MWENGE UNAENEZA UKIMWI NA UFISADI HATUUTAKI TENA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BAADHI ya wabunge wamekosoa mbio za Mwenge wa Uhuru, huku wengine wakitaka ufutwe kwa maelezo kuwa hauna tija kwa sasa. Wabunge hao wakiwamo wa upinzani na CCM, walisema Mwenge umekuwa kero na kwamba wakati mwingine ofisi za umma hufungwa kutokana na mbio zake na hivyo kusababisha wananchi kukosa huduma.

Sakata hilo lilitokea jana Bungeni mjini Dodoma, baada ya Mbunge wa Musoma Mjini Vicent Nyerere (CHADEMA) kutaka kujua faida na hasara zilizopatikana tangu Mwenge wa Uhuru ulipoanza kukimbizwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Nyerere alisema wakati fulani viongozi wa Serikali walimtisha Naibu Meya wa Manispaa ya Musoma, Nyamero Bwire, kutokana na hatua yake ya kuzuia gari la wagonjwa la hospitali ya wilaya kutumika katika mbio hizo.

Katika swali lake la msingi, mbunge huyo aliuliza kwamba “kwa kuwa tangu mwenge ulipohamishiwa katika mfumo wa Serikali, wananchi wamekuwa wakilazimishwa kuchangia fedha kwa nguvu pamoja na matumizi yasiyokuwa sahihi ya magari ya Serikali. Je, Serikali haioni kwamba kuanzia sasa ianze kukimbiza mwenge katika maeneo yale tu ambayo wananchi wake wapo tayari kuchangia michango ya mwenge?” 

Aidha, Mbunge huyo pia alitaka kujua kiasi cha bajeti ya mbio za mwenge kwa mwaka na iwapo matumizi ya fedha hizo hufanyiwa ukaguzi.

Kwa upande wake Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kesy (CCM), alisema mbio za mwenge hazina faida kwa Watanzania walio wengi kwani shughuli za kiuchumi zimekuwa zikiathiriwa.

“Binafsi hiki kitu kinachoitwa mwenge sikitaki kabisa, kwani ni wazi tangu maandalizi yake hadi kufika kwake kumekuwa na mateso, kwani viongozi wanatakiwa kutoa huduma lakini wote huondoka ofisini.

“Wanatumia siku tatu kwa ajili ya kukagua miradi inayoitwa ya mwenge, huku wananchi wakisota kuwasubiri na hata baada ya kufika na kukesha katika eneo husika.

“Wakati mwingine hutumia siku mbili kupumzika badala ya kuwahudumia wananchi kwa kisingizio cha mwenge. Sasa tulipofika inatosha, ni vema mwenge usikimbizwe kwani umekuwa na matumizi mabaya,” alisema Kesy.

Baada ya maswali hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utawala Bora, George Mkuchika, alisimimama kujibu kwa kwa kusema “Wale wanaodai kwamba mbio za mwenge hazina umuhimu si kweli. Malengo yake yalikuwa ni kukimbizwa Tanganyika na umekuwa ukitoa elimu kama vile elimu kuhusu dawa za kulevya, rushwa na kuzindua miradi ya maendeleo.” 

Hata hivyo majibu hayo yalimfanya akumbane na zomea zomea kutoka kwa wabunge wa kambi ya upinzani, huku zikisikika sauti za wabunge wakisema; “Mwenge unaeneza Ukimwi”, “unaeneza ufisadi na hatuutaki tena”.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli tu mi naona hauna maana yeyote

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa mwenge ni upuuzi tu nchi yenyewe masikini

    ReplyDelete
  3. Huyo mkuchika point yake haina maana hata kwani kufungua shughuli za maendelea mwenge ndo unafunguo?kutoa elimu ya dawa za kulevya toeni mashuleni hizo pesa walpeni walimu vizuri pumbavuuuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad