JE UNGEKUWA WEWE HAPA KATIKA SITUATION HII UNGEFANYAJE?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Umefukuzwa kazi kampuni ya upimaji Almasi, waijua almasi nje ndani. Sasa una shida sana yaani hivi karibuni kila kitu kimekuwa kigumu, umeshakopa sana na hata huaminiki tena na marafiki zako, hivyo ukikopa tena wanakutolea nje. Ukaona heri umshawishi rafiki yako akusaidie walau mkopo. Akakwambia yeye analima viazi, na sasa ni kipindi cha kulima, mkopo hana ila atakupa shamba hekari moja, ulime, atakupa pembejeo zote, kumwagilia hamna ni mvua tu, na utakula msosi kwake mpaka viazi uvivune uviuze, ambapo utapata pesa ya kujitegemea kula na kupanua kilimo kwa kukodi mashamba makubwa msimu ujao, yeye utampa 10% tu ya mavuno ya hekari hiyo aliyokupa, na anakupa business plan nzima ya ulimaji viazi, huna haja kum-Doubt maana yeye viazi ndo mpango mzima, yupo njema kweli hadi anaitwa "Sudi Maviazi" Kariakoo nzima wanamjua. Unakubali. Siku ya kwanza umefika shambani umepiga jembe hatua 3, ukachimbua kipande cha almasi...kwa uzoefu wako ni cha kama 100m/= hivi, je, Utatupa jembe ukimbilie mjini kuiuza?, ukulima tupa kule, ama utaendelea na ukulima bene bene na Sudi Maviazi?

-Bwana Mushi
Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. nitaendelea kulima

    ReplyDelete
  2. kwa sabab alikua ana nia ya kunisaidia bac inabid nika mwambie nme shndwa kuendelea ngoja nika chek michakato mbele, Afu ndo naenda kuuza kwaku2lia

    ReplyDelete
  3. itabidi uuze kwaza halafu umpe kama msaada maana alikua na lengo lakusaidia pia ukimwambia kabla akakugeuka akakuua mi sijui

    ReplyDelete
  4. Jembe la nini tena wakati nishapata shot cat, nilikuwa na mpango wa kulima kwa kwa kukosa pesa sasa nishapata milion 100 nalima nataka nini tena,

    ReplyDelete
  5. Utaendelea tu madhali umeiona jua kuna nyengine zaid ya hiyo kma na shamba lenyewe unalinunua toka kwa sudi mapapatato

    ReplyDelete
  6. Ntakubali kulima coz kwa baadae naweza kupunguza shida na hayo madeni.

    ReplyDelete
  7. Sijajua mantiki ya hii stori!

    ReplyDelete
  8. Nitakufa hapohapo

    ReplyDelete
  9. Akachimba chimba akapata yooo.alimas alinacha bin abunuas

    ReplyDelete

Top Post Ad