UFOO SARO AELEZA TUKIO ZIMA LA SAKATA YAKE LILIVYOKUWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Ufoo ambaye mara kadhaa katika mazungumzo na gazeti hili alionekana kukunja uso akiashiria kupata maumivu, alionyesha eneo la chini ya bega katika mkono wake wa kulia lililofungwa na bandeji ambalo alisema ndipo alipopigwa risasi ya kwanza wakati akigeuka na kujaribu kuepuka mauti muda mfupi baada ya Antheri kumfyatulia risasi zilizomkuta mama yake mzazi.

Akijaribu kuvuta kumbukumbu ya tukio lilivyoanza, Ufoo alisema mzazi mwenzake huyo alifika nyumbani kwake akitokea Sudan alikokuwa akifanya kazi usiku huo huo wa tukio na akamtaka kwenda kwa mama yake (Ufoo) eneo la Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Kabla ya kufika Kibamba na kwa sababu ambazo Ufoo hakuzieleza, alimkariri mzazi mwenzake huyo akisema alikuwa amefikia uamuzi wa kujiua yeye na mtoto wao.

“Hata sijui ni nini kilitokea. Wakati tukitoka nyumbani Antheri alianza kwa kuniambia kwamba alikuwa amepanga kujiua yeye na mtoto wetu,” alisema Ufoo kabla ya kukaa kimya kwa sekunde kadhaa na kuendelea na simulizi yake ya kusikitisha.

Akiwa na sura ya ujasiri, Ufoo anasema pamoja na kumwambia maneno hayo bado Mushi alimsisitiza kwamba waende kwa mama yake (Ufoo) baadae warudi kumchukua mtoto wao japo Ufoo hakusema walitaka kwenda wapi baada ya hapo.

Alisema walipofika nyumbani kwa mama yake walikwenda moja kwa moja sebuleni na wakiwa wamekaa kwenye makochi baada ya salamu za hapa na pale ghafla Mushi akasimama akamwambia mama yake Ufoo kwamba; “Mama nimeishafanya maamuzi”  

Kwa mujibu wa maelezo ya Ufoo, baada ya Mushi kutamka maneno hayo ghafla akaingiza mkono nyuma ya suruali  alikokuwa ameweka bastola  yake na kisha akaichomoa.

Katika maelezo yake Ufoo alisema baada ya kuichomoa bastola hiyo mama yake naye alisimama na kwenda kujaribu kumpokonya, kitendo hicho kilimfanya amiminiwe risasi mfululizo.

Alisema kuona hivyo aliamua kukimbia kuelekea jikoni ambapo Mushi alimuona na kuanza kumiminia risasi ambayo moja ilimpata eneo la mkono wa kulia ambayo ilitokezea mbele na kuchana titi la kulia.

Kwa mujibu wa Ufoo jeraha hilo halikumfanya akate tamaa ya kunusuru maisha yake kwani alijaribu kukimbia ingawa Antheri alifyatua risasi nyingine kadhaa ambazo zilimpata juu kidogo ya mgongo na kutokea tumboni ambazo zilisababisha aanguke chini 

Akiendelea kusimulia, anasema ingawa alikuwa akivuja damu nyingi, na huku akijiburuza ardhini, Ufoo alisema wakati akitambaa aligeuka nyuma na akamuona Antheri akijielekeza bastola eneo la kidevu na alipofyatua risasi alianguka chini.

“Nikiwa chini nilimuona Antheri akijipiga risasi kidevuni na akaanguka chini, sikujua kilichofuata baada ya hapo kwani niliendelea kujiburuza ili kuokoa maisha yangu,” alisema Ufoo  

ALIVYOJIOKOA 

“Nyumbani kwetu, pale Kibamba si mbali sana na barabarani, wakati nikikaribia kufika barabarani wakati huo nikitokwa na damu nyingi huku nikihisi tumbo langu limejaa sana nilikutana na dada mmoja ambaye nilimuomba khanga ili nijifunge kuzuia damu zisitoke kwa wingi”. 

Anasema dada yule alimpa khanga akajifunga na aliposogea barabarani alikutana na gari lililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja.

“Nilipoona kuna gari linapita nikainuka kuomba msaada. Liliposimama nilimuona mwanamke akiendesha nikamweleza kwamba nilikuwa nimepigwa risasi na nilikuwa nikiomba msaada wake anikimbize hadi katika hospitali ya Tumbi na kwamba akifika pale tu aniache mlangoni.

“Si rahisi kuamini, yule mama alikataa kunisaidia akisema alikuwa akiwahi sehemu kumchukua mzazi. Sina la kusema niliamua kumsamehe tu yule mama ingawa niliumia sana,” alisema Ufoo. 

Alisema muda mfupi tu baadaye alitokea kijana aliyekuwa na pikipiki, maarufu kwa jina la bodaboda ambaye alimuomba msaada wa kumkimbiza hospitali ya Tumbi na akakubali.

“Yule kijana aliniuliza iwapo nilikuwa ninao uwezo wa kujishikilia vizuri na niliposema nitaweza akanisaidia kupanda katika bodaboda.

“Wakati huo nilikuwa naona kama tumbo linazidi kujaa. Nikiwa kwenye pikipiki kuna wakati nilikuwa nikihisi kwamba naweza nikaishiwa nguvu na kuanguka katika barabara na kisha kupitiwa na gari na kupoteza maisha. Lakini nilipata ujasiri na kujishikilia,” alieleza kwa sauti ya chini.

Alisema anakumbuka wakati walipofika eneo la Kibaha ilipo mizani ya kupima uzito wa magari makubwa walikuta barabara ikiwa imejaa magari na yeye alimuomba dereva huyo wa bodaboda kupita hata nje ya barabara eneo la nyasi ili kumwahisha hospitalini jambo ambalo kijana yule alilifanya.  

“Nilipofika eneo la mapokezi pale Tumbi nilimueleza muuguzi niliyemkuta kwamba nilikuwa nimejeruhiwa kwa risasi na nikamuomba asaidie kuokoa maisha yangu. Yule nesi alisita akitaka kwanza kupata kibali cha polisi (PF3) lakini nikaumuomba apigiwe simu, Kaimu Mganga Mkuu wa Tumbi, Dk. Dattan ambaye tunafahamiana” 

“Baada ya muda mfupi Dk. Dattan alifika na nikamweleza yaliyonipata na mara moja nikaanza kuhudumiwa kwa kuniwekea dripu, na nikamsikia akiwaeleza wauguzi kwamba isingekuwa busara kwa hali niliyonayo kama wangeanza kuchukua picha za X-ray kwani hatua hizo zingeweza kusababisha kupoteza maisha,” alieleza akikumbuka yaliyojiri hapo Tumbi. 

Kwa mujibu wa Ufoo, akiwa bado ana fahamu alimsikia daktari aliyekuwa akimhudumia akiomba msaada wa gari la kubeba wagonjwa ili limchukue na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wito ambao ulijibiwa kwa maelezo kwamba lilikuwa halina mafuta.

Majibu hayo kwa mujibu wa Ufoo, yalisababisha daktari huyo aombe kuletewa gari la wagonjwa la wagonjwa maarufu (VIP) ambalo lililitwa na muda mfupi baadaye akapakizwa tayari kwa safari ya kukimbizwa Muhimbili. 

Alisema wakati akikimbizwa Muhimbili anakumbuka namna alivyokuwa akipatwa na maumivu makali wakati wote gari ile ya wagonjwa ilipokuwa ikipanda matuta ya barabarani na kuna nyakati alikuwa akihisi kupoteza pumzi na kuishiwa nguvu. 

MTANZANIA 

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

46 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bulshit ukweli anaujua mwenyewe

    ReplyDelete
  2. Sisi hatutaki kujua wewe uliokolewaje,tunataka kujua ulimfanyia nn mushi mpaka anachukua uamuz huo?kani mushi alikuwa kichaa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. umeona ee mdau that what we want to know

      Delete
  3. Kwanza bora hujasema kisa,maana ungetudanganya ututie hasira tukupige mawe bure

    ReplyDelete
  4. Muongo mkubwa hata la maana halipo hapo!

    ReplyDelete
  5. Jamaa hawezi kuwa mjinga aseme atajiua yeye na mtoto bila sababu. We mwanamke mwizi mkubwa usie na aibu.

    ReplyDelete
  6. Hivi kweli upigwe risasi zote hizo utaweza kuhimili mikimiki ya boda boda? Na kweli mtu anakwambia anataka kuua mwanae na ye mwenyewe unachukulia simple? Kweli maelezo yake yana utata!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeona eeh! Huyu ukweli anaujua sema anaficha aibu tu!
      Mtu hawez kusema atamuua mtoto na yeye mwentewe bila sababu!
      Halafu watu wanataka kujua sababu ya mkasa wote, co yeye alivojiokoa!

      Delete
  7. Mmh... utata kweli

    ReplyDelete
  8. Sema ana roho ya paka risasi mwiluni muda wote huo duh

    ReplyDelete
  9. Jamani tusihukumu tusije tukahukumiwa! Hakuna kati yetu anaejua ukweli wa kikichotokea zaidi ya here say ambazo hazina uthibitisho. Kwanini sasa mumuone ufoo ndo mwenye makosa bila kuwa na uthibitisho? Mliona hizo hati za nyumba alizobadili majina? Mlikuwepo wakati ana shirikiana na mamake au yote hayo mnaongea kwa kusikia taarifa za kwenye vijiwe vya kahawa na viti virefu? No research no right to speak! Ambae hana dhambi awe wa kwanza kumpiga ufoo saro mawe!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe fala kweli, huna ushahidi je hata akili huna? Mushi ni chizi atoke Sudan na mshahara wote huo aje kumuua mtoto wake na mkwe na Ufoo just for nothing! unafikiria kwa kutumia makalio. issue hapa so nani ana dhambi na nani hana dhambi, suala hapa is why Mushi can come all the way from Sudan akaacha mshahara wa UN kuja kuua. Ufoo c mzuri wa kiivo wa kumfanya mtu ajiue labda kama ana extra qualities. Swali is Kamfanya nn Mushi na sio stor ya jinsi Mushi alivyowaua.

      Delete
    2. Dah unaposema sio mzuri wakati mwenzio kikojoleo chake ndo kilikuwa kinapata faraja hapo nakuona unakosea sana penzi si sura na kama kwako ufoo mbaya mushi alimuona mslaika upo hapo????

      Delete
  10. Ni muongo mkubwa! Sihara ye ndo aliyempiga mushi then mushi katika kujiami a

    ReplyDelete
  11. nilikuwa nampenda huyu mtu lkn kwa hili nimemchukia ila itafahamika

    ReplyDelete
  12. OYAAAA UFOO USTUZINGUE,HAKUNA ANAETAKA KUJUA ULIFIKAJE MUHIMBILI,TUNATAKA KUJUA KILITOKEA NN KATI YA WEWE NA MUSHI,TUNATAKA KUJUA NANI ALIYEANZA KUFYATUA RISASI NA CHANZO NI NINI,MAMAAKO ANAHUSIKAJE HADI KUKUTWA NA UMAUTI,TUPE UNDANI MAANA MUSHI HAKUWA CHIZI HADI KUFIKIA MAAMUZI MAGUMU..HAYO YA MUHIMBILI UTAWASIMULIA WORK MATES WAKO..JAMII INATAKA KUJUA CHANZO CHA HILI SAKATA HADI KUPELEKEA KIFO CHA MUSHI NA MZAZI WAKO..USITUZUBAISHE,GOLD DIGGER!!!!

    ReplyDelete
  13. pole dada Ufoo. hapa duniani hujafa hujaumbika. tusihukumu mungu mwenyewe ndiyo anayehukumu. ila hii ni kwa wote tuwe waangalifu sana tunapochagua wenzi wa maisha. si mwanaume wala si mwanamke.

    ReplyDelete
    Replies
    1. msenge kweli wewe kampe pole kwake kama dadako.

      Delete
  14. dada yangu pole lakini techenically atujakuelewa.haya ndio yale yakuzaa na mwanaume mwigine kumchomekea mtoto mwanaume mwingine.to story nyingine tukuelewe

    ReplyDelete
  15. Asante mdau hapo juu uliyesema habari za vijiwe vya kahawa, ni kweli kabisa hakuna sehemu kwenye uwongo na unafki kama sehemu hizo, tena kwenye vijiwe hivi asilimia kubwa no shule kama ujuavyo so uwezo wao wa kufikiri au kuchanganua ni mdogo sana zaidi ni kujazana pumba na kuzieneza mitaani kama unavyona hii ya huyu dada.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dah! Uwezo wakobwa kuona mambo ni F,

      Delete
  16. Jamii inataka kujua chanzo kilichopelekea maafa yote hayo, kwan haiwezekan m2 atoke sudan na kuja kukuambia anataka kumuua dogo&mwenyewe pia inasadikika kabla hamjaondoka kwenda kibamba kulikuwa na minong'ono je ilikuwa yanin?

    ReplyDelete
  17. Stoey hai add up, uambiwe ma mzazi mwenzio.nataa kuua mtoto.wetu unaacha kuarifu polisi unapanda gari unaenda kibamba? .kweli hata kutuma msg ya kuomba mssaada kwamba mume.wangu anasema anataka kuua mtoto na yeye? Yaani you will.have a hard time coming up with a story inayo.eleweka

    ReplyDelete
  18. Ufoo anajaribu kutafuta sympathy vote ndo maana anaweeleza story ndefu ya amefikaje muhimbili bottom line kama mushi hakuwa mgonjwa wa akili na alikuwa naendesha maisha yake bila tabu basi kuna sababu ya actions zake, watu wanataka kujua hizo.sababu sio habari za aliekunyima lifti na aliekubeba anyway get well soon

    ReplyDelete
  19. Ninyi wendawazim mnaotumia makamasi kfikria mnasema watu wanamhuku hebu achen ujinga wenu hapa,wangetaka kumhukum si angeuliwa na yeye? Au nyie ndugu zake ufo nn,pumbavu zenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huna haja ya kuwatukana yaa hao ni wale.wenye tabia kama.za huyu dada, hakuna hata anayemuhukumi Ufoo.ni kwamba tu wachache wenye uelewa nanaona the story behimd the curtains.

      Delete
    2. We anony hapo juu huna akili kabisa, Hakuna aliyemuhukumun ufoo wht we want to knw is "nini kilichopelekea mushi awaue? Na mama mkwe kaingizwaje? Na kama kulikuwa na maelewano mazuri baina yao kwa nini asiende kumuua mama yake mzazi aende kwa mama mkwe? Wewe huoni ilo tukio linautata na linapelekea watu kujiuliza maswali mengi?

      Delete
    3. We anony hapo juu huna akili kabisa, Hakuna aliyemuhukumun ufoo wht we want to knw is "nini kilichopelekea mushi awaue? Na mama mkwe kaingizwaje? Na kama kulikuwa na maelewano mazuri baina yao kwa nini asiende kumuua mama yake mzazi aende kwa mama mkwe? Wewe huoni ilo tukio linautata na linapelekea watu kujiuliza maswali mengi?

      Delete
  20. na nyie mnataka ukweli upi???na utawasaidia nini huo ukweli pumbu zenu kama ni wanume maana siono cha maana mnachozungumza mnataka ukweli nyie ndo familia ya mushi?mbona mnafikiria matako katika akili zenu yaone kwanza misura imewasinyanyaa kama mboo iliyotoka kutombana pumbavu kabisa...pole mwaya ufoo mwenyezi mungu na akuongoze utapona tu aliyetangulia kashaenda na kwa sababu imeandikwa kila nafsi itauonja umauti basi hata wewe pia zako zikifika utakufa tu na mushi siku yake ilikuwa imeshafika na iliandikwa atakufa siku moja sawa na mama yako mzazi kasoro dakika na sekunde tu.REST IN PEACE MAMA UFOO &MUSHI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Una akili ndogo sana unatukana ili.iwaje sasa, na umeishia kuandika pumba tu anyway, ndugu wa mushi wamesema.kuna jeraha zaidi.yya kidevuni na wanaomba ifanyiwe investigation, sasa.unakurupuka tu ma.matusi ili.nini grow.up

      Delete
    2. Na wewe kama si kutaka kujua au umbea nini kimekuleta uku? Ni vichwa vya habari vingapi umeviacha leo bila kuvisoma lkn hili umesoma hadi coment, hahaaaa si kutaka kujua huko ama na wewe ni familiavya mushi? Kwa hiyo babu wewe tutaoe radhi na iyo mitusi yako ya mtu ambae hajaenda shule na anaekurupuka

      Delete
  21. duuu!! pole cana dada, lkni inawezekanaje mtu kufikia uwamuzi paspokuwa na sbbu haingii akilini.

    ReplyDelete
  22. Hizo ni bangi za sudan.hata kama umekosewa kias gan huwez kufanya mambo ya kikatil kias hicho.huo ni upumbavu wa hali ya juu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unaongea ushuzi ww inaelekea nawe ni Gold Digger vile vile..Bangi za Sudan ulimvutisha ww???una uhakika ni Mushi ndio alifyatua risasi???siku nyingine funga mkundu wako kama hujui kitu..Kwa taarifa yako Ufoo na familia yake ndio walitaka kummaliza jamaa ktk kujitetea ndio na yy mauti yakamkuta,hujiulizi kwa nn Ufoo hakuomba msaada kwa majirani na badala yake akakimbilia barabarani kupanda gari???yy alikuwa keshatoka nje na majeraha sasa alijuaje kuwa Mushi kajipiga risasi ya kidevu???na ya bega ambayo yy haitaji lkn madokta wamemkuta nayo Mushi nani alimpiga???TAFAKARI SIO KUPANUA TU KUNDU KUONGEA USICHOJUA na jeshi la polis limeshasema Ufoo anakesi ya kujibu..Watch the space,Idiot.

      Delete
    2. Unauona ukatili wa Mushi lkn wa Ufoo huuoni???hivi mwanamke wa aina gani anamchuna mzazi mwenzie anaempenda kwa dhati,kumchukulia mali zake na kumhamishia mamayke??Mushi alikuwa akiishi maisha ya kujinyima Sudan na pesa zoote anatuma kwa Ufoo ili wajenge kwa maisha yao na mtt lkn hilo limwanamke likafoji kila kitu na kubadilisha ktk jina lake..Ungekuwa ww mwenzetu ungefanye???unajua uchungu wa kudhulumiwa jasho lako??hujui..sababu wewe pia unatabia kama za Ufoo...stupid woman,tena Ufoo alipaswa kufa yy lkn Mungu kampa 2nd chance ili aje kujutia na kutubia madhambi na laana yake ya tamaa...Wadada wote tunachuna lkn sio mpnz wako au mzazi mwenzio anaekupenda na kuteseka kwa ajili yako,tunachuna maboya yanayojiingiza kichwa kichwa....

      Delete
    3. Keeling lakini

      Delete
  23. Jamani hili suala ni gumu sana lililomtokea Ufoo,kwanza pale alipo hayuko sawa,vyombo vya habari muacheni kwanza apone ukweli utajulikana hakuna damu ya mtu inayomwagika bure,kama Ufoo ana mchango katika kumwagika kwa damu ya Mushi na mama yake mungu atamuhukumu hawezi kumuacha,na kama Mushi aliamua tu kujiua na kuua bila sababu nae asubiri hukumu yake,nawaambia ukweli Ufoo ukweli hawezi kusema hata mumfanyaje,ukweli anaujua yeye na mungu maana mushi ameshatangulia,lakini sasa hivi tutabaki kuongea ya kuhisi na ya kusikia,ukweli anao Ufoo na mimi naamini hawezi kusema kamwe!!! Ila kwa Mungu hakuna siri mungu anajua yote yaliyomsababishia Mushi kufanya maamuzi ya kinyama kiasi kile. Hatana sababu ya kutukanan humu ndani kwanza ni utovu wa nidhamu wewe unayetukana humu unaonyesha jinsi gani ulivyo huna hata hofu ya Mungu hata kidogo, kwanini unatukane matusi makubwa hivyo??Binadamu humu tunapita hatuna haja ya kuhukumiana ila tuombeane hata cha msingi huyu Ufoo tumuombee ili aijue kweli kama yeye ni sababu ya Mushi kufanya yote yale na yake yanakuja,malipo ni hapahapa duniani, Mungu hadhihakiwi.

