SHABIKI WA YANGA ALIYELIA BAADA YA KUFUNGWA NA SIMBA?SASA AAMUA KUJINYONGA KABISA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

In Summary
Kauli ya shabiki huyo inakuwa mzigo kwa wachezaji wa Yanga kama, Athuman Idd ‘Chuji’, Kelvin Yondani, Mrundi Didier Kavumbagu na  Wanyarwanda Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ kuhakikisha wanafanya vizuri na kuokoa maisha ya kijana huyo mwenye miaka 31.

SHABIKI maarufu wa Yanga, Steven Mwamwala amedai kuwa, kama wakifungwa na Simba mechi ya Jumapili ijayo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, atajinyonga.
Na akamsisitizia mcheza filamu, Wema Sepetu afike uwanjani kuona mechi ya Simba na Yanga Jumapili ili ampe zawadi yake ya jezi ya Yanga aliyoigharamia Sh45,000.
Mwamwala ana historia na Yanga ilipopigwa mabao 5-0 aliangua kilio cha nguvu na video zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Kauli ya shabiki huyo inakuwa mzigo kwa wachezaji wa Yanga kama, Athuman Idd ‘Chuji’, Kelvin Yondani, Mrundi Didier Kavumbagu na  Wanyarwanda Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ kuhakikisha wanafanya vizuri na kuokoa maisha ya kijana huyo mwenye miaka 31.
Aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Nimeandaa kamba ya katani kabisa, nimeificha na siwezi kusema nilipoiweka kama Yanga itafungwa mchezo huo, nitajinyonga ili kupoteza uhai wangu. Unajua inauma sana mnapofungwa, nataka timu yangu ishinde Jumapili ili niwe na amani kwa ushindi wowote ule ilimradi tutoke na pointi tatu.”
Kuhusu, Wema shabiki huyo alisema anampenda sana kama dada yake na anatamani akutane naye.
“Nimemtafuta sana na naomba siku hiyo aje kwa sababu nimemwandalia zawadi. “Nimemnunulia jezi ya Yanga na tayari nimeiandika jina la Wema, imenigharimu Sh 45,000,” alifafanua Mwamwala ambaye anaishi Tabata Segerea jijini Dar es Salaam

Mwanaspoti


Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wema ipo china baba

    we komaa na kina mwajuma tu

    ReplyDelete
  2. Usipo jinyoga wanasimba tutakugonga na gari si umetamani kufa ww ni 3 bila ili ufe vizuri

    ReplyDelete
  3. huyu ana wazimu

    ReplyDelete
  4. Ni hii mijibangi mnayovuta utotoni ndio inakusumbua kijana.

    ReplyDelete
  5. Kwa Wema umekula wa Chuya kwani itabidi usubiri mpaka hapo Diamond atakapomaliza shoo zake huko China

    ReplyDelete
  6. hili limjamaa tumetoka kjji kimoja alikua anaanguka kifafa msimuone hivyo shuleni alikuA taahira haelewi

    ReplyDelete
  7. kwakweli vichaa n wengi. Wema anavaa milion kwa mara 1 we unatangaza nmemgharamikia jezi yake sh 45,000? Jpange bab

    ReplyDelete
    Replies
    1. 45,000/ndio uwezo wake mwamwala bwege wewe

      Delete
    2. Huo sasa sio kupenda yanga Bali kukuta tamaa na maisha.
      michezo Ni burudani na upendo wala sio kifo

      Delete
  8. Huo wake ni ushabiki wa.kishamba. inavyoelekea hajui kama kwenye mpira kuna matokeo 3 yaani kishinda, kishindwa na droo. Huyo jamaa aache ushabiki wa kishamba.

    ReplyDelete
  9. Jaman mbona mmenuna?inamaana hamjui kuwa dunian kuna utani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Akamtanie mama yake. kwenye mambo ya kifo hakuna utani

      Delete
  10. Hana lolote anataka sifa tu

    ReplyDelete
  11. Hana lolote anataka sifa tu

    ReplyDelete
  12. Huyu mjinga ana ana clip yake hapa ktka u turn http://www.u-turn.co.tz/index.php?option=com_zoo&view=frontpage&Itemid=53&page=5

    ReplyDelete

Top Post Ad