"SIWAJUI VIGOGO WAUZA UNGA "KAMANDA WA POLISI VIWANJA VYA NDEGE-KATTO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAKATI Rais Jakaya Kikwete akidaiwa kukalia orodha ya mtandao wa vigogo wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya, Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege nchini, Deusdedit Katto, amewataka wanaowafahamu watuhumiwa hao watoe taarifa.
Katika mazungumzo yake na kituo cha televisheni cha Channel Ten juzi, Katto alisema hawafahamu vigogo hao wanaotuhumiwa na kwamba yeyote mwenye ushahidi akatoe taarifa.

“Wakati mwingine tunasema tu, kama tuna ushahidi kuhusu hilo utolewe. Mimi nalisikia neno hilo la vigogo hata kabla sijaja hapa,” alisema Katto alipotakiwa kufafanua kuhusu uuzaji wa dawa hizo kuhusisha mtandao mkubwa.

Alisema hilo ni tatizo kubwa duniani na kwamba hakuna serikali yoyote ambayo inacheza nalo.

Alisema wanapambana na suala hilo kwa namna mbalimbali na kudai kuwa kuna baadhi ya nchi ndogo wafanyabiashara hiyo wamekuwa wakishindana na serikali zao.

Kuhusu uteketezaji wa dawa hizo kufanyika kwa siri, Katto alisema si kweli kwani taratibu zinafuatwa kwa kuwashirikisha watu wengi.

“Kuna vyombo vinatajwa lazima viwepo wakati wa kuteketeza, mfano jaji aliyesikiliza kesi, mawakili wa serikali na wale wa utetezi, Mkemia Mkuu wa Serikali ili athibitishe kama zilizoteketezwa ni dawa za kulevya,” alisema

Source:Mtanzania Daima
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad