RAY C ANARUDI KWA VISHINDO AMPA KIPIGO CHA MWAKA NORA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Na Musa Mateja

KATIKA hali ya kushangaza, siku chache baada ya kuripotiwa kupona na kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ anadaiwa kugeuka mwanamasumbwi na kumpa kipigo mwigizaji Nuru Nassoro ‘Nora’, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wiki iliyopita ndani ya studio moja ya kurekodia muziki iliyopo Kinondoni, Dar ambapo wawili hao walikutana walipokwenda kurekodi ngoma zao.
Ilidaiwa kuwa akiwa studio hapo, Nora alikutana na Ray C ambaye pia alizama mahali hapo bila mawasiliano na prodyuza anayemtengenezea ngoma mpya.


Chanzo hicho kilipasha kuwa baada ya Ray C kuingia studio hapo alimkuta prodyuza huyo akiandaa ngoma ya Nora ambapo alihoji kilichompeleka mwigizaji huyo mahali hapo.

Ilidaiwa kuwa prodyuza huyo ambaye jina halikupatikana alimwambia Ray C kuwa Nora alifika kurekodi wimbo wake.

Ilisemekana kuwa Ray C hakuridhishwa na majibu hayo, akaomba asikilizishwe ngoma hiyo ya Nora lakini baada ya kusikiliza ilidaiwa kwamba Ray C aliiponda mbele ya Nora, jambo ambalo mwigizaji huyo hakufurahishwa nalo.
Ilidaiwa kuwa Nora alipandwa hasira na kujikuta akimjibu mbovu Ray C.

Habari ziliendelea kutiririka kuwa siku hiyo walimalizana kwa kusonyana na siku iliyofuta walikutana tena studio hapo ambapo Ray C alidaiwa kutinga akiwa ‘masanga’.
Ilisemekana kuwa alipomuona Nora alianza kumpa vijembe, jambo lililosababisha Nora kushikwa hasira ndipo wakavaana na kuzichapa.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa Ray C ndiye aliyeibuka bingwa wa ndondi hizo kwa kumtwanga Nora hadi kumvimbisha jicho kabla ya maprodyuza na watu wengine kufanya kazi ya ziada kuwaamulia.
Ilisemekana kuwa baadaye Ray C alitolewa nje ndipo akahamishia hasira kwenye gari la Nora aina ya Toyota Vitz kisha akalivunja kioo na kutambaa zake.

Baada ya kupenyezewa ‘niuz’ hizo gazeti hili lilimtafuta Nora ambaye alikiri kutokea kwa sekeseke hilo huku akibainisha namna alivyoumizwa jicho lake na kuvunjiwa kioo cha pembeni cha gari lake.
Aliongeza kuwa siku hiyo alipoteza pochi wakati wa ugovi huo.

“Ray C alinikuta studio nikifanya wimbo, kilichonishangaza baada ya kuniona tu alibadilika ghafla.
“Nilijua angenishauri kwa kuwa ndiyo ninaanza gemu kumbe mwenzangu alifikiria vingine,” alisema Nora na kuongeza:
“Mbali na kuniumiza jicho lakini alinifanyia mambo ya ajabu sana, kama kusingekuwa na watu wa kutuamulia basi chochote kingetokea.

“Sikwenda kuripoti polisi. Niliamua kusamehe kwa sababu kuna watu walinisihi niachane naye kwa sababu bado kuna mambo yanamwendesha. 

Kwa upande wake Ray C alitafutwa kwa kila njia kupitia simu ya mkononi na kumvizia studio lakini hakupatikana hivyo juhudi za kumpata zinaendelea.

Source:GPL

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Cmuelewi huyu Rayc kaponea msaada mayb saahi angekua na jina la ziada Marehem Reyc!! Hana aibu?? Alitakiwa aonyeshe utu kwa watu like alivyo onewa huruma akapewa msaada akapata hizo nguvu zakujifanya CHEKA kwa wenzie? I wish Jakaya asingekysaidia coz haya ndo malipo yako kwa jamii hiv umepona kwel? Husikiki kwa mazuri ww? Malaya mkubwa ww!

    ReplyDelete
  2. Anatafuta kiki huyo ya kurudi kwenye gemu na kwa taarifa yake ata akirudi si kama zaman

    ReplyDelete
  3. Replies
    1. Tulia ww! Anaanzaje?! Atapotea vibaya ampige mke mtarajiwa wa Yahaya?? Kwa taarifa yako km hujui alimuomba msamaha Zamaradi ndo kupata chance ya fiesta.

      Delete
  4. HUYO Inawezekana Hajapona, Bado ana2mi baddrug. MR.LOVE

    ReplyDelete
  5. na wewe wa wapi ruge sio yahaya ruge ni joto hasira, yahaya yupo mjini

    ReplyDelete
  6. madawa ya kulevya mabaya saaaaaaaaaaaaaaaaaana;

    ReplyDelete
  7. Unga bado upo kichwani,kwa huyo malaya pori

    ReplyDelete
  8. huyo Ray C ni mkorogo au ndio madawa kawa hivyo duh!!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad