WEMA SEPETU ADAIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Skendo ya mastaa mbalimbali Bongo kutajwa katika biashara na usafirishaji wa madawa ya kulevya ‘unga’ linazidi kuchukua sura mpya ambapo tayari majina ya wasanii wawili wakubwa, Wema Isaac Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ yametajwa huku kinachowaponza kikijulikana.

Habari zinadai kuwa mastaa hao wameanza kujutia tambo zao za kutangaza utajiri walionao hivyo kuibua maswali kuwa huenda wana uhusiano na wafanyabiashara wa dawa za kulevya ikiaminika ndiyo njia ya haraka ya utajiri.

WEMA
Inadaiwa kuwa kitendo cha Wema kutangaza kununua nyumba, magari ya kifahari na kutapanya fedha ndiko kulikomponza na sasa anatajwa na wengi vinywani mwao juu ya kuhusika katika biashara hiyo haramu.

Kuna madai kuwa bosi huyo wa Endless Fame Productions amehojiwa juu ya suala hilo lakini meneja wake, Martin Kadinda alikanusha uvumi huo.

DIAMOND
Wiki iliyopita, Diamond aligeuka gumzo baada ya kuripotiwa akihusishwa na biashara hiyo huku ikidaiwa kuwa kinachomponza ni utajiri alioupata ghafla.

Ilidaiwa kuwa kitendo cha kutangaza kununua nyumba takriban tano jijini Dar, kumiliki kiasi cha Sh. bilioni moja kwenye akaunti na kuendesha magari ya kifahari ndivyo vilivyochangia watu kugeuzia antena za runinga zao kwake kutaka kujua ni matunda ya muziki tu au kuna kingine.

Madai ya jina la Diamond kutajwa katika saga hilo yalikwenda mbele zaidi ikielezwa kuwa kitendo cha kusafiri mara nyingi nje ya nchi huku akipiga picha na watu wanaosemekana kujihusisha na biashara hiyo nacho kilimponza.

Kwa upande wake, Diamond alisema kuwa hakuna mtu asiyejua namna anavyotafuta fedha kwa jasho juani hivyo watu wakimuona akila kivulini lazima wakumbuke kuwa amechumia juani na hajui chochote juu ya dawa hizo.

http://www.globalpublishers.info/
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yawezekana sababu petii man mpambe wake inasemekana ni pusha maarufu mjini

    ReplyDelete
  2. Wema amefanya kazi gani iliyomwingiza pesa kwa haraka kias hiki..

    ReplyDelete
  3. Kujiuza kwa vigogo na kuuza unga sababu hata hiyo ya vigogo still is not enough to be that rich wanaume wa bongo si wahongaji kiasi hicho hata wawe na pesa kibao they are so stingy tena wakishakupitia ndo wanakata Kamba kabisaa Kama au kupunguza kuhonga demu mwenyewe cha wote nani apoteze mamiliioni yake kwa kicheche Kama wema. Huyo ni madawa tu wachunguzwe zaidi hata huyo diamond wote show tu pekee haziwezi kumpa kipato chote hicho

    ReplyDelete
  4. Time will tell and the truth will stand still.
    Ipo siku mawe yatasema.

    ReplyDelete
  5. All hidden thinngs shall one day be made manifest!

    ReplyDelete
  6. KAFULIA HUYU HANA JIPYAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete

Top Post Ad