BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU IMETANGAZA KUKUSANYA MAREJESHO YA MIKOPO KUPITIA M-PESA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imetangaza kuanza kutumia huduma ya M-pesa katika kukusanyia marejesho ya mikopo kutoka kwa wanufaika hatua ikiwa ni katika mikakati ya bodi ya kuimarisha makusanyo ya urejeshaji wa mikopo hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi Bw. Asangye Bangu amewaambia waandishi wa habari wakati wa zuinduzi wa huduma hiyo mpya jijini Dar es salaam kwamba bodi inaendela kujipanga kuhakikisha inaboresha njia za urejeshaji mikopo ili kuwpatia walengwa urahisi.

Amesema mojawapo ya kazi za Bodi ni kusimamia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi waliodahiliwa kwenye vyuo vya elimu ya juu pamoja na urejeshwaji wa mikopo iliyotolewa na Serikali kwa waliokuwa wanafunzi wa elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 mpaka sasa kwa nia ya kuufanya mfuko wa Elimu ya Juu kuwa endelevu.

"Tunayofuraha kubwa sana leo kutangaza kwamba sasa wanufaika wa mikopo ya Bodi wanauwezo wa kutumia mfumo wa M-pesa kufanya marejesho ya mikopo yao moja kwa moja kwa Bodi."Alisema Bangu

Bingu amesema bodi inaimani kuwa M-pesa itawapatia urahisi wanufaika kuweza kutimiza wajibu wao kisheria wa kurudisha mikopo waliopatiwa kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu.

Amesema wanufaika wa mikopo wanapaswa kuanza kurejesha mikopo yao mara baada ya miezi 12 kuanzia wanapohitimu masomo ya elimu ya juu au wanapositisha masomo kwa sababu yoyote ile, akiwa ameajiriwa ama hajaajiriwa.

Bingu amesema wanufaika walioajiriwa wanalipa mikopo yao kupitia kwa waajiri wao ambapo hukatwa marejesho ya mikopo kwenye mishahara yao ya kila mwezi na mwajiri huwasilisha makato hayo kwenye Bodi kupitia kwenye akaunti zake huku wale ambao sio waajiriwa hupeleka huwasilisha marejesho ya mikopo katika benki za bodi.

"Wanufaika wanaorejesha mikopo yao kwa pesa taslim wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali wakati wa urejeshwaji wa mikopo yao kupitia kwenye akaunti za Benki ikiwa ni na benki hizo kutokuwa na matawi ya kutosha yaliyokaribu na warejeshaji wa mikopo pamoja na kutumia muda mwingi kwenye foleni."Alisema Bingu "M-pesa itapunguza changamoto hizo na hatimae kuwajengea mazingira mazuri ya urejeshwaji wa mikopo, Bodi inatangaza rasmi kuanza kutumika kwa utaratibu huu mpya wa urejeshaji kwa M-pesa kuanzia sasa."

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Bw. Salum Mwalim amesema kuzimduliwa kwa huduma hiyo ni mwendelezo wa jinsi ambayo huduma ya M-pesa inavyorahisha miamala nchini kuzidi kuwa rahisi.

"M-pesa imekuwa suluhisho la changamoto nyingi zinazohusiana na malipo ama miamala mengine ya kijamii na kibiashara."Alisema Mwalim na kuongeza. "Ni wazi sasa hakuna atakaekuwa na usumbufu katika kulipia mkopo wake kwenye Bodi ni kiasi tu cha kupiga *150*00# na hapo anauwezo wa kufanya mrejesho wake wakati wowote mahali popote."

"Tunaishukuru Bodi kwa kuendelea kuiamini huduma yetu ya M-pesa walianza kwa kuitumia katika ukusanyaji wa ada za uombaji wa mikopo na sasa wanakwenda mbali zaidi kwa kuichagua kuitumia katika makusnayo ya marejesho ya mikopo kutoka kwa wanufaika."Aliongeza

Mwalim amesema kwa njia hiyo ni wazi sasa Bodi itashuhudia mabadiliko makubwa kwenye makusanyo ya marejesho kwa kuwa huduma hiyo imeenea nchi nzima na hasa kwa kuwa inauwezo pia wa kumuunganisha mteja na benki yake.

"Kwa mtandao mpana wa huduma hii mawakala na na mtengamano wake na mabenki na jinsi inavyotumika ni wazi mtarajie ufanisi kwa kuwa sasa mmewawezesah wanufaika wa mikopo kuwa na uwezo wa kufanya marejesho kwa njia rahisi zaidi Wakati wowote mahali popote kwa usalama na uhakika zaidi."AAliongeza


Ili mnufaika aweze kulipia kupitia M-pesa anapaswa kwanza kuhakikisha kuwa ana taairfa ya Mkpo(loan Statement),Kiwango cha Marejesho na Nambari ya Kumbukumbu amabvyo vinapatikana ofisi za Bodi hiyo ya mikopo. Taarifa hizo zitatumika Wakati w akulipia baada ya mteja kupiga *150*00# kutoka kwenye simu yake ya Vodacom na kuchagua nambari nne ambayo ni ya malipo na kuendelea na maelekezo kadri yanatakavyokuwa akiyapata kutoka kwenye simu yake ya kiganjani.

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. BIG UP LOAN BOAD LKN MSI2MIE M-PESA PEKEE TUMIEN NA TIGO-PESA na AIRTELL-MONEY HAKATWI M2 HAPA.MAANA WENGINE VODA TULISHAIACHA KITAMBO.Niite ORUJONJOMOGO.

    ReplyDelete
  2. Hatujapata kazi mikopo tunarudishaje hebu tulieni huko

    ReplyDelete

Top Post Ad