INAVYOONEKANA DUNIA INAPENDA DIAMOND NA WEMA WARUDIANE..ONA WANAVYOSEMWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WACHUMBA wa zamani, Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ ndiyo habari ya mjini kwa sasa, kwamba wawili hao wamerudiana tena kwa kasi kupita ile ya mwanzo, Amani limechimbua.
Habari zinasema wawili hao walikutana Dubai hivi karibuni  kabla Diamond hajaenda Malaysia na Wema akiwa njiani kuelekea Hong Kong, China ambapo walikula bata kwa sana.
Ikazidi kuelezwa kuwa wameamua kuwa kwenye uhusiano wa siri na lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha mpenzi wa sasa wa msanii huyo wa Bongo Fleva, Penniel Mungilwa ‘Penny’ hajui kitu chochote.

TAARIFA ILIVYO
Kwa muda wa siku nne, ndani ya mitandao ya kijamii hasa kwenye Instagram, maneno yenye kuashiria kuwa wawili hao wapo pamoja tena yamekuwa yakichukua nafasi.
Baada ya kusambaa kwa habari hizo, Penny naye alitupia picha yake akiwa kitandani na Diamond na kuandika kuwa waachwe kama walivyo.
Ndani ya mtandao wa Instagram yakazuka makundi mawili, upande wa mawifi wa Penny, akiwemo Halima Kimwana na kundi lingine la mawifi wa upande wa Wema.
Kundi la Wema waliandika kuwa mwanamke anayependwa na ndugu wa mume siku zote mwanamme huwa hampendi hivyo Wema ni mpenzi sahihi wa Diamond kwa vile hapendwi na ndugu kama Penny.

MBAYA ZAIDI
Mbaya zaidi, katika hali isiyotegemewa kwenye akaunti yake ya Instagram, Wema alitupia wimbo mpya wa Diamond uitwao My Number One na kuweka maoni yake kwamba anaupenda wimbo huo.
Wengine waliochangia walisema Wema ana lake jambo kwa Penny kwa vile si jambo jepesi kusifia wimbo wa mwanamme ambaye alikuwa mpenzi wake na sasa ana mwingine anayejulikana, yaani Penny.

PICHA YA WEMA SASA
Wema hakuishia kuposti wimbo huo tu, alikwenda mbele zaidi kwa kutupia picha yake yenye pozi tamu na kuuliza; huyu hapa baby wa nani huyu? (yaani yeye).
Wengi walimsifia lakini wengine walifunguka kwa kusema ni baby wa Diamond, jambo ambalo Wema hakulipinga.

PENNY AONGEA NA AMANI
Kufuatia kuenea kwa habari hizo, Amani lilianza kuwasaka watu watatu ambao ndiyo wenye uwezo wa kubainisha ukweli au uongo wa ishu hiyo iliyoenea mjini.
Watu hao ni Diamond mwenyewe, Wema anayedaiwa kurudiwa na Penny, mpenzi wa sasa wa Diamond.
Wa kwanza kupatikana alikuwa Penny ambapo alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa madai hayo alifunguka:

AKIRI KUNYETISHIWA
“Ni kweli hata mimi nimenyetishiwa habari hizo lakini siamini kama inawezekana hao watu wakarudiana.

ASEMA KUNA KUNDI LINAPANGA NJAMA
“Nijuavyo mimi kuna kundi la watu ambao wapo upande wa pili (wa Wema) ndiyo wanaoeneza hizo habari, pengine wanataka niamini kisha nimwache Diamond, simuachi ng’o.

ANATAKA USHAHIDI 
WA PICHA
“Kama niliweza kumvumilia kwa kuona picha akiwa na Irene Uwoya hotelini sembuse hili la safari hii hata picha hakuna?”

ALISHAMUULIZA DIAMOND
“Mimi nilishamuuliza Diamond, japo hakusema ni kweli au uongo ila aliniambia achana na hizo habari.”

DIAMOND APIGA KIMYA
Baada ya kuongea na Penny, 
 lilimpigia simu Diamond ambapo alipokea na kusema yuko kikaoni na kumtaka paparazi kupiga baadaye. Hiyo ilikuwa saa 4:16 asubuhi ya juzi.
Saa 7:11 mchana, Diamond alipigiwa simu tena lakini hakupokea. Akatumiwa meseji ya kumkumbushia, hakujibu. Akatumiwa meseji yenye madai ambayo pia hakuijibu.

