google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html BILA KUWEKEZA KWENYE VIDEO MZIKI WA TANZANIA HAUWEZI KWENDA POPOTE-GODZILA | UDAKU SPECIAL

BILA KUWEKEZA KWENYE VIDEO MZIKI WA TANZANIA HAUWEZI KWENDA POPOTE-GODZILA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rapper wa Thank You, Godzilla amesema kama wasanii wengi wasipokuwa ‘risk takers’ mfano wa AY, ni vigumu muziki wa Tanzania kufanya vizuri kimataifa.

Amesema ili wimbo wowote hata kama ni mzuri uweze kwenda kimataifa, ni lazima uwe na video kali. Hata hivyo amesema video kali ina gharama kubwa.

Akiongea na Bomba FM kwenye kipindi cha Kali za Bomba, Godzilla amesema upande wa audio hatuna tatizo na huenda tukawa sawa na Nigeria ambao wametuzidi kwa kutoa video kali.

“We need quality videos, na bajeti ya quality video ni kuanzia milioni 10 huko, milioni 15,” alisema.

“Kama unataka kwenda mbali zaidi inabidi uanze kuwekeza kwenye muziki wako. Watu hawajawa willing kutoa milioni 15, nikapate video moja kwenda Afrika nzima, watu bado wanaogopa risk wakati entrepreneur mzuri ni yule anayechukua risk, yaani huogopi.” Huwezi kuwa na quality ya video ya milioni 1 ukataka kwenda kupiga milioni 800, wekeza hela nyingi upate hela nyingi.”


Aliongeza pia kuwa waongozaji wengi wa video za muziki wa hapa Tanzania hutumia vifaa duni na hivyo sio rahisi kufanya video zenye viwango vya kimataifa.
Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad