SERIKALI YAKANUSHA KUWA MAMA SALMA KIKWETE SI MNYARWANDA NA WALA KIKWETE SI SHEMEJI YAO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa “twitter ”  na  wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana. 

“Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,” amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.

Madai  hayo  yaliandikwa  jana  na  mitandao  ya  Rwanda  wakidai  kuwa  mama  Salma  Kikwete  ni  Mnyarwanda  na  ni  binamu  wa  aliyekuwa  rais  wa  zamani  wa  Rwanda.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa wanahitaji dawa.Wakome kabisa kumchafua Rais wetu.

    ReplyDelete

Top Post Ad