NGASSA ARUDI AZAM, AUNGANA NA MWAIKIMBA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Na Khatimu Naheka
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa ameikumbuka timu yake ya zamani ya Azam FC baada ya kuonekana akiwa kwenye Uwanja wa Chamazi Complex nje ya jiji la Dar es Salaam.
Ngassa, ambaye awali aliuzwa na Yanga kwenda Azam FC kwa kitita cha pauni milioni 98, miaka mitatu iliyopita kabla ya kurudi msimu huu, juzi alitua kwenye Uwanja wa Chamazi na kushuhudia mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji na Mgambo Shooting.
Ngassa aliyeondoka Azam FC kwa mgogoro huku timu hiyo ikimpeleka Simba, alikuwa kivutio na wengi walianza kuonyeshana alipokuwa amekaa jukwaani.
Baada ya kufika uwanjani hapo, moja kwa moja Ngassa alikwenda kukaa alipokuwa amekaa mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba waliyewahi kukipiga pamoja Jangwani.
Mara baada ya mechi hiyo, kiungo huyo aliyerudi kwa kasi katika Klabu ya Yanga, kwa kuifungia bao moja mpaka sasa, alisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo na kuondoka zake.
Ngassa alipoulizwa sababu za kwenda uwanjani hapo alisema kwa ufupi: “Nimekuja kutembea tu.”

Tayari Ngassa yupo mjini Bukoba kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya wenyeji Kagera Sugar, kesho.
GPL
Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. eti kitita cha pauni milioni 98 afu RONALDO NA MESSI WATAUZWA PAUNI MILIONI NGAPI?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwandishi kanjanja hata zingekuwa ni tz milions hakuuzwa kwa hela hiyo!.afu kwenda uwanjan sio kurud timu mnatupotezea muda kusoma ujinga wenu!

      Delete
  2. achen mambo yenu milion hamsin et paun 98 kama hujui c uache

    ReplyDelete

Top Post Ad