UNDANI WA ALIYEMPIGA RISASI UFOO SARO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MAISHA ya Anthery Andreas Mushi (40) anayedaiwa kumpiga risasi mzazi mwenzie, Ufoo Peter Saro, kumuua kwa risasi mama wa Ufoo kisha kujiua yeye mwenyewe, yameanikwa, Risasi Jumamosi inayadadavua.
Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu ambaye aliomba asiandikwe jina gazetini kwa sababu hakuwa msemaji wa familia, maisha ya Anthery akiwa Sudan kikazi yalikuwa ya kujinyima sana.
Alisema marehemu aliishi hivyo kwa lengo la kuhifadhi sehemu kubwa ya mshahara wake ili aweze kujijenga kimaisha kwa kuwa mpango wa kufunga ndoa na Ufoo ulikuwa upo.

ALIKUWA AKILA MARA MBILI KWA SIKU
Ndugu huyo alisema marehemu alikuwa akila mara mbili tu kwa siku yenye saa ishirini na nne, asubuhi ya saa tatu na usiku wa saa moja.
“Jamaa aliishi maisha ya kujinyima sana. Lengo lake lilikuwa kujiwekea akiba ya fedha za mshahara ili aweze kutengeneza maisha huku Dar.
“Mwaka jana alinitumia dola za Kimarekani elfu kumi (sawa na shilingi Mil. 16 za Tanzania) nimuwekee, lakini baadaye akaniambia nimrudishie ili amtumie mtu ambaye atampa maagizo ya ujenzi wa nyumba lakini hakuniambia ni nani wala nyumba inajengwa wapi,” alisema ndugu huyo.

HAKUWA NA MWANAMKE SUDAN
Ndugu huyo alizidi kusema kuwa marehemu hakuwa na mwanamke aliyekuwa akiishi naye Sudan kwa vile akili yake yote ilikuwa kwa Ufoo na alipanga baada ya kufunga ndoa angemfanyia uhamisho mkewe ili wakaishi wote nchini humo.

NDUGU WALISHAANZA KUONA MBELE JUU YA MAISHA YAKE
Habari zaidi zinadai kuwa, miezi ya karibuni alipenda kuwapigia simu baadhi ya nduguze na kuwapa malalamiko kuhusu uhusiano wake na Ufoo.
“Miezi ya karibuni alikuwa akitupigia simu baadhi ya ndugu na kulalamika kuwa kuna watu hapa Tanzania wamekuwa wakimtonya kwamba, wanasikia Ufoo anataka kuolewa na mwanaume mwingine.
“Tulimshauri kupuuza maneno ya watu kwa vile Ufoo mwenyewe hajamuwekea wazi au kama anaamini hayo maneno basi afadhali aachane naye kwa vile anaishi mbali, atakuwa akisikia maneno mengi kuhusu mzazi mwenzie huyo ambayo yatamuumiza.
“Lakini kuna siku alinipigia simu na kuniambia amefikia hatua ya kuchukua uamuzi mgumu kama mwanaume. Mimi nikajua labda atamuacha mzazi mwenzie, nilivyosikia hili la risasi nilishangaa sana,” alisema ndugu huyo.

MAITI YADAIWA KUTENGWA NA KANISA
Habari kutoka Uru Mawela, Moshi Vijijini zinasema kuwa, Kanisa la Roman Katoliki limeutenga mwili wa marehemu  Anthery kwa sababu alizaa nje ya ndoa. Marehemu ana mtoto mmoja aliyemzaa na Ufoo, anaitwa Alvin Anthery Mushi (10).
Ikadaiwa kwa sababu hiyo, mazishi yake yaliyotarajiwa kufanyika jana Machame, Moshi yasingekuwa na ibada au misa ya kumwombea marehemu.

UFOO ALIMTUMA BOSI WAKE AKAMUAGIE MWILI WA MAMA YAKE   
Kutoka Kibamba wakati wa kuuaga mwili wa mama wa Ufoo, Anastazia Saro, Mkurugenzi wa ITV na Radio One ambako Ufoo anafanyia kazi, Joyce Mhaville alisema alitumwa na mfanyakazi wake huyo kwenda kumwagia mwili wa marehemu kwa kuwa yeye asingeweza kufika.  
Joyce aliyasema hayo Jumanne iliyopita wakati akisoma hotuba fupi kwa niaba ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Abraham Mengi.

MTOTO WA MAREHEMU AWALIZA WENGI

Katika mazishi ya mama Ufoo yaliyofanyika Uru Moshi, Jumatano iliyopita, mtoto wa Ufoo, Alvin aliwaliza wengi kutokana na mazito yaliyowapata wazazi wake
-GPL
Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad