DENTI WA MIAKA 12 APACHIKWA MIMBA HUKO KIPUNGUNI JIJINI DAR

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Binti wa Darasa la sita katika Shule ya Msingi Kilimani iliyopo Kipunguni, Dar mwenye umri wa miaka 12 (jina tunalihifadhi kwa sababu za kimaadili) amejikuta akishindwa kuendelea na masomo baada ya kupewa ujauzito na kijana wa mtaani aliyejulikana kwa jina moja la Roja.

Akizungumza kwa huzuni mama wa mtoto huyo, Aziza Mohammed alisema kuwa mwishoni mwa mwezi uliopita ndiyo aligundua kuwa binti yake huyo ni mjamzito na ilikuwa ni baada ya kukataa kwenda shule huku akitapika mara kwa mara.
Mama huyo alisema, baada ya kuona ilibainika kuwa ana mimba, wakanipa taarifalili hizo  aliamua kwenda kununua kifaa cha kupimia mimba lakini mwanaye huyo alikimbilia kwa mama yake mdogo, Temeke ambako waligundua kuwa ni mjamzito.
 “Alipofika kwa mama yake mdogo, nikawaomba wamlete kisha tukampeleka hospitali ambako tulithibitishiwa na daktari kuwa kweli ana ujauzito wa miezi mitano,” alisema mama huyo na kuongeza:
“Nilimbana aniambie mwenye mzigo huo ambapo alimtaja kijana aitwaye Roja. Akaniambia kijana huyo ambaye ni jirani yetu amekuwa akimbaka na kumtishia kumuua ikiwa atasema.
“Kwa maelezo hayo ilibidi tumtaarifu mjumbe wa mtaa wa Kipunguni B, Bakari Issa ambaye tulikwenda naye kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari na kufungua jalada la kesi lenye namba STK/RB/18639/2013 KUMPA
 MWANAFUNZI MIMBA
“Jamani naomba taasisi husika zinisaidie kwa sababu baada ya kutoa ripoti polisi nimekuwa nikuzungushwa tu...mtuhumiwa hakamatwi.”
 SIMULIZI YA KUSIKITISHA
Binti aliyepata dhahama hiyo alipata kuzungumza na Ijumaa ambapo alisimulia simulizi ya kusikitisha sana ikionesha jinsi mchezo mzima ulivyokuwa.
Alisema: “Wadogo zake Roja ndiyo walikuwa marafiki zangu...Roja alikuwa akiwatumia wao kuniita kila siku jioni na nilipoenda alikuwa akinifungia chumbani kwake na kunilazimisha kufanya naye mapenzi huku akinitishia kuwa nikisema ataniua.
“Pamoja na vitisho hivyo alikuwa akinipa shilingi elfu tatu hivyo nikawa naogopa kumwambia mama na nilipogundua nina mimba nilimtuma wifi yangu (dada wa Roja) akamwambie lakini akakataa na kusema mimba siyo ya ndugu yake, mimi sijawahi kufanya mapenzi na mwanaume mwingine zaidi yake,” alisema binti huyo.
 KUTOKA IJUMAA
Tukio hili linaumiza na kusikitisha. Ni wito wetu kwa taasisi husika kufuatilia sakata hili na kumsaidia binti huyu ambaye ndoto zake zimezimwa ghafla akiwa bado mdogo.

Aidha, ni vyema wazazi wakawa makini katika kufuatilia nyendo za watoto wao kabla mambo mabaya hayajawakuta.
Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. C nishabiki wa Chelse ndomana,afu alie mpa uo ujauzito atakua shabiki wa Arsenal

    ReplyDelete
    Replies
    1. teh teh masiara hayo

      Delete
    2. Kwanza kwa nini waweke jersey ya Chelsea? Kwani wachezaji WA Chelsea ndo wnafanya hayo mambo...,eh pole dada kwa majanga,ILA tubadilike mtoto ea mwenzio Ni Wako...,

      Delete
  2. Hiv wabongo 2taelimika lini jaman? duuh...

    ReplyDelete
  3. kayataka mwenyewe huyo km kwel alkuwa hapend amekufanyia ktendo hcho kwa mala ya kwanza akkuita uclud tena lkn unaitwa na unaenda umependa uc2ongopee

    ReplyDelete
  4. Wabongo mtakuwa lini lkn kila siku kutukana watu na kuandika ujinga katika mambo yakusikitisha!

    Mi niliozeshwa nikiwa na umri wa miaka 13 nilikuwa mtoto na nikaaharibiwa maisha yangu mpaka leo imekuwa ngumu kwangu kuwasamehe wazazi wangu kwa kuninyima haki yangu kama mtoto. Very sad!

    Ushauri wangu nindeni kwao na huyo kijana myaongele hayo matatizo nakumsaidia huyo binti..TZ hakuna sheria kwa asie kuwa na pesa ! Poleni sana wazazi wa huyo binti na msimtenge huyo binti bado mtoto alikuwa hajuwi atendacho karubuniwa tu. Inauma kusema kweli, umaskini ulaaniwe !

    ReplyDelete
  5. duuh huyo jamaa nae hata atafut watu wazma wenzye pia sasa ivi pia watoto wa sasa ni kizaz cha laana kwann alikataa kupima mimba had akakimbilia hko Tmk kwann alivyo ona mabadiliko ya kimwil hakumwa mbia mamaye sasa nn alicho kuwa ana kificha??

    ReplyDelete
  6. Duh!! We mwenye blog mimba haipachikwi eeeh! Utapachika chaja kwenye socket sio mimba tumboni, nakuomba uwe unatumia kiswahili fasaha ili kukuza lugha hii ya kibantu,

    ReplyDelete

Top Post Ad