Akina Dada, Sio Kila Ex Wako Anayeomba Mrudiane Anamaanisha...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Sio Kila EX wako anayeomba Mrudiane anamaanisha! Wengine huomba kurudi ili wakutesti tu jinsi ulivyo Mbulula,jinsi usivyo na msimamo na jinsi ulivyo CHEAP na huna Misimamo wala Future.
Jitu mmeachana miezi 6,leo linakutesti lirudishe majeshi,na wewe ulivyo kiazi,upo-upo tu,ina maana miezi yote hii ulikuwa umeganda unasubiria rehema zake ama??


Kurudia Matapishi ya EX ukitegemea Amebadilika ni Sawa na Kupika Sufuria la Makande kwa Mshumaa,Utaambulia Masizi tu..
Kipi kipya kakiona kwako hadi arudi??Nini Kilimshinda huko nyuma ambacho leo anakiweza anataka kurudi??Akafie Mbele huko.


KUWA NA MSIMAMO,Ukisema Its Over umaanishe,sio unakuwa na hisia zinapepea tu kama Bendera ya Katibu Kata wa Kishumundu...Mtu kama Hajielewi achana nae,siku akijirudisha mwambie kwanza akapimwe Minyoo ya Kinyarwanda.
Umekazana kuwaambia marafiki zako 'Siku hizi hakuna Mapenzi ya dhati watu wote Majanga tu',nani amekwambia hayapo??Yapo sana ila wewe unatumia mbinu tofauti..Huwezi kusoma Degree ya Law halafu u-apply kazi ya Chief Accountant wa Bodi ya Tumbaku...Kila siku utasingizia Balance Sheet haina Jurisprudence..Lawyers mmenielewa!


Acha kudate watu wasiojielewa,Usidate kwa sababu uko lonely,Usiwe desperate kuingia Mahusiano kwa sababu shosti zako wanakusimulia walivyopelekwa Ruwenzori Waterfalls..Ingia kwenye Mahusiano pale Moyo wako ukiwa tayari na mtu uliyemfia kihisia na amekuwa approved na Veins,Auricles,na Aorta za Moyo wako kwamba He/She is really the One..
Unadate na mtu ambaye mustakabali wake mwenyewe haujui,ukimuuliza anataka kuwa wapi ndani ya miaka 5 ijayo anakwambia Mungu anajua dont worry,halafu BBM na Instagram unajiita Baby Ake Mie Iam in Love..Utaishia kufua boxer hadi kucha zinukie gololi!


Mbwa kamwe hashughuliki na kesi za Paka kufungiwa kabatini.Date the Right Person,With Right reasons,in a Right Time uone kama Mapenzi hayapo...

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jamaa namkubali kwaq kuimbisha

    ReplyDelete
  2. mmmmmmh maneno kuntuuu i hv to change my ways kwa kweli mana nadet kwa kuwa lonely tu khaaaaa

    ReplyDelete
  3. Mi naona sio sahh mtu lazma uwe unaxamehe kwa hyo mwanaume mwenyewe akixema nilikoxea ,mpe nafac nyingine ,hayo mawazo ya waimba mipasho ndio maana sio uhalisia wa maisha ya kimahusiano

    ReplyDelete
  4. ni kweli kabisa kama ameamua kukuacha usirudi nyuma endelea na maisha yako utavuka

    ReplyDelete

Top Post Ad