MAMA WEMA KABLA YA KUULIZWA AFUNGUKIA MADAWA YA KULEVYA 
Amani liligundua Wema bado yupo Hong Kong hivyo liliamua kumpigia simu mama yake, Bi. Miriam Sepetu ili kuomba namba ya bintiye, lakini kabla ya ombi hali ikawa hivi:
“We nani, hivi kuna gazeti moja limeandika eti mwanangu amekamatwa na madawa ya kulevya China anasubiri kunyongwa, ni akina nani wale, wana akili kweli?
“Mimi sikubali safari hii, tutafikishana kwa mwanasheria wangu. 
“Tena ukikutana nao waambie waache kumzushia mwanangu, wasimtie mkosi bure, hajakamatwa yupo salama kabisa.” 
Mpaka sasa ushahidi wa kuonesha wapenzi hao wa zamani kuwa  wamerudiana bado haujawekwa hadharani.

GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acha kudAnganya watu Dunia inawajua Hawa? Hata Kijiji cha Chandarua Songea. Hawawajui Hawa sembuse Dunia?

    ReplyDelete
  2. Acha ujinga huyo wema na diamond ndy kina nani?

    ReplyDelete
  3. Acha ujinga huyo wema na diamond ndy kina nani?

    ReplyDelete
  4. Woww na warudianeee jaman ntafurahii sio hilo bb vaa kiremba

    ReplyDelete
  5. mimi nitafurahi sana wakirudiana

    ReplyDelete
  6. Best couple dunia nzima... Yani wema na diamond ni zaidi ya beyonce na jigga.... Yani ni mapenz yasiyotumia nguvu kabisaaaa

    ReplyDelete

  7. Penny don't fool ur self unategemea kwa akili yako Diamond atakwambia ukweli wake. Jiulize swali ya kwamba Hao wengine aliowahi kuwa nao aliwahi kuwaambia ya kwamba ana mabibi pembeni! AMA kweli umekuwa kipofu.amini usiamini usijisifie eti uko peke yako.cku ukimwagwa cjui utatembelea mitaa gani.ni afadhali kuwa kimya never say never.kwanza kabisa big percent ya watanzania hawakutegemea Kama Wema angeachwa.

    ReplyDelete
  8. Nyie mwachen,amwuli yaliyo mpa diva,uctaa unawatesa sana wanawake,iv mnadha peny angekuwa na mtu wa kawaida angekuwa mtumwa hivo?angeshatimua vumbi mapema sana

    ReplyDelete
  9. Habar nilovyoona sosi ni global hata cjaangaika kusoma ninavyowachukia!

    ReplyDelete
  10. Najua washarudiana ila naomba muwe waz mtupe raha mashabiki wenu huyo pensel sie ht hatumjui jmn tunaemjua sis ni wema,yan siku mkieka wazi sjui ht ntaakuaje mie mtoto wa marehem,diomond usijiazimishe kumpenda huyo et kisa familia inamkubali wema alikupenda kwanza atiiii

    ReplyDelete
  11. ukweli hata mimi ninayoandika hapa nilikuwa napenda sana hiyo couple ya wema na diamond yaani wakirudiana nitafurahi sana uafikiri nina undugu nao lakini sinao ila hiyo couple ilikuwa poa sana inapendeza kwakweli yaani sasa hivi watanzania wakiambiwa pigeni kura nani anafiti kati ya penseli na wema wa mamaa ni wema atapata kura nyingi sana beliave me so kama kweli wamerudiana ni vizuri sana kwani huyo penseli alimuumiza sana mwenzie na ukizingatia walikuwa marafiki kweli waswahili walisema rafiki ni mkia wa fisi sasa ni wakati wa penseli kulia movie ndio kwaanza imeanza i can wait jamani afanye kweli tumechoka kusubiri

    ReplyDelete
  12. Warudianeeeeeeee yeeees....Peny kwisha habari yako

    ReplyDelete
  13. daaaa wema arudiane 2 na diamond a apriciat them

    ReplyDelete
  14. uhawara huishi

    ReplyDelete

Top Post Ad