POLISI 56 WAFUKUZWA KAZI KWA MAKOSA YA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

JESHI la Polisi nchini limewafukuza kazi askari wake 56 katika kipindi cha mwaka mmoja, kutokana na makosa ya kuomba na kupokea rushwa pamoja na utovu wa nidhamu.
  
Kamishna msaidizi wa jeshi hilo, Patrick Byatao, alisema hayo jana alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali hususan masuala ya nidhamu kwa askari wake katika warsha ya siku maalumu ya polisi iliyofanyika mjini Bukoba.
  
Alisema kuwa askari waliofukuzwa ni kutoka katika mikoa mbalimbali nchini ambao wamekutwa na tuhuma za utovu wa nidhamu ikiwemo kuomba rushwa kwa wananchi. Kwa kipindi cha mwaka 2012, waliwafukuza askari 35 na mwaka huu 21.
  
Kwa mujibu wa Byatao, wapo baadhi ya askari ambao wamekuwa wakitoa visingizio vya kuomba rushwa kwa sababu mishahara yao ni midogo na haitoshelezi mahitaji yao.
  
Alisema ni heri askari wa aina hiyo wakaacha jeshi, vinginevyo wataendelea kuchukuliwa hatua kama hawatafuata masharti ya kazi yao.

Akitoa mada juu ya kuimarisha maadili ndani ya jeshi hilo, Mrakibu Msaidizi wa Polisi kutoka makao makuu, Andrew Makungu, alisema wameanzisha mkakakati wa kudhibiti vitendo vya ukiukwaji maadili kwa askari wake ikiwemo rushwa.
  
Alitaja maeneo lengwa kuwa ni chumba cha kupokea taarifa za mashitaka, usalama barabarani na upelelezi wa makosa ya jinai. Bado juhudi zinaendelea ili kuboresha maeneo mengine.
  
Makungu alisema ubia wa kiutendaji wa jeshi hilo umekuwa ukiimarika kila siku baada ya sehemu kubwa ya jamii kutambua nafasi yao katika jukumu hilo. 
  
Alisema mambo hayo yanaonekana kutokana na wananchi kufanya ulinzi wa maeneo yao, kuchangia rasilimali kwa jeshi, kutoa taarifa sahihi za uhalifu, kujenga vituo vya polisi na kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi. Hadi sasa viko vikundi 5,344 nchi nzima huku Mkoa wa Kagera ukiwa na 431.
  

Naye mgeni rasmi katika warsha hiyo, Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe, alisema kuwa Jeshi la Polisi limekuja na mkakati wa polisi jamii/ulinzi shirikishi unaoelekeza kuwapo kwa mashauriano, majadiliano ya kiutendaji yanayosisitiza uwepo wa maadili katika kazi, ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa ndani ya jamii.

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad