WASTARA ALA IDD KABURINI KWA SAJUKI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, yeye ameamua kula Sikukuu ya Idd El Fitr kwa staili ya tofauti na watu wengine ambapo alikula kaburini kwa mumewe, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
Ishu hiyo ilijiri Ijumaa iliyopita siku ya sikukuu hiyo ambapo Wastara alitundika picha zake zikiwa zinamuonesha akiwa ameshika tama na nyingine akiwa analifanyia usafi kaburi la marehemu Sajuki lililopo katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar.
Wastara alikiri kuwa aliitendea haki Sikukuu ya Idd kwani alipata nafasi ya kuzuru kaburi la mumewe na kujisikia faraja japo kimwili hayupo naye lakini kiroho wako pamoja.
“Sikukuu yangu nimeitendea haki sana kwa kwenda kuzuru kaburi la mume wangu, alhamdullilah nimefarijika sana, kimwili siko naye ila atabaki kuwa fikrani mwangu milele,” aliandika Wastara.
Mashabiki wake na wadau mbalimbali walimpa pole huku wengine wakimpongeza kwa hatua hiyo kwani wasanii wengine waliotumia sikukuu hiyo kujiremba, kwenda klabu na kujirusha. Sajuki alifariki dunia Januari 2, mwaka huu na kuacha mtoto mmoja wa kike.

Source:Global Publisher
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. U me fanya vizuri m.mungu atakupa wepesi

    ReplyDelete
  2. Maskini Wastara, yani nashindwa kuelezea jinsi ninavyokukubali. u mrembo, una mapenzi ya kweli na mumeo, mwanamke shujaa..huwezi amini na type huku machozi yananitoka. Mungu akupe nguvu, dua pia muhimu sana mamii..wewe bado mdogo na Mungu atakufariji na kukupa kile nafsi yako inahitaji. Ila kwa kweli wewe ni mwanamke bora na mfano wa kuigwa. hakika Mungu alimpa Sajuki mwenzi hasa!

    ReplyDelete

Top Post Ad