MASKINI:CHINJA CHINJA WAUA KIKONGWE KWA MAPANGA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mauaji ya kikatili yanayodaiwa kufanywa na Kikundi cha Chinjachinja dhidi ya vikongwe, yamezidi kuutikisa Mkoa wa Geita baada ya kikongwe mwingine, kuuawa kwa kukatwa kwa mapanga akiwa nyumbani kwake.

Marehemu huyo ametajwa kuwa ni, Maua Ikoti(60) mkazi wa Kasang'hwa, wilayani Geita .

Mauaji hayo yamekuja huku takwimu zikionyesha kuwa  vikongwe watatu, wameuawa na kikundi hicho katika kipindi cha wiki nne zilizopita.

Baadhi ya watu wanahusisha maujai hayo  na imani za kishirikina.

Tukio la mauaji hayo lilitokea saa 6 usiku wa kuamkia juzi  baada ya wauaji  kuvamia familia hiyo na kisha kuingia ndani ya chumba alimokuwa amekala kikongwe huyo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kasang'hwa, Maganiko Ndiomali, alisema wauaji walimkata kwa mapanga kikongwe huyo kichwani,mikono na kwenye matiti.

Alisema pamoja na mayowe yaliyopigwa na watoto wa marehemu ili kuomba msaada, juhudi za wananchi kuwasaka wauaji hazikuzaa matunda.

Kuna madai kuwa kikundi kinachohusishwa na mauaji hayo kimekuwa kikodiwa na baadhi ya watu ili kulipiza kisasi baada ya kufiwa na ndugu zao wakiamini kwamba wamerogwa.

Kikundi hicho kinadaiwa kuhusika na mauaji ya kikatili dhidi ya Mondesta Nchambi (53) mkazi wa kitongoji cha Isabilo wilayani Chato kwa kumchinja mithili ya kuku.


Kamanda wa polisi mkoani Geita,Leonard Paulo alithibitisha kuwepo kwa matukio hayo lakini alisema hadi sasa hakuna mtu au watu waliokamatwa wakihusishwa na mauaji hayo.
Source-Mwananchi
Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. duuh! nouma kwel, wa2 kaa hawajui km kuna moto wa milele uko kwa mungu?

    ReplyDelete
  2. Huo ni wizi mtupu kwa kazi ipi anayoifanya si bora hyo pesa wawagawie walimu wanaowatengeneza na wakawa vle.

    ReplyDelete

Top Post Ad