MSHAHARA WA RAIS KAA LA MOTO..SEREKALI YASEMA ZITTO ALIKOSEA KUTAJA MSHAHARA WA MTU

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam. Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe kutaja hadharani mishahara ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, serikali imekataa kuizungumzia mishahara hiyo.

Msimamo wa Serikali kutotaja mishahara ya viongozi wakuu unatofautiana na utamaduni wa nchi nyingine kama Marekani, Afrika Kusini, Ufaransa na Kenya ambazo mishahara ya wakuu wake huwekwa wazi kwa umma.

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema akiwa wilayani Igunga Mkoani Tabora, alisema Rais Kikwete anapokea zaidi ya Sh30 milioni kwa mwezi (sawa na Sh360 milioni kwa mwaka) ikiwa ni marupuru na mshahara kwa mwezi bila kodi, huku Pinda akipokea Sh 26 milioni kwa mwezi.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani alisema kiongozi yeyote haruhusiwi kutaja mshahara wa mtu mwingine kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya utumishi wa umma.

“Kuutaja mshahara wa mtu mwingine ni kinyume cha sheria na kosa, siyo utaratibu. Kwani wewe upo tayari watu waujue mshahara wako?” alihoji.

Aliongeza kuwa ingawa mishahara ya viongozi hao inatokana na kodi za wananchi, sheria ndiyo inayozuia watu kuyataja malipo hayo hadharani na kwamba hayupo tayari kuutaja mshahara wa rais au kiongozi mwingine labda mtu huyo autaje yeye mwenyewe.

“Siwezi kutaja mshahara wa bosi wangu wala wa kwangu mwenyewe. Wewe unaujua mshahara wa Obama (Rais wa Marekani)?” alihoji tena.

Akizungumzia mishahara ya marais wa nchi nyingine duniani kuwekwa wazi, Kombani alisema kila nchi ina utaratibu wake na kwamba Tanzania haijafikia hatua hiyo.

Alipotafutwa kulizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue simu yake ya mkononi iliita bila kupokewa. Gazeti hili pia liliwasiliana na Naibu Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza Idara ya Mageuzi ya Kilimo Ofisi ya Rais Ikulu, Peniel Lyimo ambaye alisema yeye si mhusika. “Masuala yote yanayohusu utumishi yapo Wizara ya Utumishi,” alisema Lyimo.

Akianika mshahara wa Waziri Mkuu, Zitto alisema kwamba kiongozi huyo analipwa Sh11.2 milioni kama mbunge, Sh8 milioni kama waziri na Sh7 milioni kwa nafasi yake ya Waziri Mkuu, hivyo, kumfanya kupokea zaidi ya Sh300 milioni kwa mwaka.

Hata hivyo, Kombani alilionya gazeti hili kuandika taarifa za mishahara ya watu kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa.


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Bashiru Ally alisema Mwalimu Nyerere aliwahi kutaja mshahara wake hadharani na kuhoji viongozi wanaotaka mishahara yao isitajwe wanaficha nini


“Hata wakificha mishahara yao bado wananchi wataona maisha wanayoishi kuwa si safi,” alisema.



Wanaharakati pia wahoji

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba alisema siyo kosa kwa mtu yeyote kutangaza mshahara wa viongozi wa umma kwa kuwa wanalipwa kutokana na kodi za wananchi.

Aliongeza kuwa kuanzisa sasa atakuwa balozi wa kutangaza mishahara ya viongozi hao, ili kila mwananchi aweze kufahamu kama ambavyo imekuwa ikifanyika katika nchi nyingine duniani.

“Ninachojua mimi ni kuwa dhana ya mshahara inataka kuwepo na siri baina ya mwajiri na mwajiriwa, lakini si kwa viongozi wa umma ambao wanalipwa na kodi za wananchi. Kuanzia sasa hivi nitakuwa balozi wa kutangaza mishahara ya viongozi hao ili kila mtu ajue,” alisema Kibamba.

Katibu Mkuu wa Tanzania Labor Party (TLP), Jeremiah Shelukindo alisema ni vyema kila mtu akaheshimu sheria inayozuia kutaja mshahara wa mtu mwingine kwa kuwa kitendo hicho kinaweza kuwaudhi baadhi ya viongozi wa umma.

“Si vizuri kuingiza siasa kwenye mambo ya mishahara. Siyo mara ya kwanza kusikia watu wakijaribu kutaja mishahara ya watu wengine huko ni kukiuka sheria,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa asasi ya Sikika, Irenei Kiria alisema umefika wakati ambapo inabidi uanze kufanyika mchakato wa kuzibadili sheria zinazolenga kulinda masilahi ya viongozi wa umma.


“Tunataka kujua viongozi wanalipwa shilingi ngapi na kwa nini wanalipwa kiasi hicho,” alisema Kiria.


Nchini Marekani, mshahara wa rais unajulikana tangu mwaka 1789 kiongozi wa nchi hiyo alipokuwa analipwa Dola 25,000 kwa mwaka.

Kuanzia 2001 hadi sasa, Rais wa Marekani analipwa Dola 400,000 (Sh 640 milioni) kwa mwaka, sawa na Sh 53.3 milioni kwa mwezi.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma analipwa Randi 2 ,917 038 sawa na zaidi ya Sh400 milioni za Kitanzania kwa mwaka, Rais wa Ufaransa, Francois Hollande Sh475 milioni, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron Sh338 milioni, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Sh277 milioni na Rais wa Namibia, Hifikepunye Pohamba Sh226 milioni kwa mwaka.

