UFOO SARO AZUNGUMZA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mtangazaji wa Kituo cha televisheni cha ITV, Ufoo Saro, ambaye alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake Jumapili iliyopita, ameahidi kutoa ya moyoni atakapopona na kuruhusiwa kutoka hospitalini.
Ufoo ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kitengo cha moyo tangu wiki iliyopita kutokana na majeraha ya risasi, afya yake inazidi kuimarika na sasa ameanza kula mwenyewe na kufanya mazoezi ya kutembea.
Ufoo kwa sasa haruhusiwi kuonwa au kuzungumza na watu ovyo kutokana na ushauri wa daktari wa kutaka apumzike kwa muda mrefu.
Mtangazaji huyo alipigwa risasi mbili na mzazi mwenzake ambaye kwa sasa ni marehemu, Anthery Mushi, katika ugomvi unaodaiwa kuwa ni wa kifamilia ambapo mama yake mzazi Ufoo, Anastazia Saro aliuawa.
Akizungumza na gazeti hili jana katika wodi ya moyo, Saro, ambaye alikutwa na mwandishi wetu akiwa amekaa kwenye kiti, alisema anamshukuru Mungu kutokana na matibabu ya takribani wiki moja yaliyomwezesha kuanza kula chakula laini na kufanya mazoezi ya kutembea na kukaa.
"Na mshukuru sana Mungu, kwani sikutegemea kama mimi nitapona kutokana na kupata majeraha makubwa katika mwili wangu, kwani nilijua nitaiaga dunia,'' alisema.
Aliongeza kuwa, anawashukuru watu wote waliofanikisha kupatiwa matibabu hayo, na hali hiyo imesaidia afya yake hivi sasa kuzidi kuimarika.
Alipoulizwa kuhusu chanzo cha tukio hilo, Ufoo alisema kuwa hayupo tayari kulizungumzia suala hilo kwa sasa, lakini aliahidi kuzungumza siku ambayo atakuwa amepona kabisa na umma utajua ni nini kilitokea.
"Siwezi kusema kitu chochote sasa hivi ngoja nipone kabisa kila kitu nitakiweka wazi,'' alisema.
Naye dada wa Ufoo Julieth Saro, ambaye analala na Ufoo katika wodi hiyo, aliiambia NIPASHE kuwa hali yake (Ufoo) inazidi kuimarika kila siku kutokana na matibabu anayopata kutoka kwa madaktari wake.
"Tunamshukuru sana Mungu kwa kumuwezesha kupata matibabu ambayo yamesaidia hali yake kuzidi kuimarika kila siku na kuzidi kutupa matumaini sisi wanafamilia,'' alisema.
Afisa uhusiano wa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, aliiambia NIPASHE kuwa hali ya Ufoo inaendelea vizuri kutokana na juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na madaktari bingwa wa kitengo cha moyo.
Aliongeza kuwa Ufoo alipoletwa hapa hospitalini alikuwa ana hali mbaya na alikuwa hawezi kula wala kutembea, lakini baada ya kupatiwa matibabu hivi sasa anafanya mazoezi ya kutembea pamoja na kula chakula.
Alisema kuwa Ufoo anaweza kuruhusiwa muda wowote ule kutokana na hali yake kuendelea vizuri.
"Japo mimi siyo daktari wake wa kulizungumzia hilo ni lini ataruhusiwa, lakini anaweza kuruhusiwa muda wowote ule kutokana na hali yake kuwa nzuri, kwani hivi sasa anaweza kula na kutembea,'' alisema.

Oktoba 13, mwaka huu, majira ya saa 12.30 alfajiri, mzazi mwenziwe Ufoo, Mushi alimpiga risasi mama mkwe wake na kuumua, kumpiga risasi Ufoo na kisha kujiua mwenyewe.

SOURCE : NIPASHE JUMAPILI
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

22 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tunasubiri kauli toka kwako kwani mengi yanasemwa kuhusu mkasa mzima.Mungu akuponnye haraka

    ReplyDelete
  2. Get well soon UFOO SARO a.k.a GOLD DIGGER uje umalize sintofahamu iliyopo...

    ReplyDelete
  3. Nyie wasenge kweli, ingekuwa gazeti ningeelewa kichwa cha habari mna nia ya kuuza udaku wenu, sasa kwenye blog mnauza nini kama c ufala tu?
    Ufoo atoa ya MOYONI!? yako wapi!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli! Yan unaweza kuvutiwa na kichwa cha habari kumbe kilicho andikwa tofaut kabisa yan!
      Cjui wapoje?

      Delete
  4. Ukweli hatutegemei kutoka kwako,tumeshaupata ktoka kawa ndugu wa marem,we sema tujianda kudanganywa,maana familia yako haitakubal uongee ukweli ili idhalilike,tunajua utakaa na famimilia yako mtunge uongo mzuriiiiii,ili kujisafisha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yan umepatia mule mule!!
      Kama ulikuwepo,yan wanao subiri ukweli kutoka kwa ufoo watakaa san watu washa jua nini chanzo so watakao danganyika ni wachache,watu saiv washajua kwamba kilichosababisha co wivu wa mapenzi wala nin!

