CHADEMA WASHIKANA UCHAWI..KUMBE ANAYE KICHAFUA CHAMA MITANDAONI NI KIONGOZI CHADEMA ARUSHA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Kaskazini, kimemsimamisha Uongozi Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa  wa Arusha Samson Mwigamba kwa madai ya kukihujumu chama hicho. 
  

Taarifa ambazo tumezipata kutoka ndani ya kikao cha Baraza la uongozi kanda ya Kaskazini, kilichofanyika katika Hotel ya Corridor Spring leo usiku, zimedai uamuzi wa kusimamishwa Mwigamba umefikiwa na Kikao hicho baada ya kuwasilishwa kwa vielelezo kadhaa vya Mwigamba na yeye kukiri  kuwa ni vyake huku vingine vikimuonyesha kuwa ndiye mmiliki wa Akaunti ya Jina la ‘Maskini Mkulima’ ambalo limekuwa likitumika kukichafua chama kwenye mitandao ya kijamii.


Hakuna kiongozi ambaye amekuwa tayari kuzungumzia suala hili kiofisi, lakini taarifa za uhakika ambazo tumezipata kutokana  na maamuzi ya kikao hicho  zimebainisha kuwapo kwa maamuzi hayo pasipo shaka.


“Kikao hicho kimemsimamisha Uongozi kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili, hivyo kuanzia sasa mwigamba siyo kiongozi, nadhani tamko litatolewa baadaye,” alieleza mmoja wa wajumbe wa kikao  hicho kilichofanyika  Arusha na kuongeza kuwa katika Kompyuta yake baadhi ya maandiko ambayo yamekuwa yakikikashfu chama yamekutwa ikiwa ni pamoja IP address ya Jina na Maskini Mkulima ambalo limekuwa likituma post ndani ya Jamiiforums kukuta zinafanana.


Jina la ‘Maskini Mkulima’ lilijiunga na mtandao wa jamiiforums mnamo Desemba 27, 2011 na mpaka jana inaonyesha alikuwa ametuma zaidi ya Post 27 ikiwamo hii iliyokuwa na kicha cha habari: Wito kwa wana CHADEMA wote.



Makala hiyo ambayo ndiyo imefanikisha kumbaini ilitumwa Jamiiforums Oktoba 19 Mwaka huu chini ya kichwa cha habari cha ‘Wito kwa wana CHADEMA wote!’, 

SOMA MAKALA HIYO HAPA

Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na madhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwa wana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wachama.


Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr. Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi chama kinaenda kwa matukio.


Naandika nikiwa mwana CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Nimawasiliano baina yetu wana chadema na tunahitaji tutulie na kutafakari.


Nimekuwa mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika.

 Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake.


CHADEMA iliyopiga kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM kumshambulia mwenyekiti wakamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake nini? 


Kama chama kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu zake hofu ni ya nini? Si wasubiri kikao na kamati ya bunge katibu mkuu aende na hizo ripoti na nyaraka zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu hizo?


Napenda kabla sijaendelea mbele kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wakutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu. 

Hawakuwa madikteta na nawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kila mwanachama.


Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada ya hapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili.

 Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.


Napenda pia kumpongeza mwenyekiti aliyepo madarakani, Mbowe. Kuna mengi kakifanyia chama. Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani. 

Kakichukua kikiwa na wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49.

 Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake CHADEMA imebeba agenda nzito za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa raslimali, katiba mpya,nk.


Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Ni muhimu kwa Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo asitake kulazimisha kusonga mbele akidhani bila yeye hakuna CHADEMA. 

Akiache chama kikiwa salama, abaki kama mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao.


Leo nitaainisha mambo machache tu yanayohusiana na fedha za chama na uaminifu ili wanachadema muelewe kwa nini viongozi wakuu wa chama wamehamaki sana kusikia wanatakiwa kuwasilisha ripoti za fedha wakajikuta wanapambana na mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati na hata kufikia kusahau kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni mwenzao, ni naibu katibu mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa siku nyingine nitakapopata fursa:


1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano. 

Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. 

Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama.


Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti. 

Kama kingekuwepo leo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi.

 Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe,  bali kwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.


2. Matumizi ya fedha za chama:

Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani Mwenyekiti Taifa, katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha.

 Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. 


Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza kuu cha mwezi January kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya namajimbo na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi hayo hayajatekelezwa ipasavyo.


Nyinyi viongozi wa kanda,mikoa, wilaya na majimbo ni mashahidi wa hili . Lakini kuna michango ya watu binafsi kama Mzee Sabodo, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. 

Hapo sijataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es Salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.


3. Taarifa za fedha

Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za chama. 

Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu niliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. 

Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.


 4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama


Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. 

Mawazo mazuri kama la kuanzisha kampuni la uwekezaji la chama litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, na hivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndoto ya mchana. 

Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.


5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi


Chama chetu kinayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya sekretariat. Lakini kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu,wamekubali kuzimwa.

 Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, kadi za uanachama, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa katibu mkuu, hawana. 

Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Hivi tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye aliyenunua magari na pikipiki zote za M4C.


Hivi tunavyoongea kuna shilingi milioni 80 ambazo mwenyekiti taifa alizichukua na kuagiza kadi za uanachama tangu mwaka jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi kuonekana. 

Na mwenyekiti anafanya mambo hayo yote akitambua kwamba yeye ni mwenyekiti na hayo ni masuala ya kiutendaji ambayo yako chini ya katibu mkuu kama mtendaji mkuu wa chama na kamati yake ya tenda. Huu si ufisadi ni nini?


6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya uenezi vya chama

Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya chama na chama kinanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya chama kama bendera vinauzwa na mtu binafsi. Jambo hili linajulikana kwa Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu wake tu. 

Napenda kwanza kuipongeza kamati ya bunge kwa kuvikomalia vyama vinavyopokea ruzuku bila kujali ni chama tawala ama pinzani.


Pili namshauri CAG unaweza kutumia kampuni binafsi kwenye wizara, idara, taasisi, wakala, na asasi zote za kiserikali na serikali za mitaa kwenye ukaguzi lakini kamwe usiruhusu vyama vya siasa vikaguliwe na kampuni hizo. 

Hapo nenda mwenyewe ndo utajionea mwenyewe. Kampuni binafsi kwenye vyama huko zinafundishwa ziandikeje maoni yao. Nenda mwenyewe ujionee.


Pia kuna mkakati unaendeshwa na CHADEMA Makao Makuu kwa sasa wa kuwapigia simu viongozi wa mikoa hasa hapa Dar es Salaam na mikoa mikubwa kama Mwanza, Arusha, Mbeya, nk, wakiwataka viongozi wa mikoani mtoe matamko kumpinga Zitto. Kataeni ushenzi huu. Hili si jambo la Zitto ni la kamati ya bunge na kimsingi ni la uadilifu ndani ya serikali na vyama. 


Hata kama jambo lenyewe lingekuwa limeagizwa na Mwigulu Nchemba msingetoa matamko ya kupinga zaidi ya kuwaacha viongozi wetu wakuu watoe ripoti kuthibitisha uadilifu wao japo kidogo maana ni ukweli pia kwamba kwenye ripoti wanaweza kuzuga zikawa safi lakini ufisadi umefanyika. 

Kama ni matamko toeni matamko ya kuutaka uongozi wetu utoe hizo ripoti, na hapo ndipo mtakapo jua kwanini hampati ruzuku. Kuna matumizi mengi sana ya hovyo na ufisadi mkubwa unafanyika hapo Makao Makuu.


Nitaendelea kuwadondolea ili muone kwa nini napendekeza tuung'oe uongozi huu chini ya Mbowe.

Ahsanteni kwakunisoma!

Masikini Mkulima

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad