SIMUELEWI BINTI HUYU, AMENITENDA ILA BADO ANANING'ANG'ANIA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kuna binti (mwanachuo) ambaye tulikubaliana kuwa baada ya miaka kadhaa tutaunda kafamilia ketu, Baada ya miaka miwili ya mahusiano yetu (march 2013) nilipata tatizo la kusimamishiwa mshahara na ndani ya kipindi hicho huyo mrembo(aliyekuwa mchumba wangu) aliniambia kuwa anashida ya pesa, Nami kwa kusema ukweli sikuwa na kitu na ningefanyaje hali ya kuwa nishazoea kukinga kwenye ATM mashine tu! Nikampa ukweli kuwa nimevamba kwasababu sina mshahara ila hakuniamini, Akaanza kuniropokea maneno mi nikamwambia "usinisumbue kwani we si una wazazi na wanajua uko chuo? Waambie wakutatulie tatizo lako kama kweli ni la msingi."
Na ukweli wazazi wake hawana njaa sana. Ila baada ya hapo mawasiliano hayakuwa mazuri nami sikumfatilia kwasababu nilimuona sio muungwana, Yeye alikuwa ananipigia mara chache lakini maongezi yalikosa utamu ule uliozoeleka. Mwezi wa nane nilihudhuria mafunzo fulani yaliyonilazimu ninunue modem ya Airtel hivyo nikapata namba mpya ya simu na kwakuwa nilijiunga na vifurushi ktk laini hiyo mpya nilikuwa na muda na sms za kutosha. Jion moja nikamtext "Niambie mke wangu?" Akanijibu kwa ukali lkn nikamzingua had akawa mlain japo hakunijua mimi nani. Tukaendelea kuchat had ukafika muda nikamlazimisha aniambie mimi ni nani maana alishaniambia yeye ana mume mmoja ila alipotaja jina nusura chozi linitoke kwani alinitajia jina tofauti na langu. Nikakaa kidogo nikampigia aliposikia sauti yangu akapatwa na bumbuwazi akakata simu, nikampigia tena akapokea lakini hakuweza kuongea la maana alianza kulia huku akiniambia huyo aliyenitajia ni jamaa mmoja wa first year(ye ni 2nd yr). Alimtongoza tu walikuwa wanawasiliana na anamuita mumewe,baby ili tu amnyenge pesa zake ila hajasex nae hivyo nisiamue lolote. Niliamua kumpuuzia toka siku hiyo ila bado ananisumbua anaomba nimsamehe ili tutimize lengo letu. Kinachonisumbua zaidi sikubahatika kufanya maamuzi ya wazi nimekaa kimya tu nausikilizia upepo japo maisha bila mpenzi nimeyaona ya amani ila hayana furaha.


SASA WAUNGWANA NIPENI MAWAZO YENU:

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. (UKWELI WA MAISHA)
    mademu wazuri utaishia kuwaita shemeji.

    ReplyDelete
  2. duuh,huyo co m2 mzuri na inaonesha alikupendea 2 hela zako...xo km vp achana nae 2!

    ReplyDelete
  3. (nje ya box)

    Tafuta mwingine huyo mwachie nikk wa pili

    ReplyDelete
  4. Siku nyingine usitangulize kutamtangazia ndoa mtu usiyemjua tabia yake, jifunze.

    ReplyDelete
  5. Kama unataka furahaia maisha futa namba ya huyo mwanamke leo,

    ReplyDelete
  6. Mbona madem wote cku hizi wako hivo? wanapenda hela tu na wanakupiga mixer hata uwe tajiri kiasi gani, c unajua flavour mbali mbali za wanaume ndo shida yao, to explore what mens have. kama unadhani utakujapata dem katulia miaka hii, whether una pesa or not basi imekula kwako bora umgeukie mungu uwe padre tu usioe au kuwa na dem milele, wote ni mcharuko, kua utayaona mwanangu, hayo yako madogo sanaaaa, zungumza nae tu pengine ni foolish age tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dah dem malaika kabisa huyo hajamzingua kabisa dah akipata wa kumzingua itakuwaje !?
      Watu tumezinguliwa tukisema unaweza utamani kuishi dunia ambayo haina madem!
      Kweli bdo umri wake mdogo kwenye mahusiano .
      Dem mzuri kabisa hyo kwenye ulimwengu wa vicheche hayopo ata kwenye 1, 000, 000/= bora muweke ndani shauri yko !

      Delete
  7. Bora huyo mmezoeana nae m mwingine atakuzingua zaidi ila usiendelee kumpa pesa nyingi

    ReplyDelete
  8. Mdogo wangu wanawake wa kileo ni matatizo,wewe ongea nae tu hayo ni madogo sana nionavyo mimi,sisi wengine tukisema yetu hutatamani kuingia kwenye mahusiano zungumza nae umsikilize anachosema then uchukue maamuzi.

    ReplyDelete

Top Post Ad