ya kuendelea kuwa mke wake mpaka leo hii, sheria inasema kuwa Kushi alitakiwa kumrejea Wastara kabla ya miezi mitatu kupita tangu alipompa talaka moja,” alisema na kusisitiza kuwa ndoa hiyo ilishakufa.

YATOKANAYO
Awali ilidaiwa kuwa Wastara aliwahi kuolewa mara mbili kabla ya kufunga ndoa na staa mwenzake wa filamu, Sajuki.
Ndoa ya kwanza ya Wastara aliifunga mwaka 1998 na Juma Mpemba ambaye alibahatika kupata naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Samir.
Sajuki alikuwa mume wa tatu kwa Wastara ambaye naye alibahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Farheen.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kumbe kuna talaka 3 waislam bwanaa

    ReplyDelete
  2. Tafadhali mcangiaji usilete udini tafadhali sana ysuingilie dini ya mwenzio na kuikashif

    ReplyDelete
  3. kumbe hakuna kuachana kwa wakiristo bwanaaaaaaaaaa hata ukimkuta jamaa anakula uroda kwa mkeo husamehewa dhambi tu ni raha eeeeeeeeeh

    ReplyDelete
  4. Unajua watu wengine ovyo sana mbna munata kuleta commet za kdn zisizo faida yyte bali ni kuwekea chuki sio waislamu tu wanaoachana mm nimeoa mwanamke mkristo aliyeachwa na mumewe nimemsilimisha mpaka ss tunamtt 1 mwaka 4.

    ReplyDelete
  5. Mdau co poa kukashif dni ya mwenzio n if u hv nting 2 share bac pga kmya...!!

    ReplyDelete
  6. Wastara anamatatizizo kwanini aachike kwa wanaume wote hao?

    ReplyDelete
  7. WE INNO MAWAZO YAKO MGANDO!!! ETI WASTARA ANA MATATIZO KWANN AACHIKE MARA TATU???!!! MAYO ZAKOOO

    ReplyDelete

Top Post Ad