YANGA YATAMBA "TUTAIFUNGA SIMBA KIRAHISI KAMA KUMSUKUMA MLEVI TAREHE 20 OCT"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Ernest Brandts, amesema kuifunga Simba katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom itakayochezwa Oktoba 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ni kazi rahisi. Brandts amewatoa hofu viongozi na mashabiki wa Yanga, huku akitamba kupata ushindi dhidi ya mahasimu wao Simba. 

Akizungumza na RAI jana, Brandts alisema Simba hawamtishi kwa kuwa ana kikosi bora ambacho kina kila sababu ya kushinda mechi hiyo.

Alisema amekuwa akiifuatilia Simba mara nyingi inapocheza mechi na hakuna ushindani ambao umekuwa ukionyeshwa na wachezaji wa timu hiyo, licha ya kupata ushindi katika mechi zake.

“Simba hawana kiwango kikubwa, wanabebwa na mabao ambayo kwa bahati wamekuwa wakifunga, kikosi changu mimi ni bora, wachezaji wangu wana nguvu za kutosha na uwezo zaidi kuhakikisha tunashinda,” alisema.


Yanga tayari imewasili Bukoba kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Kagera Sugar itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Kaitaba

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. lazima tummalize huyo mnyamaaa!

    ReplyDelete
  2. SIMBA kama kawaida yetv, ni mwendo wa 5 tu

    ReplyDelete
  3. xema mnyamaaa ndo habar ya mujin hatar sanah hiyooo et simba lazima 2mkalishe mtoto wa kwny jangwa

    ReplyDelete
  4. simba wanaumeeeeeeeeee

    ReplyDelete

Top Post Ad