Wengine na malipo wanayopata kwa mwaka ni Marais wa Urusi, Vladimir Putin, Sh174 milioni, Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia Sh137 milioni, Michael Satta wa Zambia, Sh126 milioni, Rais wa Angola, Jose dos Santos Sh91 milioni, Rais wa Lesotho, Profesa Pakalitha Mosisili Sh88 milioni, Armando Guebuza wa Msumbiji, Sh84 milioni na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping Sh60 milioni.


Wengine ni Rais wa India, Pranab Mukherjee Sh49 milioni, Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe Sh27 milioni, Naibu Rais wa Afrika Kusini, Kgalema Mothlanthe Sh331 milioni, Waziri Mkuu wa Namibia, Nahas Angula Sh160 milioni, huku Baba Mtakatifu wa Kanisa la Romani Catholic, Papa Benedict XVI akifanya kazi bila kulipwa mshahara.

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duuh Mugabe na udicteta wake wore anapewa ml 27 ?

    ReplyDelete
    Replies
    1. yule ndiyo mzalendo wa kweli,na ndiyo maana atatawala hadi kufa

      Delete
    2. Mugabe sio dictator mkuu, ila ni mtu mwenye misimamo yake hakuna msenge yeyote wa kizungu au afrika anaweza mbabaisha hata kama kwa kufanya hivyo atalala njaa na watu wake. Ni aina ya watu kama Nyerere hivi ila tofauti yake na Mwalimu ni kwamba yeye amezidi ungunmu, vyombo vya magharibi ndio huweka picha mbaya juu yake bt jamaa ni mzalendo haswaaa.

      Delete
    3. Nakubaliana na wewe mdau kuwa raid Mugabe Ni kiongozi mzuri tens asiyefuata upepo WA ulaya wala America. Natamani Tanzania tungepata kiongozi mwenye msimamo kama Mugabe. The man has done so much for his country Zimbabwe

      Delete
  2. Kwanini wakatae kutaja mishahara yao ili hali hawakatwi kodi. Looh sh.mil 30. Wakati mpiga kura wake hata kula yake ya siku haijulikani.halafu pay asyou earn anapunguza asilimia moja.ndio maana wanaishi kama wapo peponi.big up zitto endelea kutupasha.tuambie na kombani anapata bei gani

    ReplyDelete
  3. Piga hesabu kombani 19.2 per month 11.2 as mbunge na 8 ya uwaziri mtatuuaaa viongoziwe wetu kheeee,,

    ReplyDelete
  4. Alooh. Ndio maana hawataki mishahara yao ijulikane ili wajifanye kua tuko nao sawa. Wanajipangia mishahara mikubwa halafu watumishi mishahara mshahara mpaka may mosi ndio wawaongeze kiduchu na kodi juu kweli hawa si wenzentu .tukilalamika maisha magumu hawana lakusema.

    ReplyDelete
  5. Na zitto, mbowe na slaa wanapata sh ngapi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimekupendaje mdau na wenyewe waweke hadharani mapato yao..

      Delete
    2. Rais mstafu ali hasan mwinyi aliweka waz mshahala wake na hali ile ilikuwa zamani kwani kunatofauti gani na sasa tusileteane siasa mama celina kombani usiogee kwakuwa upo ndani ya madaraka ongelea really kinachotakuwa kuelezewa kwamba rais analipwa kiasi flani kama mh zito alikosea kutaja we lekebisha tu cyo kuanza kusema kutaja mshahala wa mtu cyo haki mbona wabunge wanajulikana wanalipwa bei ngani na wamechanguliwa na wananchi raisi kwani kajichangua mwenyewe...na ww katibu mkuu wa TLP usiogee tu kama huna kichwa mtanzania anashindia dolla moja alafu acjue mshahala wa kiongozi wake kivp yeye analipa kodi lazima ajue pesa yake inatumika vp

      Delete
  6. Kumamae walai wanyonge hatuna chetu kwa style hiyo kwann wafiche mishahara yao wakat ya walimu inajulikana wana roho mbaya sana hao zitto baba kamua nawachukia mm hao na kura yangu ni kwako.

    ReplyDelete
  7. I hate my president

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole but he doesnt knw kma una exist......too bad

      Delete
  8. kweli inauma sana tena sana...yaniiii jamani mjue naskia kulia! Afu kwanin walimu mishahara yao itajwe alafu wao ictajwe.jamani jamani walaniwe aise

    ReplyDelete
  9. Kama Nyerere aliweka hadharan mshahara wake, hawa wengine kwa nini wafiche? Bas mafisad

    ReplyDelete
  10. Dah! Zito anafaa kuwa Rais wa hii nchi, unatusaidia kutufumbua mengi yaliofichika, Yaani nchi maskini kama hii Rais analipwa hela nyingi kiasichi hicho? Wakati nchi ilioko juu kiuchumi kama China rais analipwa robo tatu ya ya huo mshahara sh ml. 60 kwa mwaka? Sio siri ndio manake hawataki watangazwe hadharani ni aibu kwa taifa

    ReplyDelete
  11. Hii ni Tanzania,Mwl hana issue na ndio maana mshahara wake anaujua mpaka Mwnf wa Cheke ila mshahara wa Peprezidaa anapaswa kujua ni First Lady na siyo mwingine,acheni dharau nyie viongozi wetu kwanini wenzenu mnawafanya kama hawana haki yeyote na kujiona nyie ndo kila kitu?

    ReplyDelete
  12. HALAFU HUYU MAMA MI SIMPENDI HATA KIDOGO,KWANZA KIINGEREZA CHAKE NI CHA UGOKO! HALAFU SIJUI ANA MASLAHI GANI NA JK,MAANA KILA BARAZA LA MAWAZIRI LIKIPANGULIWA YEYE NDANI WAKATI HATA UWAJIBIKAJI WAKE HAUONEKANI!

    ReplyDelete

Top Post Ad