YANGA NOMA YAIRARUA RARUA AZAM-NGAO YA JAMII YARUDI JANGWANI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Yanga imeng’arisha nyota ya mwanzo wa msimu wa baada ya kuifunga Azam FC bao 1-0 katika mechi ya kibabe kuwania Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa jana, Dar es Salaam.

Shujaa mechi hiyo kwa upande wa Yanga alikuwa Salum Telela aliyefunga bao pekee mwanzoni mwa mchezo na kupeleka hoihoi nzito Mtaa wa Jangwani

Ushindi huo unaifanya Yanga kuweka rekodi ya kutwaa mara tatu taji hilo.

Ilianza kulitwaa mwaka 2001 walipoifunga Simba 2-1, mwaka 2010 wakiifunga tena Simba kwa penalti 3-1 kufuatia sare ya 0-0.

Azam ndiyo timu pekee haijawahi kutwaa taji kati ya zilizowahi kucheza mechi ya Ngao ya Jamii. Mwaka jana walifungwa mabao 2-1 na Simba, Mtibwa walikuwa washindi wa mwaka 2009 walipoifunga Yanga 2-1.

Kocha wa Azam, Stewart Hall alikubali matokeo hayo na kusema, timu yake ilipoteza mchezo huo baada ya kushindwa kuwa makini dakika tano za mwanzo za mchezo, na kuisifu Yanga kwa kusema ilicheza vizuri.

Kwa upande wake, kocha wa Yanga Ernest Brandts alikisifu kikosi chake na kusema kilicheza vizuri na pia amefurahi kuona wachezaji wake wanazidi kuimarika kila siku.

Iliwachukua Yanga dakika mbili tu kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Salum Telela aliyeunganisha mpira wavuni akimalizia kazi nzuri ya Didier Kavumbagu.

Katika mchezo huo, Yanga iliwakosa wachezaji wawili kutokana na kuumia, akianza beki Kelvin Yondan aliyeshindwa kuendelea na mchezo kufuatia kugongana na John Bocco na nafasi yake kuchukuliwa na Mbuyu Twite.

Kipa Ally Mustapha naye alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Deogratius Munishi baada ya kuumia kwenye piga-nikupige langoni kwa Yanga katika dakika ya 19.

Azam nao walimkosa mshambuliaji wao Bocco aliyelazimika kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Mwaipopo baada ya kugongana na Twite katika dakika ya 73.

Azam wangeweza kusawazisha katika dakika ya 30, kama siyo shuti kali la mshambuliaji, Kipre Tchetche kugonga mwamba wa Yanga na mpira kutoka nje, huku Jerry Tegete akipaisha juu shuti lake dakika ya 57
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. icho ndo walichovuna Azam south Africa

    ReplyDelete
  2. mambo mazuri hayaitaji haraka boda Azam wananafasi ya kushnda TPL

    ReplyDelete

Top Post Ad