      Delete
    2. Mdau umenena!

      Delete
  5. well said mdau hapo juu

    ReplyDelete
  6. well said mdau hapo juu

    ReplyDelete
  7. 2nashukuru km afya yko inaendelea vzur!

    ReplyDelete
  8. ha ha ha ha ha ha ha Gold digger...

    ReplyDelete
  9. Uwezekano mkubwa huyu Ufoo ndio alitaka kumuua Antheri Mushi..Ufoo alipigwa risasi akajikokota hadi barabarani kutafuta msaada,alijuaje kuwa Mushi alijipiga risasi ya kidevu??na ya begani nani alimpiga??je alianza kujipiga ya bega ndio akajipiga ya kidevu au vipi ni vipi na muda huo Ufoo alikuwa wapi nje au ndani..Na walienda kwao kufanya nn kama sio kummaliza maana Mushi tyr alikuwa kishampa alert kuwa atafanya maamuzi magumu,na kwann Mushi amuue mama alikuwa na kosa gani???GOLD DIGGER TAMAA IMEKUFANYA UKOSE MAPENZI NA MZAZI..HAYA UTAKUMBATIA HYO NYUMBA YA MUSHI MILELE MAANA HAKUNA ATAEKUTAKA MUUAJI KAMA WEWE.

    ReplyDelete
  10. Hili ni somo kwa kina dada na wanawake woote,dont take for granted mwanaume anayekupenda kwa dhati,Money comes money life is important..Haya leo hii Ufoo ameweza kugushi na kubadili hati ya nyumba ya Mushi akishirikiana na mama yake lkn mama huyo huyo saivi ni marehemu whats the point?kwa nn usimuombe mpnz wako akusaidie?Mi nlishangaa saana eti Mushi kajiua kwa wivu wa mapenzi ha ha ha haaa huo wivu kwa Ufoo?Hicho ni kisasi cha kuzurumiwa mali yake,jasho la mtu linauma usiskie!Sasa Ufoo hata hyo nyumba utakaa kwa amani kweli bila ya kivuli cha Mushi kukusurubu..Itabidi usali na kutubu saana hyo ni laana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau nmeipenda hiyo. Kumbe chanzo mjengo... duuh hawa wanawake watatuua

      Delete
  11. bora na ww ungekufa tu coz unadhambi ambayo haitafutika milele.

    ReplyDelete
  12. Mi sielewi kwann hujafa na ww,ila nadhan mungu anataka ujifunze na uachane na huo ushetan wako,na hatutaki utwambie chochote mana najua utauddanganya uma

    ReplyDelete
  13. Tamaa mbaya jaman!wamachame tumebaki na sifa mbaya hasa wanawake hali yetu uraian ni mbaya!je tutasafishika?make karibia wote tumechafuka!Mungu tusamehe!haki itendeke na kama kweli alifanya kitendo hiki damu ya mtu haiendi bure!

    ReplyDelete
  14. wanacoment big up sana kumbe mnajua mengi niite ORUJONJOMOGO

    ReplyDelete
  15. Umenyimwa sura basi hata mapenzi ya dhati pia huna?khaaa kwanza kwa jinsi ulivyo kumpata kaka wa kukupenda ulitakiwa na wewe na umpende kikwelikweli lkn wapi..roho mbaya kama ilivyo sura yako unawaza mali tu,hujui kuwa zinatafutwa?Ufoo wewe ni aibu,laana na mkosi ktk kundi la wanawake!wenzio wanachuna mabuzi ww unamchuina mzazi mwenzio na mama yako anasapoti upuuzi huo,sasa mshahara wa dhambi ni mauti ila ww umabaki ili Utubu na ujutie ulichokifanya!SIKUONEI HURUMA..

    ReplyDelete
  16. msiwe hivyo jamani!! haya ni majanga yanamkuta mwanadamu ye yote kwa namna tofauti, Hivyo si vema kumuhumu Ufoo tumwombee Mwenyenzi Mungu mwingi wa rehema apone aweze kumlea mwanae.

    ReplyDelete
  17. WALA HAKUNA SABABU YA KUSILILIZA UJINGA NA UONGO WA HUYO UFOO: YOTE HAYO NI ROHO ZA WANAWAKE WA KIMACHAME KUPATA MALI.NENDA MACHAME AKINA MAMA WENGI HAWANA WANAUME,AKIWEPO ANA-STROKE AU AWE ZEZETA; BIG UP TO MACHAME BOYZ. ACHA ALAMBE RISASI NA MZIMU WA ANTERY HAUMTOKI. NAWAJUA WAMACHAME KIDOGO NITENDE LAKINI NILIMWACHIA MUNGU.YALINIKUTA.SHAME ON MACHAME LADIES.

    ReplyDelete

Top Post Ad