WANAWAKE NCHINI SAUDI ARABIA KUANDAMANA KUPIGA SHERIA YA MWANAMKE KUTORUHUSIWA KUENDESHA GARI NCHINI HUMO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Leo October 26 2013 ndio Wanawake nchini Saudi Arabia wamepanga kuandamana kupinga wao kunyimwa kuendesha magari sehemu yoyote nchini humo ikiwa ni nchi pekee duniani ambayo inakataza Wanawake kuendesha magari hata kama wanaweza.
Unaambiwa kwa sasa Mamlaka za Saudi Arabia zimewaonya Wanawake hao kutoandamana  katika maandamano hayo yatakayokua ya aina yake na ya tatu kutokea nchini humo toka mwaka 1990 ambapo Wanawake kadhaa walikamatwa na wengine kuachishwa kazi, onyo hilo linakwenda pia kwa Mwanamke yeyote ambae amepanga kuendesha gari
Msemaji wa Serikali amesema Mwanamke yoyote atakae endesha gari leo atachukuliwa hatua za kisheria ambapo wakati siku hii ya kuandamana ikisubiriwa Wanawake kadhaa wa Saud Arabia tayari walishaweka video zao wakiendesha magari sehemu mbalimbali za Saudia lakini mpaka sasa hawajakamatwa.

Mpaka sasa zaidi ya watu elfu 17 wamesain kura ya ndio itakayo waruhusu Wanawake wa Saudi kuendesha magari ambapo pia idadi ya Wanaume wanaosupport imeendelea kuongezeka kwa kasi.
-Millardayo

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yaan mambo mengine bwana. unyanyasaji tu usio na kichwa wala miguu

    ReplyDelete
  2. Yaan kwel mdau. Sasa waliendesha tatizo nn? Sijui n sheria za din! Ni ujinga kwelkwel

    ReplyDelete

Top Post Ad