SHEIKH PONDA AFUNGULIWA MASHTAKA MPAYA MOROGORO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro imemfungulia mashitaka matatu na kisha kumnyima dhamana Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, kutokana na kukiuka agizo la mahakama.

Hatua hiyo ilikuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana kumfutia kesi ya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyofunguliwa hivi karibuni.

Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, baada ya kuwasili kwa helikopta ya Jeshi la Polisi katika uwanja wa gofu mjini Morogoro.

Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Richard Kabate, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bernard Kongola, alisema kuwa Agosti 10, mwaka huu, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Manispaa ya Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.

Alidai kuwa Sheikh Ponda aliwaagiza waumini hao kuwa endapo watu hao watajitokeza kwao na kujitabulisha kwamba ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti, wafunge milango na madirisha wawapige.

Ilielezwa kuwa kauli hiyo ni kinyume cha agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyotolewa na Hakimu V. Nongwa Mei 9, mwaka huu, ambayo ilimtaka Ponda ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani.

Katika shitaka la pili, Kongola alidai kuwa Agosti 10, mwaka huu, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu kuwa serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi ili kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi hao ni Waislamu.

Kwamba, Ponda aliwaambia wafuasi wake kuwa serikali haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo walipokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa huko ni Wakristu.

Shitaka la tatu ambalo linafafana na lile la pili, ambalo nalo linadaiwa kutendwa Agosti 10, mwaka huu, ambapo kauli ya Ponda inadaiwa kuumiza imani za watu wengine kinyume cha kifungu cha sheria namba 390 na kanuni ya adhabu namba 35 cha mwaka 2002.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo na kuyakana, mwanasheria wa serikali aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kupanga kuanza kusikilizwa Agosti 28, mwaka huu.

Mapema baada ya Sheikh Ponda kuwasili mjini hapa kwa helikopta, aliingizwa kwenye gari maalumu ambalo liliongozana na magari mengine matatu ya polisi huku ulinzi ukiwa umeimarishwa katika eneo la mahakama.

Alipofikishwa eneo la mahakama saa 5:00 asubuhi, magari yalisimama kwa takriban dakika 30, kisha akashuka akiongozana na askari kadhaa kuingizwa mahakamani.

Mawakili wake, Ignas Punge na Bartlomelo Tarimo, walisema sababu za kuomba kesi isikilizwe tarehe hiyo ni kutokana na mteja wao kuwa bado mgonjwa, anayehitaji kupatiwa matibabu.

Baada ya kesi kuahirishwa, Ponda alipandishwa tena katika helikopta mchana kurejeshwa jijini Dar es Salaam.

Mapema asubuhi jijini Dar es Salaam, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Hellen Liwa alisema kuwa Ponda alifutiwa shitaka la uchochezi baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kutokuwa na haja ya kuendelea na kesi hiyo.

Hata hivyo baada ya Hakimu Riwa kumwachilia huru, Ponda alikamatwa tena na kupakizwa kwenye magari ya wana usalama kwa ajili ya kupelekwa mkoani Morogoro kufunguliwa kesi ya jinai.

Agosti 15, mwaka huu, wana usalama walimwondoa Ponda katika wodi ya MOI na kumhamishia katika Gereza  la Segerea ili kusubiri kesi yake hiyo ambayo ilipangwa kutajwa Agosti 28, mwaka huu.

Agosti 14 mwaka huu, saa kumi jioni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilihamia katika wodi ya MOI, ambapo Ponda alisomewa shitaka moja la uchochezi, akidaiwa kuwa Juni 2 hadi Agosti 11 mwaka huu, katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitenda makosa ya jinai, ikiwamo kosa la  kutoa lugha ya kudhalilisha dhidi ya viongozi wa serikali.

Source:Tanzania Daima
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad