ZIJUE SABABU ZINAZOFANYA WANAWAKE WENGI KUKOSA WAUME WA KUWAOWA KWA 100%

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nimefuatilia kwa kina nakujiuliza ni kwanini wasichana wengi kuolewa imekua tabu?
Na hii ni research nimefanya kwa wasichana na vijana wa kiume ili nipate majibu sahihi.
Nimekuja kugundua matatizo ya wasichana ni mengi ndio chanzo cha wao kukosa waume.

1. 
Umalaya – 
Ule wakati binti anaanza kuchanua badala ya kujitunza nakujiheshimu yeye ndio anatumia nafasi hiyo kuuchezea mwili wake kila mwanaume anayemtongoza anamkubali mwisho anajikuta ana maboyfriend zaidi ya mmoja, hapo anaanza kuangalia sasa maslahi na sio upendo wa dhati anajikuta kaingia kwenye wrong choice basi ataendelea kusakanyia mwengine na mwengine na mwengine ili akutane na right choice hapo kuna mabuzi kibao kuna waume za watu na vijana matapeli wote anabambana nao mwisho anashtukia yuko above 30 ana anza kulia ohh na mkosi sijui nuksi nk.

2. 
Maringo – Nipale wakati binti anapokua nakujishtukia kuwa yeye ni mrembo wa ukweli, basi hapoa ataanza kujisikia kuwa yeye ni yeye kudharau wengine na kujiona babkubwa na kuwa too much selective, inapotoke kijana kampenda atakapomfata huwa anamuangalia nakumuona hana hadhi ya kuwa na yeye, itaendelea hivyoooooo mwisho atakuja kukutana na kijana mtanashati wa ukweli hapo ndio atajiaminia huyo ndio mwenye hadhi yake kumbe gubegube, mpaka aje kugundua kashaumizwa anaanza sasa kuumizwa kila mara hapo ataamua sasa kujishusha na kusarandia vijana wa kawaida, kila atakae date nae anakuta ni mchumba wa mtu au mume wa mtu au bf wa mtu, hapo ndio tayari keshakua majeruhi wa mapenzi basi itabidi aishie kuchuna mabuzi fumba na kufumbua yuko above 30 anaanza kulia nina mkosi ohh nuksi nk.

3. 
Roho ya kukataliwa – samahani maana hii ipo spiritual zaidi mtaniwia radhi, kiukweli kuna watu wana roho ya kukataliwa utakuta ni msichana mrembo tabia nzuri na sifa zote nzuri anazo shida ni akwamba wachumba wanamkataa dk za mwisho, ikumbukwe huyu sio muhuni anajiheshimu na anajitambua vizuri, atapata mchumba ghafla mchumba atamtema nakwenda kwa msichana mwingine inaweza kuwa kashamvisha hata pete ya uchumba wameshatambulishana hata kwa wazazi haijalishi mwanaume atamtema tuu, hawa kwakweli ndio wanaongoza kwakujiita wana mkosi nuksi nk.

4. 
Majini Mahaba – Baadhi ya wasichana wana majini mahaba kwahiyo kuolewa kwao imeshakua ni tabu anaweza apate mchumba afe au mwanaume abadilike tabia nakumchukia au mwanaume aanze kuwa Malaya na kushindwa kumvumilia hatimaye wanaachana mauzauza yanakuwa kibao kwenye mapenzi yake mwisho anajishtukia yuko above 30 anajiona ana mkosi na nuksi.

5. 
Marafiki wabaya – Msichana anaweza kuwa haolewi kumbe marafiki alionao sio wema kwake, ukipata mchumba tayari umeshaenda kumweleza shosti wako au mashosti zako, bila wewe kujua wanampeperusha, watakuzunguka ,watatembea nae, watamtega, watakuongelea vibaya, watakuloga, watamloga, watakuharibia mpaka utaachwa kila mara usipokua mjanja ukashtuka ndio hivyo uanajikuta uko abave 30 unaanza kulia ohh nina mkosi sijui nuksi nk.
Mpaka hapo nina amini kwa wewe msichana ambaye huolewi kuna fungu lako moja kati ya hayo hapo juu, sasa chakufanya jitambue na ujipange upya kama ushapita above 30 usihofu sana hata miaka 60 wanaolewa bado.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Research yako ina maelezo machache but only TRUTH, ndio maana hawaja comment, silence means clear, keep it up uwe unawapa masomo ya maisha kama haya based on research watakao chukia TUPA KULEEE lakini wengi watajifunza.GOD BLESS U.

    By json

    ReplyDelete

Top Post Ad