PAMBANO LA SIMBA NA YANGA:SIMBA MPYA. YANGA YA ZAMANI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


ama ulikuwa hujui hivi ndivyo ilivyo! Wachezaji watano kati ya 11 wa Simba watacheza pambano dhidi ya Yanga kwa mara ya kwanza baada ya kujiunga na timu hiyo msimu huu.

Simba na Yanga zitashuka uwanjani Jumapili hii kuumana katika pambano la Ligi Kuu litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wachezaji hao ni nyota wa Uganda, kipa Abel Dhaira na beki Joseph Owino, Warundi Gilbert Kaze na Amisi Tambwe na mshambuliaji wa Tanzania, Betram Mwombeki. Dhaira, Owino, Tambwe, Kaze na Mwombeki ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba msimu huu na ambao wamejihakikishia namba kwenye timu hiyo inayofundishwa na Kocha Abdalah Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo.

Licha ya sura hizo mpya, pia kikosi cha Simba kitawakosa wachezaji sita waliocheza pambano la mzunguko pili msimu uliopita dhidi ya Yanga lililopigwa Mei 18 na Yanga kushinda 2-0.

Wachezaji hao ni kipa Juma Kaseja, mshambuliaji Felix Sunzu, mabeki Shomari Kapombe, Mussa Mude na viungo Mrisho Ngasa na Mwinyi Kazimoto.

Wakati Kaseja na Sunzu mikataba yao ilimalizika, Mude alikatishwa mkataba, Kapombe alitimkia Ufaransa kufanya majaribio ya soka la kulipwa kama ilivyo kwa Kazimoto aliyekwenda nchini Qatar, huku Mrisho Ngasa akihamia Yanga.

Hata hivyo, Yanga inayonolewa na kocha wake yule yule Mdachi Ernest Brandts inatarajia kushuka uwanjani na wachezaji 10 kati ya 11 waliocheza mechi dhidi ya Simba Mei 18.

Mchezaji pekee kwenye kikosi cha Yanga ambaye atacheza mchezo huo kwa mara ya kwanza tangu aliposajiliwa ni Ngasa mwenye mabao mawili miongoni mwa vinara wa kutikisa nyavu katika Ligi Kuu msimu huu.



Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. What's up to every one, it's really a fastidious forr me to pay a visit this web page,
    it consists of important Information.

    Alsso vist my wweb page :: diabetic dog foods (diabetesprotocol.cq491.com)

    ReplyDelete
  2. My spouse and I absolutely love your blog aand find nearly all
    of your post's to be just what I'm looking for. Would you offer guest
    writers to write content foor yourself? I wouldn't mind writing a post or elaborating on some of the
    subjects you write with regards to here. Again, awesome web log!


    my webpage - bluetooth advertising

    ReplyDelete

Top Post Ad