    ReplyDelete
  24. hasani makono we msenge kinoma. unamsifia ufoo wakati yeye NDO KAUA???? UFOO HANA SURA YENYE MVUTO WALA NINI ILA KILICHOTOKEA NI YEYE NA MAMAKE MZAZI KUMRUSHA MSHIKAJI HELA ZAKE ALIZOKUWA AKIWATUMIA AKIWA SUDANI. MAAMUZI MAGUMU ALOCHUKUA MSHIKAJI NI BAADA YA KUDAI HELA NA KUAMBIWA HUNA CHAKO HAPA. HATA KAMA UNGEKUWA WEWE UNGEFANYA NINI????????? UFOO ALIPASWA AFE KABISA. TENA YEYE NDO ALIYEMPIGA RISASI MSHIKAJI KISHA AKAKIMBIA KUFUTA USHAHIDI. POLISI WETU WANGEKUWA MAKINI WANGEKUTA ALAMA ZA VIDOLE VYA UFOO KATIKA ILE BASTOLA. LAKINI KWA SABABU POLISI WETU NAO WENGI NI FOMU FOO KAMA UFOO ALIVYO BAS WALIKIMBILIA KUAMINI MAELEZO YA UFOO. ILA USHAHIDI UTAPATIKANA TU.

    ReplyDelete
  25. Cjaelewa maelezo hapo,, risasi alikua anapigwa ufoo baada ya kukwepa zikampata mama yake au mama alizani ile bastola ni sanamu akasimama mbele yake kutaka kumjaribu uvumilivu wake,, mhhhhhhh bado mvurugo upo kny maelezo ya tukia Zima,,, Mungu akuponye Ufoo, na yeye ndio atahukumu pale penye dhambi..... Ila cjapenda story ya tukio Zima hata kama ni stori za vijiweni,,hata wapelelezi wanapatiaga information kny vijiwe vya kahawa na kny stuli ndefu.

    ReplyDelete
  26. Maelezo feki tu non-sense haiingii akilini mtu kuwa na maamuzi magumu kama hayo kirahisi ivyo Ufoo anaficha tu anatupa hadithi za Shigongo. Mushi nae kama sio mjeshi sasa ye kichwa hakukiona ungemtia za shingo tu mbili basi ili tujue moja au za tumbo kumi ili liwe kama neti. Rest In Peace Mushi...

    ReplyDelete
  27. Asee Watanzania ni wanoko balaa, sasa mushi kutapeliwa au kujiua na kumkili mama mkwe inawahusu nini?

    ReplyDelete
  28. PF3 ZINATUUUUWAAAA.....................

    ReplyDelete
  29. UKIPONA TU MIE NAKUCHUMBIA NA NDOA JUU DADA UFOOO UTAKUBALI ETI...

    ReplyDelete
  30. Jamani kweli lazima tukubaliane kwamba Mushi hatujasikia kwamba aliwahi kuugua kichaa kwanini afikie hapo lipo lililompelekea hata mimi kama mwanamke nakiri wanawake tumekuwa wanyama sana kwanini kuangalia mali kuliko utu? Ufoo atuambie kwanini mwenzie afikie hapo ukwelia anao yeye ila hata asiposema Mungu atamuumbua tu!!!!

    ReplyDelete
  31. DADA UFOO. WASIKUZINGUE!!!!!!! WENYEWE WANAELEWA TABIA ZA WAMACHAME.MALI? MUME? IS EQUAL TO KIFO

    ReplyDelete

Top Post Ad