NIMEGUNDUA MCHUMBA WANGU KATOA PENZI KWA MTU MWINGINE-NIFANYAJE

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wana jamii naombeni ushauri wenu kijana mwezenu yamenikuta, mimi nina girlfriend tangu mwaka jana, nimekuwa nikimpa support ya shule kama ada na mahitaji mengine kadri ninavyoweza. Mwaka jana aliombwa na dada yake akampe campani huko mbagara kwaani alikuwa amepata motto mchanga. Tangu aende kuishi kwa dada yake alianza kubadirika katika mawasiliano, aliniambia kuwa hakuwa free kama alipokuwa kwa wazazi wake temeke. Kwaani kila nikimhitaji ilkuwa ni ngumu au kwa nadra sana mfano tuliweza kuonana mara moja kila baada ya miezi 1-2. Mawasiliano yetu makubwa yalikuwa ya simu. Kwa sababu ya mawasilano yetu kuwa finyu tuliweza kutofautiana mara kwa mara hivyo hata ile support yangu ikawa inapungua kwa sababu ilikuwa ni lazima niende kwenye tigopesa kumuwezesha nayopia ilitegemea nimepata muda gani kulingana na mazingira ya kazi yangu.

Bahati nzuri mpenzi wangu amerudi nyumbani kwa wazazi sasa yapata mwezi mmoja na tunaweza kuonana mara kwa mara na mahusiano yetu yamestawi vizuri tena. Kwa bahati mbaya juzi siku ya Eid simu yangu nilimwazima mdogo wangu alikuwa amepoteza simu yake huku akiwa na issue ya pesa. Hivyo mpenzi wangu hakuweza kunipata alichukia sana mpaka akawa hapigi simu wala hajibu sms zangu kwa muda wa siku 3. Ijumatatu wiki hii baada ya kazi nilienda kujua kulikoni, aliponiona tu aliniambia nimefuata nini? Nilimshangaa sana, akasema kuwa najifanya sijui kwa nini sikupokea simu yake siku ya Eid. Nilimwelewesha na kumwomba msamaha. Baadae nilimuuliza kuwa nilikuwa nimeona gari pale nyumbani kwao na nikajifanya kama nimepata taarifa kuwa ni ya mtu wake, alinijibu kuwa kwa hiyo nina amuaje? Niliamua kuchukua simu yake kwa nguvu nikaondoka nayo. Usiku iliingia sms iliyikuwa inamtaka wakafanye mapenzi kwaani ilikuwa yapata miezi 4 tangu wafanye mala ya mwisho. Sikuamini nilichokiona. Jana jioni nilienda kukutana nae na kumuuliza kuhusu sms hiyo alilia na kuomba nimsamehe kwani alifanya mara moja kwa kuwa hatukuwa na mawasiliano mazuri kipindi hicho akiwa Mbagara eti alihisi tulikuwa tumeachana na alikuwa na shida ya shule hivyo ilimbidi kumkubari mtu bila kupenda. Zaidi aliniambia kuwa mbona yeye alinisamehe mwaka jana alipopata uja uzito tukautoa hata bila ya wazazi au dada yake kujua? Ni kweli tulitoa mimba ya mwezi 1.5. Lakini tulishauliana kuwa asome kwanza hayo mengine ndiyo yafuate. Akakubari.

Wana jamii naombeni ushauri wenu nifanyeje kijana mwenzenu yamenikuta na binti nampenda lakini kwa sababu ya hili la kutokuwa mwaminifu nimemwambia kuwa tangu jana tumeachana, kiukweli usiku kucha sijapata usingizi hata dk 5. Hapa nilipo nawaza sana. Na yeye ananiomba msamaha hatarudia ilitokea bahati mbaya.

Source:Jamii Forums
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. dah! Msamehe2 kwani binadamu yatupasa kusameheana.

    ReplyDelete
  2. da msamehe tu hamna jinsi kwasababu mlikua mbal itakua hisia zilimzid nguv ilakama ameomba msamaha msamehe ila mwambie akirudia tena mteme

    ReplyDelete
  3. Piga chini hako ni kamalaya kasiri Kaka, utakuja kulia zaidi mbeleni

    ReplyDelete
  4. Temana nae huyo ni kicheche mdogo!! Unakumbuka alikuambia kwan we unaamuaje??? Ulipomuuliza hilo gari ni la bwanaako au vp?? Huyo kicheche yupo after money, tena hizo unazompaga kwaaajiri ya xul!!! Utakuja juta akimaliza shule!!

    ReplyDelete
  5. Unatakiwa kumweleza msimamo wako ili ajue, kama atafanya kosa tena akubali matokeo. Msamaha hujenga. Maana aombaye msamaha anajutia alichokifanya.

    ReplyDelete
  6. Haha nyie ndii mnafanya wanawake wayumbe msamehe hawez rudia tena kuwa karbu nae sana kma anakupenda kweli hyo hali haiwez jirudia tena

    ReplyDelete
  7. Kama aliweza kukusaliti na kutembea na mtu mwengine just because mawasikiano yenu hayakuwa mazuri basi tarajia mda wowote itakapotokea hali ya nyinyi kukwaluzana basi atarudia kama kawaidia.
    Kama unamsamehe samehe ila elewa kuwa hakuwa muminifu kwako na mda wwt anaweza kurudia alichokifanya

    ReplyDelete
  8. Msamehe tu, ht ww yanaweza kukukuta. Aombae msamaha anajutia alofanya

    ReplyDelete
  9. mlivyo tongozana mkafanya agreements nani uliyemwomba ushauri? yaani unga umezidi leo hii unajifanya kuomba ushauri

    ReplyDelete
  10. Inategemea msimamo wako binafsi kuhusu kosa kama hilo. Kwangu ni ukiukwaji wa kiini cha mkataba - hivyo kosa mama hilo likigundulika halina mjadala.

    ReplyDelete
  11. correction: Inategemea msimamo wako binafsi kuhusu kosa kama hilo. Kwangu ni ukiukwaji wa kiini cha mkataba - hivyo kosa kama hilo likigundulika halina mjadala. Ni mwisho wa kila kitu.

    ReplyDelete
  12. USHAURI WANGU UENDE POLIS UKAFUNGULIWE MASHITAKA YA KUGONOKA NA MWANAFUNZI AMBALO NI KOSA LA UBAKAJI.HVY JISALIMISHE POLISI.

    ReplyDelete
  13. Fuata moyo wako unasema nini na si kuomba omba ushauri.

    ReplyDelete

Top Post Ad