google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html TOFAUTI KATI YA WASICHANA WA UDSM NA WALE WA UDOM HIZI HAPA | UDAKU SPECIAL

TOFAUTI KATI YA WASICHANA WA UDSM NA WALE WA UDOM HIZI HAPA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kuna tofauti kubwa kati ya mabinti wa UDSM na wale wa UDOM. Mbali na kwamba wote ni wazuri na wamemeenda vidato lakini zipo tofauti kubwa baina yao zinazowatofautisha. Kwa ujumla tofauti zao ni hivi zifuatazo;
Muonekano (image)
Binti wa UDSM mara nyingi atapenda avae vitu mpaka aonekane kama mwanamitindo. Atajiwekea make up za kila aiana japokuwa tayari ana uzuri natural. Atataka avae fasheni mpya mpya zinazotokana kwa kuwa yuko town na mara nyingi hata kama boom haliruhusu kuna wananchi wengi wa kuwapiga mizinga.  Nguo zao wananunulia Mlimani City, Quality Center, Makumbusho, Mwenge kwa White na maeneo mengine kama hayo.  Jinsi wanavyovyaa unaweza ukawaogopa kudhani ni expensive saaaaana.
Binti wa UDOM kwa upande mwingine anavaa kawaida tu. Viatu vyake vya mchomekeo wanavinunua pale SabaSaba lakini waulize wavulana UDOM sasa, watakwambia binti katoka bomba yule si mchezo. Viatu vyao ni bei za kawaida na huvumilia hali zote za hewa. Huwa shopping zao wanafanya Saba Saba.

Sehemu ya kuangalia movie (cinema)
UDSM huwezi kumpeleka binti kucheka movie room kwako! Sijui eti Hall 3 au ghetto Survey! Utampeleka Suncrest Quality Center au Mlimani City na hapo uweke bajeti ya PopCon na mazagazaga kibao ya kucheki cinema.
Binti wa UDOM wewe tu na laptop yako unamkaribisha chumbani Block 9, 10, etc maeneo ya Haiti mnacheki movie huku mkinywa maji ya kudownload, bites za Discount shop au chai. Umemaliza.
Sehemu ya kukutania (Date location)
Kama unadhani binti wa UDSM utampeleke room yako namba 2409 kule Hall 3 sahau! Kama huna ghetto la ukweli Survey au Sinza au Ubungo Maziwa au unamiliki nyumba kabisa jua imekula kwako. Sehemu ya kukutania lazima iwe ya kueleweka na treatment isomeke vizuri kama misosi iliyosimama, Pizza, Burger, Chicken Chips, etc. Hapo lazima Bamaga upajue vizuri, Mikocheni na Sinza. Kishushio Savanna au Red Bull. Mjomba huna hivyo UDSM utawapata wa kuhesabu kukusikiliza maelezo yako ya kuunga unga.
Binti wa UDOM yeye hata hajali. Wewe tu, uwe kule porini mnapaita Ng’ox au Social Room kwako atakuja. Mtengenezee chai kwa ule mkate wako wa juzi halafu anza kumwaga point zako. Huna haja ya kupajua Area D, Area C wala Lodge za Area A ila ukikosea ukakuta mwenye kaupepo ka jiji lazima kuku wa Club Maisha na 84 ujue bei yake.
Upatikanaji wao (Availability)
Binti wa UDSM atakuona akitaka kukuona si kinyume chake. Ukimpigia simu mkutane atakupa sababu kibao utabaki kichwa kinakuuma ila yeye akikupigia simu mkutane hataki kusikia sababu yako hata moja. Anapenda yeye awe na control.
Binti wa UDOM yeye anaelewa principle ya give and take vizuri sana. Anaelewa mla lazima aliwe na anaelewa ili uhusiano uwepo lazima kila mtu aplay part yake.  Ukimpigia simu baada ya dakika au saa chache utamuona na wanapenda kutembea na wavulana wao campus. Kama unabisha angalia idadi ya mabinti wa UDSM wanaotembea na boys ndani ya campus na wale wa UDOM wanaofanya hivyo ndani ya campus.
Mtazamo wao kuhusu mapenzi (Perception of love)
Binti wa UDSM atakupenda kwa ile ulichona nacho. Kichwa class, una hela au famous. Nje ya hapo ni wa kuhesabu bro.
Binti wa UDOM atakupenda jinsi ulivyo hasa kama shule kasoma Songea huko kwao vijijini chuo katua Dodoma, ila ukikuta ana kahewa ka Dar kidogo lazima utasanda. Yale yale.
Mwandishi wa Makala hii amejitambulisha kama shabiki mkubwa wa Orijino Komedi, Mhitimu wa Digrii ya Ukandarasi na sasa ni chizi hospitali ya Lutindi Tanga.


Source:Crazytanzanian blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hiyo umecopy n paste n Y only udom n udsm kwan vyuo vingine havina mabint?

    ReplyDelete
  2. ndio maana degree za pichu zimejaa udsm

    ReplyDelete
  3. Nataka ku like coment ya JOSEPH MARCEL. Wapi nibonyeze? :-)

    ReplyDelete
  4. UDSM na UDOM kwa sababu ndo issue ya chuo kikuu na chuo kikubwaa na labda jamaa ndo ana experience navyo.kwa sisi tuliosoma sehem zote mbili kuna ukweli ndani yake japo c kila kitu...

    ReplyDelete
  5. mabinti wa udsm ni first class div one ndo zimewapeleka pale hao wengine mh sijui but udsm chuo bora cha sita africa so unataka msichana eneo lile status iwepo mawazo tu

    ReplyDelete
  6. mabinti wa udsm ni first class div one ndo zimewapeleka pale hao wengine mh sijui but udsm chuo bora cha sita africa so unataka msichana eneo lile status iwepo mawazo tu

    ReplyDelete
  7. umesahau uhaziri tbr... yaan wa udsm hawafik japo kw theruthi

    ReplyDelete
  8. Yaani hiyo analysis ndo imeandikwa na msomi wa chuo kikuu? Lol. Mnatumia boom ovyo la serikali. Hakuna haja ya kusoma hapo

    ReplyDelete
  9. Hahhahaha kweli degree zimekosa kazi inabidi zitumike kama hivyo

    ReplyDelete
  10. Do you mean when you go to udsm or udom, you should follow up on this nonsense instead of studying, bloggers, make sure you publish blogs which make sense, im in Egerton university, laikipia, kenya,ive commented this cause i love this page,so be...

    ReplyDelete
  11. jamaa anadegree huyo minazani njaa ndiyo imemfanya awe chizi kakosa kazi kitaa kugumu eenh









    ReplyDelete

Top Post Ad