HASHEEM THABIT NOMA AMTANDIKA MCHEZAJI MWENZAKE KICHWA NA KUSIMAMISHWA KUCHEZA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mcheza kikapu ‘Hasheem Thabit’ raia wa Tanzania ambaye anachezea timu ya Oklahoma City Thunder inayoshiriki ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani maarufu kama NBA amejikuta akitumikia adhabu aliyopewa na timu yake hiyo ya kutocheza mechi moja na kukatwa mshahara wake baada ya kumpiga kichwa mchezaji mwenzake wa timu  ya New Orleans ‘Greg Stiemsma’ katika  mchezo uliozikutanisha timu hizo mbili mwishoni mwa wiki ambapo New Orleans iliibuka na ushindi wa jumla ya vikapu 105 kwa 102 dhidi ya Thunder.

Kwa mujibu wa taarifa zinasema kwamba ikiwa zimebakia dakika takribani 26 kuweza kumalizika kwa kipindi cha kwanza, Timu anayochezea Thabit ya Thunder ilikuwa inaongoza kwa vikapu 54 kwa 51 dhid ya Orleans, Thabit alijaribu kumkaba ‘Stiemsma’ hali iliyozua ugomvi baina ya wachezaji hao wawili na kuanza kupigana vikumbo hali iliyopelekea Hasheem Thabit kumpiga kichwa mlinzi wa kati wa New Orleans ‘Greg Stiemsma’ na muamuzi wa mchezo huo kupuliza kipenga kuashiria kusimamisha mchezo na kutoa foul kwa timu hizo huku akiwaamuru wachezaji hao kuendelea na mchezo.

Katika mchezo huo Hasheem Thabit aliweza kushinda Point 2 na rebounds 3 ndani ya dakika 14 alizocheza, hii sio mara ya kwanza kwa Hasheem Thabit kugombana na wachezaji wenzake kwani kipindi cha nyuma aliwahi kurushiana maneno na kutaka kupigana na mchezaji wa timu ya Houston Rockets ‘James Harden’.

Kwa wasiomfahamu Hasheem Thabit ndiye mchezaji anayeongoza kwa urefu katika ligi kuu ya mpira wa kikapu Marekani ya NBA, anakadiriwa kuwa na urefu wa Futi 7.3 ambazo ni sawa na mita 2.21 na pia ni raia kutoka Tanzania.


unaweza ukatazama video ya jinsi ugomvi ulivyokuwa hapo chini.



Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hana adabu mpira kwake kwisha kabisa muda si mrefu

    ReplyDelete
  2. Jamani mkisema hashim ndio mamba moja Kwa urefu na mume wa kloe kadashian au mtalaka wa Kim k itakuwaje?mi ndio nawaona matoluu

    ReplyDelete
  3. Admin unasifia unafikiri alichofanya ni kizuri au ni ujinga tu

    ReplyDelete
  4. MSENGE SANA HUYO DOGO,YAANI YEYE ANADHANIA HAPO YUPO SHULE YA MAKONGO? NBA NIDHAMU LAZIMA IWE MBELE NDO UTAWEZA KUPATA MAFANIKIO,AWATIZAME WATU KAMA KINA LEBRONE,DWAYNE WADE,KOBE WANAVYOKUWA NA NIDHAMU KATIKA LIGI! WAMAREKANI HAWANA MCHEZO UTASIKIA WAMEMFUNGASHIA VIRAGO VYAKE ARUDI MITAANI,YAANI MSWAHILI NI MSWAHILI TU ATA AKIWA WAPI!

    ReplyDelete

Top Post Ad