9 Aug 2013

PICHA MBALI MBALI ZA TUKIO LA KUUWAWA MFANYABIASHARA ERASTO MSUYA HUKO ARUSHA

Mwili wa Erasto Msuya (kulia) baada ya kupigwa risasi. Kushoto ni gari alilokuwa anatumia.
Wanausalama wakiubeba mwili wa marehemu Msuya.
Mwili wa Msuya ukiwa ndani ya difenda.
Marehemu Erasto Msuya.
MFANYABIASHARA maarufu wa madini Jijini Arusha Erasto Msuya amepigwa risasi na kufa papo hapo katika eneo jirani na Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Msuya anayemiliki vitega uchumi kadhaa mkoani Arusha na Manyara amepigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakati akitokea Mererani katika migodi ya madini ya Tanzanite majira ya saa 6.30 mchana jana.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo kutoka uwanja wa ndege wa KIA ambao hawakuwa tayari kutajwa majina yao, mfanyabishara huyo baada ya kuuawa hakuna kitu kilichochukuliwa katika gari yake.
‘’Hawa jamaa walimvizia njia ya panda ya Mirerani na KIA na walifanikiwa kumsimamisha na ghafla alitokea mtu akiwa katika usafiri wa pikipiki na kummiminia risasi nyingi na inaonekana alikufa popo hapo’’alisema mtoa habari huyo.


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Total Pageviews


Popular Posts

Matangazo

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger